Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Waumini fulani wameamua tutafute ukumbi mahala mkuubwaa mahala panapofikika tutalipa wenyewe Kwa harambee au mmoja mmoja kwa siri.

Mchungaji Kimaro popote ulipo ujue Mungu anataka kukuinua pakubwa sana.


Be encouraged @ Pastor.

Mchawi hasa akiwa mwanamke ni mtu mbaya sana!
 
Huo usharika una mapato makubwa, pesa ndio tatizo, Huyu mchungaji, umaarufu umezidi kuzidi wakubwa wake, ameng'aa sana kuliko viongozi wa kanisa, Tatizo la Lutheran, ukiwa kwenye usharika wenye pesa ndefu, na wewe unanufaika zaidi, Gari, nyumba, miradi, kandarasi.

Mchungaji kwenye usharika mdogo, aina ya gari na nyumba itategemea mapato ya usharika, kama ni madogo, atanunuliwa hata bodaboda, ukiwa kwenye usharika wenye pesa, hapo V8, Prado, nk.

Kingine KKKT kuna ukabila sana, mchungaji akiwa mchaga, kandarasi zote zitaenda kwa wachaga, wahaya nk.

According to History, Makabila yenye Walutheri Wengi ni Wachaga(Marangu, Mwika, Pare, Same, Usangi, Ugheno Machame, Masama, Siha, na Old Moshi).

Arusha Mjini, Meru, Babati, Loliondo Karatu, Manyara, Kiteto. Singida, Baadhi ya Wanyiramba na Wanyaturu, Kagera :- Wahaya, Mbeya Tukuyu na Kyela, Iringa Mjini, Njombe Wabena na Wakinga, Tanga Wasambaa wa Lushoto. Maneromango Wazaramo wachache.

Kwa hiyo utaona Walutheri Wengi ni Wachaga, Wahaya, Wabena, Wanyakyusa, Wapare, Wanyiramba, Wameru, Wamasai , Wasambaa na Wakinga. Hayo ndio Makabila ya Tanzania yenye Walutheri Wengi.

Je ulitaka Kabila la wasio Walutheri washirikishwe wasipoabudu?
 
kwenye Biblia yako ya MAKABAYO,ila kwa sisi tunaosoma vitabu 66 , lipo:
wewe hapo umevaa sketi ya mtumba ambayo wazungu wametoa fungu la kumi, umevaa pedi ambapo ni msaada wenzio wametoa fungu la kumi, leo asubuhi umefanya tendo la ndoa[morning glory] na mume wako kwa kutumia Durex condom toka marekani ambapo ni fungu la kumi la wazungu kwa nchi maskini, acha mkono na roho korosho, lipa zaka.
Wazungu wanatoa fungu la kumi ili wewe uvae nguo? Hahahahah

Halafu unasema nilipe Zaka, Nilipe kwa nani anayenidai?

Fungu la Kumi ni fundisho la Torati kama mafundisho mengine ya Torati.

Nikikuambia hapa unioneshe ni wapi Mungu amekuagiza wewe utoe fungu la Kumi utakimbilia kunukuu Malaki 3:10-12 ambayo hata wewe mwenyewe huielewi.
 
Nilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.

KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli, sasa jamaa huwa yupo straight forward huwa hapindipindi hata kidogo, so kwa Lutheran hiyo ni kasoro, pia kuna ngoma nyingine Askofu Bagonza huyu nae ni kisiki hawana cha kumfanya make huyu nae ni kichwa kingine ambacho kimenyooka na hakuna mtu mwenye uwezo nacho ndani ya KKKT.
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Mashahidi wa Yehova, methodist, baptist, makanisa yametulia Sana haya.
Sema kizazi hiki wanataka makanisa yasiyokataza dhambi. Feel free church yaani haipo tofauti ya Mkristo na Mtu wa mataifa
Kuna kanisa lisilokataza dhambi?? Kama lipo hilo sio kanisa la Kristo bali wanajua wenyewe ni kitu gani. Hata Yesu alionya juu ya dhambi na kufa msalabani ili tutapoanguka turudi kwake kwa toba. Huyo asiyekataza hana ushirika na KRISTO.
 
Kuna kanisa lisilokataza dhambi?? Kama lipo hilo sio kanisa la Kristo bali wanajua wenyewe ni kitu gani. Hata Yesu alionya juu ya dhambi na kufa msalabani ili tutapoanguka turudi kwake kwa toba. Huyo asiyekataza hana ushirika na KRISTO.
Ujinga mliolishwa waafrika masalio ni janga la dunia,eti yesu alionya aache kuwaonya wazungu wenzie wasiwatawale na kuwauza WAAFRIKA kama watumwa ambayo ni DHAMBI kubwa kabisa aje akuonye wewe MWAFRIKA MASALIA?
 
Tusisahau Kanisa ni Taasisi. Ina kanuni na maadili yake. Kama hivyo vitu havipo Taasisi hiyo haiwezi kusimama.

Dr Kimaro na Mchungaji mzuri tu Lakini kubwa, ni Binadamu. Sifa kubwa ya Binadamu ni mapungufu na kijisahau. Hata Musa alipotumwa na MUNGU akapige Mwamba Ili maji matamu yatoke Wana Israel wanywe, alifika akajisahau kuwa alipewa maelekezo ya ni Cha kusema na kufanya akaenda kujitukuza yeye. Matokeo yake hata Nchi ya ahadi aliyokuwa akupeleka watu hakuingia.

KKKT ni Taasisi Ina uongozi na miundo ya uongozi. Sio Kanisa la Mtu mmoja kama Kakobe. Am sure Kuna mahali taratibu na maadili yalikiukwa na hivyo ni budi taratibu zifuatwe kwani Kanisa Linaongozwa kwa Neno Lakini pia taratibu za kanuni zilizowekwa na kukubalika.
 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo.

Leo rasmi ameaga usharika wa KKKT Kijitonyama Mch. Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga usharika wa KKKT KIJITONYAMA na kuanzia kesho Mchungaji Anna ataendelea kuwa Mchungaji wa Kanisa hilo, alisema Mchungaji Eliona Kimaro.

Kwa mujibu wa barua hiyo ilisema Mchungaji Kimaro atarudi tarehe 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT Kijitonyama ambapo atapangiwa sehemu nyingine.

Amesema:
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.

Lakini ukiangalia sana, hakuna chenye mwanzo, ambacho hakina mwisho. Safari njema Kimaro.
 
Mchungaji ukikaa Sana kanisa moja muda mrefu unajenga KIBURI na unaona kama pale ni Mali yako .Ndio maana madhehebu mengine kama sabato wanautaratibu wachungaji wanaamishwa baada ya muda Fulani ,unaweza Kuta hata ndani ya miaka 10 wamepita wachungaji hata 5
 
Wazungu wanatoa fungu la kumi ili wewe uvae nguo? Hahahahah

Halafu unasema nilipe Zaka, Nilipe kwa nani anayenidai?

Fungu la Kumi ni fundisho la Torati kama mafundisho mengine ya Torati.

Nikikuambia hapa unioneshe ni wapi Mungu amekuagiza wewe utoe fungu la Kumi utakimbilia kunukuu Malaki 3:10-12 ambayo hata wewe mwenyewe huielewi.
Mlicholishwa na kukalilishwa na MBWA WAZUNGU hamtakaa muione pepo kwani mnaamini ujinga wa waziwazi,MUNGU hawezi kutuletea wakoloni na dini eti watuokoe wakati huohuo watunyonye kupitia sadaka n.k tafakari!!
 
Kuna kipindi dayosisi haikuwa na katibu mkuu, kwa hiyo pastor wa kimara MASAI alipewa ukatibu mkuu kwa mda ili dayosisi ijipange kutafuta katibu mkuu.

Sasa kumbe wakati Masai amewekwa pale akakuta kuna mashtaka yanayo mhusu KIMARO kumbuka masai na kimaro ni pete na kidole, ikabidi jamaa avujishe siri kwa kimaro, sasa kwa sababu friji haigandishi ya kimaro akaja kanisani akasimanga akajisahau mpaka akamtaja mchungaji Anna, hapo ndipo siri ilipofichuka na kuonekana kuna kitu hakipo sawa kanisani.

Na baada ya ibada ile nahisi wakubwa waliona jamaa amevuka mipaka sasa wakaamua wamle kichwa, alipokua anaelekea alikua anataka kujiona Mungu.
Kuna kipindi dayosisi haikuwa na katibu mkuu, kwa hiyo pastor wa kimara MASAI alipewa ukatibu mkuu kwa mda ili dayosisi ijipange kutafuta katibu mkuu.

Sasa kumbe wakati Masai amewekwa pale akakuta kuna mashtaka yanayo mhusu KIMARO kumbuka masai na kimaro ni pete na kidole, ikabidi jamaa avujishe siri kwa kimaro, sasa kwa sababu friji haigandishi ya kimaro akaja kanisani akasimanga akajisahau mpaka akamtaja mchungaji Anna, hapo ndipo siri ilipofichuka na kuonekana kuna kitu hakipo sawa kanisani.

Na baada ya ibada ile nahisi wakubwa waliona jamaa amevuka mipaka sasa wakaamua wamle kichwa, alipokua anaelekea alikua anataka kujiona Mungu.
Nqdhani hapo Mchungaji Hekima zilipungua pakubwa .Unajua; RC,KKKT,SDA,morovian,Anglican nk.hizi ni taasisi.Ukiwa chini ya hizi taasisi lazima ufuate sheria na taratibu zake.Short of that wewe utakuwa unafanya uasi.Kwa hiyo kama ilivyo kawaida muasi yoyote hawezi vumuliwa.Kama ukitaka mamlaka binafsi anzisha ministry yako ,kama Lusekelo,kakobe Mwingila etc.
Ila tusiache kuwaombea watumishi wa Mungu wana Pitiaga magumu
 
Makanisa na migogoro ni sawa na samaki na maji.

Makanisa yote yemejaa changamoto, wakatoliki na ushoga na ulawiti watoto, waangillikano ushoga, walutheri sadaka na ukabila, wasabato ukabila, unafiki, walokole sadaka, ni balaa tupu.

Anyway, kama anaona hatendewi haki ajutenge na kanisa lake aendelee kufunisha watu wake kama kina kamobe, mwingira, Mama Rwakatale, yule mwingine alikua anafudisha wanawake tu na mapenzi, mxee wa upako nk.
Hajasema kutotendewa haki, amesema anatii alichoambiwa na wakuu wake ambae ni Askofu Malasusa. Hajasema ameudhika amesema anatii kiapo. Sasa huo ushauri wa yeye kuanzisha kanisa lake umetoka wapi pili ukabila unaouna kanisani KKKT ni upi? Kama wewe sii muumini wa kanisa hili shut up na kuwa mtazamaji mwema.
 
Huyo
Huyo mchungaji alizaliwa Kwa ajili ya kufanya Kazi hapo kimara pekee?? Anatolewa tu, na mikia yenu ya kichaga itakamata makalio tu
 
Huo usharika una mapato makubwa, pesa ndio tatizo, Huyu mchungaji, umaarufu umezidi kuzidi wakubwa wake, ameng'aa sana kuliko viongozi wa kanisa, Tatizo la Lutheran, ukiwa kwenye usharika wenye pesa ndefu, na wewe unanufaika zaidi, Gari, nyumba, miradi, kandarasi.

Mchungaji kwenye usharika mdogo, aina ya gari na nyumba itategemea mapato ya usharika, kama ni madogo, atanunuliwa hata bodaboda, ukiwa kwenye usharika wenye pesa, hapo V8, Prado, nk.

Kingine KKKT kuna ukabila sana, mchungaji akiwa mchaga, kandarasi zote zitaenda kwa wachaga, wahaya nk.
La ukabila nakubaliana na wewe kabisa!

Hasa wanyachusa na wachaga hakika hao jamaa ni noma.
 
Back
Top Bottom