Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo.

Mchungaji Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga Washarika wake na kuanzia Januari 17 Mchungaji Anna ataendelea kuwa kiongozi wa Kanisa hilo.

Kwa mujibu wa barua, Mchungaji Kimaro atamaliza likizo yake ya lazima 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT Kijitonyama ambapo atapangiwa sehemu nyingine.

Amesema:
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.

Mimi nilikua nasali kkkt kila j2.. na nilikua nasali Kariakoo Kimaro akiwepo.

Nilikuja kujua Askofu Malasusa amebadilisha katiba ili awe askofu milele nilichoka sana. Niligundua huyu askofu ni mroho na yupo kikaz sio kiroho nina miaka mitatu sijawahi kanyaga kanisani.

Huyu askofu ana figisu sana na alikua karibu sana na mwenda kuzimu. Kimaro anajituma sana anastahili kuwa juu na hayo matamshi yalikua ni mambo madogo tu ya kurekebishana..

Yule ni binadamu anaeituma sana... just imagine huamka toka Kimara hadi kanisani kwake saa 10 alfajiri kwa ajili ya morning glory
 
Sijaona kosa la mch. Kimaro
Mimi kama mlutheri tunataka mchungaji wa aina yake. Wengi tumechoshwa na aina ya mahubiri ya kutafsiri Biblia kama hadithi, ibada nyingi zinapooza ndio maana watu wanakimbilia kwa mitume na pentekoste.

Lutheran kuna shida sehemu nyingi, mchungaji akionekana yuko karibu na anakubalika na waumini anahamishwa.
Sasa hapa ndio waumini (wenye kanisa lenu) mnapaswa kupaza sauti na kutafuta njia stahiki za kubadili hiyo aina ya mahubiri iliyopo sasa. Kumuacha mchungaji huyo afanye kinyume na taratibu ambazo hazijabadilishwa huku mkisema mnafurahia afanyacho si sawa kabisa.

Hapo mchungaji wenu haonewi bali anawajibishwa kutokana na kukiuka sheria na taratibu ambazo hamjazipinga.
 
Du ukabila tena, mbona huajawazungumzia Mchungaji Kombo na wengine ambao sio wachaga? Mchungaji wa kimara sio mchaga sasa uchaga unatoka wapi. Askofu wao Malasusa Mnyakyusa wapi mzee unakoelekea??? Mbona unaleta tena chuki za kisiasa/kikabila kanisani?
Inshu sio mchungaji mchaga, inshu kimara wachga ndo wengi na usharika kama wamegeuza kuwa wao coz wananufaika nao, ndo maana wanaongea hakuna wa kumtoa huyo Maksai wao
 
Mimi nilikua nasali kkkt kila j2.. na nilikua nasali Kariakoo Kimaro akiwepo... Nilikuja kujua Askofu Malasusa amebadilisha katiba ili awe askofu milele nilichoka sana... Niligundua huyu askofu ni mroho na yupo kikaz sio kiroho nina miaka mitatu sijawahi kanyaga kanisani. Huyu askofu ana figisu sana na alikua karibu sana na mwenda kuzimu.. Kimaro anajituma sana anastahili kuwa juu na hayo matamshi yalikua ni mambo madogo tu ya kurekebishana.. yule ni binadamu anaeituma sana... iust imagine huamka toka Kimara hadi kanisani kwake saa 10 alfajiri kwa ajili ya morning glory
Ndo Kazi yake hyo.hta Kama angekuwa anatoka mbagala
 
[emoji120][emoji120]
IMG_20230117_133705.jpg
 
Hio haihitaji kujiunga na awali kujua kuwa wamemtoa kijanja... Hizo siku sitini wamezitoa wapi. Wakati likizo normal ni siku 28-30?!

Kwani si kaenda likizoo...!! Mchungaji kupewa likizo jambo la kawaida sema yeye ndo kayakuzaaa kuonesha kuwa kaonewaaa... aina ya wachungaji ambao usharika ukikuaa na wao ndo wameweka nguvu kuukuza huwa wana changamoto sana za kuongozaaa wao wako mbele sana kukemea ila ukweli na wao ni wachafu vile vile.
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Asante kwa taarifa lakini mimi si muumini wa hapo, mambo ya Sadaka ni ngumu kujua, nilichogundua kwa haraka ni ibada kuwa tofauti kabisa na ibada za kilutheri nilizozoea.

Sasa si muumini wa hapo tulia
Waumini wamesema wana shida nae?

Hakuna kinachopambaniwa pale korogwe zaidi ya sadaka
Watu mpaka wanataka kuuana
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Ubarikiwe kwa kusema kweli
 
Dayosisi imefanya maamuzi sahihi sana, na tena yamechelewa mno.

Huyu na mwenzake wa Kimara ni wachungaji wachache ndani ya kanisa wenye kiburi kilichokomaa na kuzeeka.

Mchungaji amekuwa mtu wa kusema hovyo ili kujipatia umaarufu wa kidunia, ni juzi tu ametoka kusema vijana wa kikristo hawaaminiki na yeye anawaamini sana vijana wa kiislam, hii sio kauli ya kusemwa na Mchungaji.

Mchungaji Kimaro kama kweli ana Mungu ndani yake, atumie hizo siku 60 kijitafakari na kufanya toba, kiburi chake kiliinuka zaidi na akataka kujitwalia utukufu wa Mungu.

Ni muda sasa KKKT iangalie sana watu wa kuwabariki kuwa wachungaji na kuwapa sharika, kutokana na ugumu wa ajira watu wengi wanapigania kuwa wachungaji ili kupata uhakika wa ajira hapo baadae. Kanisa lipime sana watu, lichuje kwa kumshirikisha Mungu.

Washarika wote wanamlilia Mchungaji wakae chini na wajitafakari kama ni wakristo kweli, wanaamini katika Mungu au katika Mchunga?
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Askofu Malasusa anatakiwa kuwa mkali kidogo, amekuwa mpole na imekuwa ni nafasi kwa wachungaji kujiinua na kuwa viburi.

Huu ni muda wa kuwaonyesha hawa wachungaji kwamba kanisa ni la Mungu na sio mali yao wala umaarufu wao si kitu ndani ya kanisa.

Wakiachwa watalivunjavunja kanisa.
 
Ndo maana mnadanganywa na kina Kimaro.Mussa na Eliya wapi na wapi?Baada ya Mussa aliinuliwa Joshua.
Binafsi simkubali Kimaro ni motivational speaker na si mchungaji.

Haishangazi!

Inategemea ukoje ndani!

Sasa kwa mfano unazani Mchawi atampenda Mtumishi wa Mungu @ Dada ?

Wafitina na Mahasidi ni wazi hawawezi Mpenda maana mioyo yao imejaa chuki!

Chuki na Pendo havikai you pamoja.
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Huu mgogoro usije ukawa kama ule wa KKKT Dayosisi ya Konde, Mbeya. Inabidi busara itumike maana hii migogoro kwenye taasisi za dini haileti afya kwa maisha ya kiroho ya waumini wake.

Rejea:

Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito​

Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (6.45 MB) ~ Free Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (04:42 Min) mp3 and mp4 ~ Download lagu mp3 & mp4 Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito...............
 
Back
Top Bottom