Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Halafu kunawakati alikuwa analipuka sana. Hatahivyo walimvumilia sana
 
Duuh kazi ipoo sema Ulimi ukiutumia vibayaa nao unashidaa sanaaa.. Huo huo.unahubiri dini leo huo huo kesho unaponda dini yako na watu wake wanaoiamini na kufata mafundisho unayowafundisha sasa sijui kipi ni kipi...!! Anyway kuusifu uislamu na ujatoliki ni kuonesha kkkt inazingua na hufurahii kuwa hapoo.
Hakika

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma uliyoandika hakika wewe unaweza ukawa ni sehemu ya hayo majungu

Ungeainisha ni sheria na taratibu zipi za kanisa jamaa kakiuka, naona hapa upo mgogoro mnaupika

Muda ni mwalimu mzuri kabisa,kama wewe uliona Mchungaji anakosea ulichukua jitihada gani, kanisani si kuna wazee, mlijaribu hata kumuita mkamuonya,,naamini angewasikiliza

Inaelekea na wewe ni miongoni mwa wale mliokuwa mnampigia makofi na kumshangilia akijeuka nyuma mnaanza kumnanga..

maisha ya bidadamu ni mafupi, tupendane, tusahihishane,tukosoane kwa staha,,badala ya kujenga jamii ya wanafiki.. kwani KKT DSm makanisa yapo mangapi kwanini waumini wengi wanene mara nyingi kuhusu KIJITONYAMA na KIMARA TU

Wakati mnamnanga tambueni YEYE NI MUANzILISHI WA IBADA zA ASUBUHI NA MASIFU YA JIONI KWA KKKT PIA NI MTU WA KWANzA KUANzISHA TV KABLA HATA YA UPENDO RADIO NA TV...
Ndugu soma vizuri uelewe, nimeongea mbona kwamba kila alipo teleza aliitwa akaonywa ila akitoka huko anakuja kanisani kurusha vijembe
Hakuna sehemu aliyo onewa sema ni kiburi chake tu kimemuondoa
 
Mother one....Alisha semakuwa mchungaji alionywa Mara nyingi na haku sikia kbsa na ilionekana ana kiburi Sana

SAS wee unasema habar za wazeee wa kanisa wakt Ni was kbsa jamaaa kuwa ana kiburi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Jamaa naon ni wale wenye mahaba na kimaro kila maelezo haelewi yeye anataka kusikia mambo ya kumsifia kimaro tu
 
Huo usharika una mapato makubwa, pesa ndio tatizo, Huyu mchungaji, umaarufu umezidi kuzidi wakubwa wake, ameng'aa sana kuliko viongozi wa kanisa, Tatizo la Lutheran, ukiwa kwenye usharika wenye pesa ndefu, na wewe unanufaika zaidi, Gari, nyumba, miradi, kandarasi.

Mchungaji kwenye usharika mdogo, aina ya gari na nyumba itategemea mapato ya usharika, kama ni madogo, atanunuliwa hata bodaboda, ukiwa kwenye usharika wenye pesa, hapo V8, Prado, nk.

Kingine KKKT kuna ukabila sana, mchungaji akiwa mchaga, kandarasi zote zitaenda kwa wachaga, wahaya nk.
Kwamba wahaya na wachagga ni Tisa na kumi?
 
Asante kwa ufafanuzi, mimi ni KKKT, sijaumizwa kimaro kupewa likizo, ninachojua unapokuwa mchungaji wa kkkt kuna viapo unaapa na kuahidi kuvifanya siku zote za utumishi wako. Ninachoomba kwa sasa akirudishwa kazini apangiwe usharikani kwetu😅😅😅
🤣🤣🤣🤣 sawa tutamleta huko niambie uko usharika gani tumtupie huko!
 
Nilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.

KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli, sasa jamaa huwa yupo straight forward huwa hapindipindi hata kidogo, so kwa Lutheran hiyo ni kasoro...
Swala sio kuwa kichwa au kuwa straight foward.

Kama kuna mahali amekosea amekosa tu.

Kwa kiapo chake nilazima atumie akili zake kwa manufaa ya kanisa
 
Babu unaongea nn jitahidi uwe na imani achana na kufungua makanisa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

ukileta za kuleta wanakususpend au ban na hakuna hata anayejua na wala wa kulalamika.
Ila kuna wale mapadri waliopatikana kwenye matenki ya maji, mwingine akaokotwa mtaroni huko Mbeya

Kimaro anajituma sana anastahili kuwa juu na hayo matamshi yalikua ni mambo madogo tu ya kurekebishana.. yule ni binadamu anaeituma sana... iust imagine huamka toka Kimara hadi kanisani kwake saa 10 alfajiri kwa ajili ya morning glory
Lakini si ndio maana ya utumishi?? Unamuonaje huruma mtu kwa kazi yake? Yaani utamuonea huruma mzibua vyoo, utamuonea huruma fundi wa umeme anayebembea nguzo moja mpaka nyingine kwa waya (zile za gridi ya Taifa)..hizo ndio kazi zao, huenda wenyewe wakasikitika kuona unawaonea huruma, ni kama unasema kuwa wanataabika kwa kazi zao

Nilikuja kujua Askofu Malasusa amebadilisha katiba ili awe askofu milele nilichoka sana... Niligundua huyu askofu ni mroho na yupo kikaz sio kiroho
Makanisa ni ya Kimafia sana, ila ni taasisi binafsi za watu, kwa hiyo ni sahihi wenye taasisi kujipangia watakavyo, hawalazimishi muwe waumini wao

Hizo siku sitini wamezitoa wapi. Wakati likizo normal ni siku 28-30?!
Wanataka ajipeleke CMA halafu wambane kuwa mambo yao yanatakiwa kusuluhishwa ndani ya kanisa kwa mujibu wa katiba yao
 
Nqdhani hapo Mchungaji Hekima zilipungua pakubwa .Unajua; RC,KKKT,SDA,morovian,Anglican nk.hizi ni taasisi.Ukiwa chini ya hizi taasisi lazima ufuate sheria na taratibu zake.Short of that wewe utakuwa unafanya uasi.Kwa hiyo kama ilivyo kawaida muasi yoyote hawezi vumuliwa.Kama ukitaka mamlaka binafsi anzisha ministry yako ,kama Lusekelo,kakobe Mwingila etc.
Ila tusiache kuwaombea watumishi wa Mungu wana Pitiaga magumu
Kweli mkuu
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Hatujaambiwa sababu ya mchungaji Kuchukuliwa hizo hatua. Mbona tunalaumu tuuuu
 
Huo usharika una mapato makubwa, pesa ndio tatizo, Huyu mchungaji, umaarufu umezidi kuzidi wakubwa wake, ameng'aa sana kuliko viongozi wa kanisa, Tatizo la Lutheran, ukiwa kwenye usharika wenye pesa ndefu, na wewe unanufaika zaidi, Gari, nyumba, miradi, kandarasi.

Mchungaji kwenye usharika mdogo, aina ya gari na nyumba itategemea mapato ya usharika, kama ni madogo, atanunuliwa hata bodaboda, ukiwa kwenye usharika wenye pesa, hapo V8, Prado, nk.

Kingine KKKT kuna ukabila sana, mchungaji akiwa mchaga, kandarasi zote zitaenda kwa wachaga, wahaya nk.
Asante kwa mawazo yako. Hatuna ushahidi wa hayo unayoyasema ila ni haki yako
 
Leo mchungaji Kimaro amepata mamia wa kumpambania kuwa ameonewa, kawaida ya watanzania ni kujadili jambo kwa siku lilipotokea. Kuanzia kesho Kimaro atajiona yupo alone na siku zifuatazo atakuwa alone kabisa, yeye na familia yake tu. Ajipange kupambana asitake huruma za watu mitandaoni, watanzania sio wa kuwaamini, wanakwenda na matukio.

Nimeona post zake instagram, replies zilikuwa chache isipokuwa ile aliyopost kuwa Mungu akimwinua mtu basi hakuna wa kumfuta, inawezekana uchache wa post ukawa ni muelekeo wa wafuasi wanaomsapoti, huenda akawa anaamini ana nyomi ya watu kumbe sivyo, atathmini na hilo kabla ya kufanya maamuzi ya kufungua kanisa (kama ana mpango huo)
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Na anahitaji kijitafakari haswa. Ndo maana ameondoka kwa upole. Anajua alipojikwa. Watoa maoni humu wanaangalia alipoangukia
 
Back
Top Bottom