Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Naomba kutia neno juu ya kile kinachoendelea mitandaoni juu ya mchungaji Kimaro.
Binafsi naona kama Kiburi kimemzamisha akiwa kati kati ya jahazi la utumishi. Alitumia madhabahu ya Mungu kujijenga yeye binasfi na sio MWILI WA KRISTO. Ndio maana yeye akawa maarufu kuliko utakatifu wa waumini wake. kumbuka kipimo cha kazi ya mwaadamu aliyeitwa na Mungu ni matunda aliyoweza kuzalisha.
Nimeona video ya waumini wake wakiwa na mabango, huku wale wa kike wakiwa wamevalia suruali za kubana makalio.biblia imezuia watu wa Mungu kuvaa mavazi ya aina ile ya waumini wa mchungaji kimaro. Mavazi ya kubana makalio yanachochea matamanio kwa baadhi ya waamini ndio maana biblia ikazuia. Lakini mchungaji kimaro hakuliona hilo. Naomba kunukuu maandiko matakatifu kutoka katika kitabu cha kumbukumbu la torati 22:5 Kumbukumbu la Torati 22:5 SRUV’’Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako’’
Alizungukwa na wana wa wanadamu wengi kuliko wana wa Mungu. Ndio maana kundi kubwa linalomtetea ni la WANA WA WANADAMU. Yaani makundi ya wanasiasa na wafanya kazi wa injili za biashara kuliko wateule wa Mungu.
Amenukuliwa katika video clip akilalama kua vijana wa kiislam ni waaminifu na vijana wa kikristo wengi ni wezi. Hii ni ajabu kwa mchungaji aliyeaminiwa aifanye kazi ya Mungu. Hii ni kukiri kua biblia haitoshi kubadili tabia na mwenendo wa wafuasi wa Yesu ispokua qurani, kitu ambacho kinaacha maswali katika aina ya utumishi wake. Wenye hekima wanasema nioneshe mchungaji wako nikwambie tabia yako. Tabia ya mchungaji ndio tabia ya waumini wake. Kama waumini wake ni wezi basi ni wazi kua yeye ni mahili kwenye eneo hilo pia.