Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Zamani enzi za mkoloni tukimaliza shule tulikuwa tunapewa leaving certificate,
sasa si hicho nacho ni cheti,au siku hizi hamna leaving certificate?,

mi kinachonitia shaka huyu makonda atakuaje Daud Bashije wakati bashije sidhani kama ni jina la kisukuma?,
hapa kuna watu wataumbuka wakifanya mchezo,kama makonda ni DAUD ALBERT BASHIJE na alichukua cheti cha PAUL CHRISTIAN,then jina makonda lilitoka wapi?,

babake na huyu mkuu wa mkoa anaitwa ALBERT BASHIJE au anaitwa MAKONDA?,

So mimi kuamini hii hekaya mpaka nilipate jina la babake na huyu mkuu wa mkoa,vinginevyo hapa kuna usanii
 
Jamani, pamoja na vyeti nk, lakini vita iliyopo mbele yetu ni madawa ya kulevya.tafadhali hata kama makonda aliishia chekechea,kama ana dhati ya kusaidia taifa liondokane na huu uchafu tafadhali apewe nguvu.kabla bw makonda hajaingia kwenye hii vita hatukusikia habari hii ya kufoji vyeti. Twaona magenge ya walanguzi na madalali wa unga sasa wameungana kumshughulikia kila eneo.tuacha unafiki tutokomeze hiili baa linaharibu vijana
 
Kuna sehemu mchungaji amesema "vyeti hivi ukihitaji unaenda baraza wanakupa tu". Kwa hiyo kesho mi naenda baraza wanipe cheti cha Pascal.
 
Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya raisi ni kweli ila kuongea maneno hayo siku ya Ibaada mazabahuni si sawa pia kakosa neno samehe 7×70 na ukuu wa mkoa si taluma hata la saba aweza kama anahekima na kipawa cha kuongonza
 
Mkuu, kwanza kubali kuwa mtumishi wa Mungu ana influence kuliko Rais, mfano kwangu mimi namtii Pengo kuliko JPM.

Pia kama unasema kuwa Gwajima kasema uongo, basi weka ushahidi wa vyeti vya Makonda hapa, pinga kwa hoja
 
Pasco, "Je mtumishi wa Mungu aweza kuwa zaidi ya raisi?" Jibu ni ndiyo. Walimuuliza Bwana Yesu swali hilo wakitaka kujua kuwa ni kweli yeye ni Mfalme wa Wayahudi? Jibu lilikuwa rahisi. "Ufalme wangu si wa dunia hii." Kuna realm nyingine tofauti na hii ya asili ambayo mtumishi wa Mungu katika hiyo ni zaidi ya raisi.

Kwa kuwa watawala wale hawakuelewa hilo, waliamua kumuua Yesu. Swali lingine. "Kwa nini Gwajima anakasirika kiasi hicho cha kumwita binadamu mwenzie hivyo?" Jibu, "Haipendezi kabisa kwa namna yoyote kumsingizia binadamu mwenzio kuwa ni muuza madawa ya kulevya." Zaidi sana haipendezi kumsingizia kiongozi wa dini yoyote jambo hilo tena mbele ya vyombo vya habari. Hata wewe ungekasirika na kuudhika kama lingelikutokea. Lakini kama likikutokea lazima ufanye juhudi ya kuosha uchafu uliopakwa na kujihami kwa maana mshindani wako ni kiongozi wa serikali! Huo uchafu unauosha mbele ya "familia" yako ili waendelee kukuamini kama kiongozi wao.

Makonda pia karushiwa dongo. Kuna watakaoliamini kuwa alifeli na akawa anatumia cheti cha mtu mwingine. Hana budi kujitokeza hadharani na kujisafisha mbele ya umma ili tuweze kuamini kuwa hizo ni mbinu za wauza madawa ya unga.
 
Unabisha Mtumishi wa Mungu sio mkubwa wakati Viongozi wote wakifika mbele yao hupiga magoti na kuombewa. Tafakali upya mambo ya rohoni na Imani usijikwaze kisa unavuta pumzi utapata laana.
 
Pascal Mayalla,

Kabla ya kuanza kumchambua huyo Nduguyo Msukuma mwenzio Mchungaji Gwajima naomba kwanza tuanze na Wewe kwa kukuuliza kwamba mbona siku hizi hueleweki halafu naona kama vile kuna Vitisho umevipata au Maslahi yako yameshaanza kuguswa kwani baada ya ujio wako ndani ya miezi miwili ya kuisema Serikali ya Awamu ya Tano ( 5 ) kuanzia Rais na Watendaji wake akiwemo Daud Albert Bashite ( sasa Paul Christian Makonda ) kwa wiki hizi mbili tatu naona na Wewe umeamua tena kubadili gia angani ghafla kwa kuanza kujikosha kama siyo kujipendekeza kama siyo kujikolombweza kwa Utawala ule ule uliokuwa na naamini bado unauchukia.

Najitahidi kukutofautisha Wewe na Steve Nyerere lakini ninashindwa sijui kwanini.
 
Kwa hili mimi sina shaka hata chembe ninaiamini serikali uangu kama yanayosemwa yanaukweli basi hatua stahiki zitachukuliwa very soon!!!
 
Back
Top Bottom