Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mimbara ni sehemu takatifu, sio jukwaa la kutolea mipasho. Gwajima kama mlezi wa kiroho alitakiwa kumwita Makonda na kuongea naye kama alihisi alimkosea na sio kutumia mimbara kumkamshifu kondoo wake.

Jmabo jingine kwa kweli wafuasi/waumini wake waliokuwa wakishangilia inabidi wapimwe akili. Yaani utadhani sio kanisa bali ni kijiwe flani hivi.

Mambo kama haya yanawafanya watu makini kuendelea kumtilia mashaka na utumishi wake kila leo. Na uhakika kabisa kuwa hatutaacha kusikia mengine kumhusu yeye. He doe not behave like a Man of God.
 
a33b3b7ca75cd8516b228acb0569f9fe.jpg

I guess ana matokeo kama haya
tehe tehe tehe uwiiiiii nimeona jina la shangazi yake mdogo mjomba wa bibi
 
Kwamba Msigwa na Getrude (wachungaji) walijidemote! Na mchungaji Jesse Jackson (US) alitaka kujidemote! Fweza nazo zinalewesha!
====
Mkuu Paskalli, naomba umuulize (Gwajima) utaratibu alioutumia kupata vyeti vya Makonda, wakati tunajua vyeti vyote vya viongozi wa serikali nakala ziliwasilishwa 'serikalini ' na original vilibaki kwa wamiliki halali wa vyeti hivyo.
kuvipata ni kazi rahisi sana, Gwajima si mtu mdogo atiiiiii ni ukizingatia humo ndani kwenyewe kuna bonge la kutoelewana
 
Yaliyo ya Kaisari mpe Kaisari, alinena Kristo.

Kwa sababu hiyo kila amwaminie Kristo, kwa maneno na matendo, hutii mamlaka zilizo duniani. Mchungaji Gwajima hakika anajikuza na kuwadanganya wafuasi wake.

Hukumu yetu wote, iko baada ya kutoka duniani
 
Nawe umerudia yaleyale ya Gwajima, umehukumu. Tafiti, yawezekana Gwajima yupo sahihi. Dunia hii ina jambo moja la ajabu ambalo wengi wetu tunapopanda kimadaraka au kupata fedha tunasahau kwamba kama tunavyowajua wengine ndivyo na wao wanavyotujua. Tulizaliwa na kulelewa huko vijijini na watu wanatujua. Yawezekana madai ya Gwajima yasiwe na mashiko kwa sasa, lakini Paschal, elimu yetu Tanzania hasa hasa kati ya miaka ya 70 na 90 ilijaa magumashi tu, na hili la kutumia majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida. Leo hii ukizungumzia mwenye jina lake halisi kwa waliosoma kipindi hicho utachekwa sana kwa sababu kuchukua majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida, kwa hivyo sishangai kuyasikia haya maana ndo ulikuwa mtindo wakati huo--kukariri madarasa kwa majina ya wanafunzi watoro, wagonjwa nk. Kwa hiyo hili la Makonda kama ni kweli mimi sishangai, na watu wa aina hii wapo wengi tu, iwe serikalini au sekta binafsi. La Makonda linakuzwa tu kwa vile kagusa madawa ya kulevya!!
Na pia kwa sababu ametumia mwavuli wa madawa ku deal na personal issues zake
 
AMETAMKA MUBASHARA KUWA MUHESHMIWA RAISI AKIMKINGIA KIFUA MKUU WA MKOA NAE ATAKWENDA NA MAJI,! NI UHAINI WA WAZIWAZI KABISA!
INAELEKEA JAMAA NI ZAIDI YA RAISI KAMA ANAVYOJINASIBU
 
watu hawa msingizii asee kwa kuwa kamwaga ugali sasa watu wameamua kumwaga mboga.hivi kwn mnadhani hakuna watu waliosoma na makonda tangu awali.au wamekufa woote??vipi kitaani aliokuwa anaishi nao wamekufa woote??

acheni ulofa watu wanamjua vzr tuu.huwez kuwafanyia vbya watu wakakuangalia tuu.tanzania ya leo sio ya jana watu wameenda shule mpk kero
Hicho ndicho cha kujiuliza .......... hivi kweli huko Kolomije wakati akiitwa Daudi hakuna kijana aliyesoma na Makonda na leo ni mwanachama wa JF!!

Huko Pamba secondary nako hakuna watu waliosoma naye ambao leo ni wanachama wa JF!!?

Anyway, data za Gwajima zitakuwa na asilimia kubwa ya ukweli kwa vile wanatoka kijiji kimoja. Kuna thread niliandika huko nyuma kuwa nasikia hawa jamaa wawili wanatoka kijiji kimoja kuna mtu alinibeza.
 
Paskali ninaekufahamu au mwingine?
Hoja ya kufoji vyeti haina uhusiano kabisa na uhubiri wa gwajima... Msitutoe kwenye hoja ya msingi... Gwajima wakati anatuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya alijitokeza akajibu tuhuma na akasema anaruhusu serikali ifanye uchunguzi itoe taarifa... Serikali ikakiri kuwa ni safi.. Makonda anatuhumiwa kugushi vyeti anapaswa atoke hadharani au akanushe kwa sbb kubwa mbili..
Yeye ni kiongozi wa serikali hivyo tena mkubwa, kubaki kimya anatoa mashaka kwa taifa juu ya umakini na usafi wa nchi...
Mbili, makonda amekuwa akijinasibu mbele ya uso wa taifa hili kuwa anataka watu Smart,wasio hovyohovyo. Anapaswa kuwa safi zaidi kuliko yeyote... Paskali acha kuchanganya mambo, gwajima kasema kweli na MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU.
 
Hayo majina jamani mnampakazia muheshimiwa naona mazito daudi Albert bashite khaa! Mleta mada we unawezaje mtambua mtumishi wa Mungu wa kweli?
Kuna "video clip" ya Mzee Makonda na mke wake, wazazi wake RC Makonda, vipi hilo jina baba mtu nalo ni 'fake'.

Yawezekana majina na vyeti alivyosema Mchungaji, kuwa anavyo, ni vya watu tofauti kabisa.

Labda kama kuna au kulikuwa na mtu mwenye jina la Paulo Makonda, Mchungaji, katika "MAHUBIRI" !!! yake, hajasema lolote kuhusu kuwepo kwa mtu huyo. Hivyo "profile" ya Paulo Makonda hana.

NI UTATA MTUPU TUHUMA HIZO
 
Back
Top Bottom