Mchungaji Hananja akihojiwa na Bongo5 (ingia YouTube, kaongea nusu saa nzima) ameeleza uonevu mkubwa wanaofanyiwa na viongozi wakuu wa kanisa, na anasema yeye aliandikiwa barua na kiongozi mkuu wa kanisa kumsimamisha kazi bila mshahara kwa mwaka mzima, bila sababu yoyote ile.
Hananja anasema alikataa barua ya kiongozi mkuu wa kanisa kwa kuwa si muajiri wake,
Hananja ameeleza kwamba kanisa linapitia maumivu makubwa kwa sababu ya unyanyasaji na roho mbaya sana, na visasi walivyonavyo viongozi wakuu wa kanisa Hilo.
Hananja ameeleza kwamba viongozi wakuu wako katika wimbi kubwa la kuuza viwanja vya kanisa, na wachungaji wanapohoji, wanafukuzwa na kunyanyaswa sana.
Kuna taarifa kwamba mchungaji Kimaro, kupitia Utumishi wake, kijitonyama imenunua viwanja vya mamia ya mamilioni, na kujenga majengo ya thamani kubwa, na kuna hisia kwamba wakuu wa kanisa wanataka kuviuza waweke Hela mfukoni.
Kanisa pia lilikuwa na hotel huko matema beach, hotel ambayo viongozi wakuu wa kanisa waliweka dhamana ili kupata mkopo wa mabilioni wa kujenga chuo kikuu, mkopo ulitolewa na fedha yote ikabebwa na wakuu wakanisa, benki walivyoanza kudai deni, wakuu wa kanisa harakaharaka wakatafuta mteja waiuze kwa bei ya kutupa. Mwaikali alipokataa hoteli isiuzwe, alitengenezewa zengwe na kufukuzwa kama mbwa, yaani askofu anafukuzwa kama mbwa na kulazwa rumande!
Pia yamekuwepo malalamiko kwamba shule za kanisa zinadorora, ada na fedha za wafadhili zimefanya wakuu wa kanisa wawe mabilionea wakiogelea kwenye fahari kuu. Na hata hospitali ya seliani Sasa ni mlango wa kuzimu, kwa kuwa haina huduma nzuri, na ukipelekwa pale, ni sawa na kusaini hati ya kifo