Mchungaji Hananja: Wachungaji KKKT wakihoji vitendo vya viongozi kuuza Mali za kanisa, wanafukuzwa, asema na yeye alisimamishwa mwaka mmoja

Mchungaji Hananja: Wachungaji KKKT wakihoji vitendo vya viongozi kuuza Mali za kanisa, wanafukuzwa, asema na yeye alisimamishwa mwaka mmoja

Mazito gani? Zaidi ya kulalamika kwamba alisimamishwa mwaka mzima. Ukumbuke kwa Sasa Hananja sio MKKKT anaweza kuongea lolote ilimradi alichafue kanisa.
Mbona mipovu sana jombaa?
 
Mimi ni MKKKT na hicho ukichosema kuhusu katiba ni ukweli mtupu na nmekuwa nikisema kila siku.

Angalia mfano yule Bagonza wa karagwe jinsi alivyo na mapembe!

Yani KKKT ni moja lakini humo ndani ina vipande vingi balaa.
Yule anajitambua sanaa acha kumchafua banaa
 
Wale wazee wa "kanisa inabidi kuwa taasisi" sasa hivi comments zao zimebadilika
 
Hakuna mtu anaweza kuliumbua kanisa, hii ya Kimaro imekwisha na acheni kujifariji.

Mwaikali na kundi lake walidhani wana watu na wakadhani wakihama watahama na waumini wote wa Dayosisi ya Konde, kiko wapi leo?

Kimaro ametii mamlaka yake na kiapo chake, acheni kelele. Hata kama akiamua kwenda na kuanzisha huduma binafsi, atakwenda na ataliacha kanisa.

Mungu hawezi kukubali kanisa liumbuke kama mnavyodhani, umaarufu si kitu mbele za Mungu.
Hañanja Ni kiboko na nusu, haogopi mtu
 
Acha kumtukana Askofu Shoo.
Hapo amehusikaje ?
Malasusa ndiye anayehusika na Dayosisi ya Mashariki na Pwani na ndiye anayemsimamia Dr. Kimaro.

Kanisa la KKKT Lina katiba mbovu sana na ndiyo inayosababisha migogoro na wizi mkubwa ndani ya kanisa Hillo. Kanisa la KKKT ni Mali ya Maaskofu . Kila mmoja ana sharubu. Yaani Dr. Kimaro ni WA Malasusa na sio wa Dr.Shoo. Dr. Shoo Hana maamuzi yoyote juu ya Dr.Kimaro. Askofu mkuu alipaswa kuwa na mamlaka makubwa juu ya maaskaofu wote wa KKKT na kuweza hata kuwahamisha kwenye Dayosisi nyingine. Ndio maana Vitega uchumi vya KKKT vinakufa kila mahali Kwa sababu wengi sio waaminifu na hawana sifa za kusimamia miradi Hi hiyo

Mchungaji Hananja alinyimwa mshahara mwaka mzima, imagine, wanaomnyima mshahara ndio wanahubiri amani na upendo, kusamehe mara sabini.

Bila shaka kikombe hiki atakipitia mchungaji Kimaro mbele ya hawa watu wasio na huruma.

Mwenye connection na Dk. Kimaro amuulize atupe namba tumchangie wakati huu ambao viongozi wake wa kanisa wamejiapiza kumtesa yeye na familia yake.
Ninachokiona ni watu kuwa emotional kupitia kiasi. Mchungaji mzuri hata akinyimwa mshahara Nina uhakika ataishi tu, tena vizuri mno. Nimekuwa kwenye uongozi wa kanisa, mishahara ya wachungaji ni midogo sana, hata kwa wale wanaojua wito wao na kutumika kweli, wako vizuri na wanawazidi hata baadhi ya maafisa wakubwa serikalini. Mungu hawezi kumuacha mtu anayemtumikia kwa uaminifu adharirike hata kidogo. Zaburi37:25 inasema "Nalikuwa kijana na Sasa ni Mzee,sijawahi kumuona mtoto wa mwenye haki akiomba chakula". Sasa hao kina Hananja sijui tuelewe nini, kuwa mchungaji ni wito mkubwa sana na ndani yake Kuna baraka kubwa sana.
Itoshe kusema hata Mchg. Kimaro asijidanganyike kama anavyohamasishwa Sasa eti aanzishe kanisa lake, hata yeye anaweza kuwa mbaya zaidi ya hao, anawaona wabaya Sasa.
Kama alifanya kazi kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu, awe na hakika,haya yatapita.
Nimemsikiliza Mchg. Hananja, ukweli Kuna maeneo kasema kweli, kwamba tutafute njia nzuri ya kutatua matatizo yetu pasipo kuleta taharuki,lakini siwezi kuamini eti alisimamishwa mwaka mzima na hajui kosa lake,hapo Pana walakini.
Kwamba waumini walimzomea akabaki mwenyewe, mmh basi hata hao waumini walikuwa wamemchoka kwa hayo asiyotaka kuyasema.
Mchg Kimaro kapewa likizo ya siku 60 kwa sababu ambazo hatuzijui, na hata alipohamishiwa Kijitonyama, Sidhani kama waumini waliambiwa sababu ya yule aliyekuwepo kuondolewa.
Inawezekana kabisa viongozi wakawa na mapungufu,hata hivyo lazima wana sababu kubwa iliyowasukuma kuchukua maamuzi waliyoyachukua.
Wengine wanasema huduma yake imekuwa kubwa hivyo anaonewa wivu, binafsi siamini katika hilo. Kama karama anayo atabaki kuwa nayo tu. Mbona Mwalimu Mwakasege haonewi wivu na yeye ni mlutheri mkristo wa kawaida tu.
Mchg Kimaro amepewa mtihani na kushinda mtihani huu, asitafute huruma za waumini wake Bali aombe Roho ya unyenyekevu zaidi, na Mungu atamheshimu.
 
Dr. Mbilu ndo amemrithi Dr. Munga?
Ndo mkuu.
Ni MTU makini sana. Hua nafuatilia sana mahubiri yake na mabadiliko makubwa ya kimtizamo aliyoyafanya . Lakini pia ni MTU mtulivu sana na anaongea Kwa mamlaka bila kuyumba.
Aliikuta Dayosisi IKIWA na madeni makubwa sana . Ajira za upendeleo. Na Kila aina ya ufisadi kwenye miradi.

KKKT ina tatizo kubwa sana la kimfumo na pia ni kanisa lenye Viongozi wengi wasio na maadili. KKKT ni Mali ya maskofu Kila mmoja na Dayosisi yake binafsi.

Dayosisi Tajiri kama ya Mashariki na Pwani basi na askofu wake na wachungaji wake watakua mabilionea. Dayosisi maskini kama za Kusini HUKO Lindi basi na maaskofu wake watakua maskini.

Watumishi Wa Mashariki na Pwani wanashindana kuwa na maisha ya kifahari na majengo ya Vitega uchumi wakati huo huo wale Wa KULE umasaini na Lindi na Mtwara HAWANA Hata uwezo Wa kujenga nyumba ya Ibada. KULE kaskazini wanashindana kujenga mavyuo Kwa sadaka za Wakristo lakini hakuna mpango Wa kimkakati kama KKKT nchi nzima kuwainua waumini Wa Maeneo yenye mazingira magumu Ili watumishi wao wafurahiye zaka za mabilioni Zinazotolewa na Waluteri Wa Tanzania.
 
Hakuna mtu anaweza kuliumbua kanisa, hii ya Kimaro imekwisha na acheni kujifariji.

Mwaikali na kundi lake walidhani wana watu na wakadhani wakihama watahama na waumini wote wa Dayosisi ya Konde, kiko wapi leo?

Kimaro ametii mamlaka yake na kiapo chake, acheni kelele. Hata kama akiamua kwenda na kuanzisha huduma binafsi, atakwenda na ataliacha kanisa.

Mungu hawezi kukubali kanisa liumbuke kama mnavyodhani, umaarufu si kitu mbele za Mungu.
Tukubali tu kuwa kuna kundi kwenye Hizi taasisi ambalo halitaki mabadiliko . Hawa Hata HUKO SERIKALINI Wapo hawataki Katiba mpya .
Kuna watu wanatumia Taasisi za Dini kutafuta umaarufu. Wengi wao ni walevi ,washirikina ,Wazinzi na Wezi. Bahati Mbaya ni watu wenye ushawishi Mkubwa na FEDHA nyigi HARAMU . Sasa akitokea Mchungaji anayekua kikwazo kwao wanatumia mabaraza Yao kumkwamisha au kumshughulikia.

Kwa nyakati Hizi zile Injili za Zamani za kuogopa kuwakwaza waovu eti hawatato Sadaka hazina nafasi Tena. Kwa Sasa Injili ya kweli ndiyo Kila kitu na fungu la kumi likitolewa Kwa uaminifu Hata maskini wanatoa Kwa Baraka kubwa sana.
Zamani watu walidanganywa kuwa kanisa haliwezi kendeshwa na walokole mana HAWANA pesa. Kwa Sasa Mungu kwanza watu wanajitoa kuwatunza wachungaji waaminifu
 
Mchungaji Hananja alinyimwa mshahara mwaka mzima, imagine, wanaomnyima mshahara ndio wanahubiri amani na upendo, kusamehe mara sabini.

Bila shaka kikombe hiki atakipitia mchungaji Kimaro mbele ya hawa watu wasio na huruma.

Mwenye connection na Dk. Kimaro amuulize atupe namba tumchangie wakati huu ambao viongozi wake wa kanisa wamejiapiza kumtesa yeye na familia yake.
Ni Hatari sana .

Kanisa la Kiluteri ni kanisa la kiinjili na ndilo kanisa liloleta matengenezo Kwa kusimamia Biblia.
Hata HIVYO baadae ya Martini Luther Kiongozi Wa matengenezo akiwa NDANI ya kanisa Katoliki kufariki walitokea watu wenye Tamaa za kuwa wakubwa na kupandikiza watu NDANI ya kanisa Ili libaki Katika misingi Mibaya aliyoikataa Luther. Katiba au SHERIA za Kanisa la KKKT ni kinyume na Neno la Mungu na misingi ya kanisa ambayo ni kuhubiri Injili ya kweli Kama Luther alivyofanya na SIO kuwafurahisha maaskofu Bali Kristo. Kanisa limerudi kwenye misingi ya kuwasujudia maaskofu na kuacha Injili kama ilivyoandikwa NDANI ya Biblia.
Hatujasikia Kashafa ya Kimaro kuiba FEDHA za kanisa au Kutembea na wake za watu au KUFANYA vitendo vya kunajisi watoto ZAIDI ya kukemea ubinafsi, majungu, fitina,rushwa,Wizi , uongo, usaliti, kukosa uaminifu Kwa Wakristo,kuchongeana,uvivu na KUTUMIA madaraka vibaya. Sasa anasimamishwa Kwa kosa Gani? Anapigwa vita na wanaojiona kuwa wao ndio waajiri Kwa kosa Gani.?
Analipwa Mshahara Kwa sadaka za waumini na SIO pesa za maaskaofu Wala kanisa halina mfuko Wa pamoja Wa kuwalipa Zaidi ya kutegemea sadaka. Malasusa ana misma Karibu Ishirini kwenye uaskofu na maisha yake ni mazuri Sasa Kwa nini anasikiliza majungu na watu wenye tamaa wanazipenda kutengenezewa mausharika na wenzao wanaokesha na kufunga Ili makanisa yasonge mbele kimapato na KIROHO.

Sasa Kuna watumishi ambao ni wachumia tumbo wakishaona Mchungaji Fulani ameimarisha usharika KIROHO na kiuchumi Wanacheza dili Ili wahamishiwe kwenye sharika hizo matokeo yake ni kuwa na Taasisi iliyojaa majungu na fitina na Chawa NDANI ya Kanisa
 
Kabisa
 
Back
Top Bottom