Mchungaji Katekela atakuwepo Dodoma kwa uponyaji

Ukimtoa huyo Kolola, hakuwai kuonekana mwingine tena. Labda Maghembe naye amefanyiwa figisu kaamua aanzishe ministry. TAG imebakia usaniii usaniii tu hamna mchungaji wa kuwa na nguvu pale cz Ipo kitaasisi zaidi sio kiroho zaidi.
 
huyu.Amiel Katekela ndio Mosses Kulola wa kizazi hiki,na wote wanaobeza nguvu ya roho mtakatifu wakakashifu ..waangalie wasije wakahukumu ..na wao wakahukumiwa kwa KUMKUFURU Roho mtakatifu..
 
huyu mchungaji nauhakika naye tena huyu ndugu yangu alikuwa anasita sita kwenda kuombewa na hata alivyofika kanisani akatoka nje akanipigia simu akasema mbona kanisa dogo watu wachache halafu mchungaji kijana tu..mi nataka kurudi ...nikamshauri nimamwambia huyo ndio mtumishi wa Mungu wa ukweli ..hata kama anaonekana masikini na kanisa lake dogo hata kama umri wake mdogo ..we muamini tu..utapona nikamshawishi akakubali kuombewa...

yani alipowekewa mkono kuanza kuombewa kwanza akajikuta kapiga magoti chini analia anatubu dhambi akashangaa mkono uliopooza umeingia ubaridi ukaanza kujinyosha kunyoka wenye akawa hajielewi anajishangaa kama hakuelewa nini kimemtokea akashangaa analia anatubu dhambi zake ...baadae akasekia kama mawazo yamamsemesha kichwani kwake aache dhambi ya uzinzi na uongo...na mkono uliopooza ukawa mzima siku hiyo hiyo moja..

na hakupewa mafuta wala maji ya upako wala kitu chochote na hakulipia chochote zaidi ya sadaka 5000 tu aliyokuwa nayo na si kwa kulazimishwa kwa kupenda mwenyewe..

kuna watumishi wa Mungu waliopewa karama ya kuombea wengine kuna watu wanauhusiano mzuri na Mungu watu wa Mungu wapo ...

japo manabii wa uongo na manabii wa uongo ni wengi zaidi na ndio maana watu wote wamepoteza imani na maombi na kuona kwamba wote ni matapeli ...na kumjua wa uongo na wa ukweli ni kazi...
 

View: https://youtu.be/ZjM6RHforVk?si=wgu5Syn88xU9ALqJ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…