Mchungaji Kimaro amelewa urafiki wake na matajiri

Mchungaji Kimaro amelewa urafiki wake na matajiri

Vibe la kanisa ni maskini mkuu.
Waimbaji wengi ni Vijana wa kawaida na mara nyingi Bado hawajapata kazi au shughuli zinazowabana.
Waombaji na waaofunga ni maskini na watu wa kawaida?
Walinzi wa Kanisa ni watu maskini .
Hata wahudumu wa ofisi ya Mchungaji ni watu wa kawaida .

Hata wainjilisti ni watu wa kawaida .
Kiufupi Kimaro amejikweza kama Lusifa na amepoteza hekima .
Shetani alikua juu kuliko Kimaro lakini kiburi kilipomwingia alinyangwanywa hekima na maarifa na kushushwa mpaka kuzimu akabaki na ujanja ujanja na Hila Kwa kuwashawishi watu kupitia Mali na Fedha.
Kimaro amekwisha anguka katika Ulimwengu wa roho.


Pumbavu sana shetani .
"kimaro kumfuataa Makonda"!!??
 
Bila maskini matajiri hawawezi kuwepo.

Kila mtu ana umuhimu wake.

Unaweza kuwa tajiri lakini Kuna vitu kamwe huwezi Fanya akavifanya maskini.

Mungu haangalii mali anaangalia moyo.

Unaweza toa milioni 200 wanadamu wakakusifu ila mwingine akatia mia Tano yake Mungu akaiona na kuipokea kuliko yale makaratasi ya milioni 200.v
Mungu yupi huyo anayepokea hela? ulikutana naye wapi ukaona anavyobagua hela.Aacheni uongo bhana.Mungu yupo ila ahitaji hela yako, Mungu anataka hela ili imsaidie nini??
 
Wasalaam JF,

Hekima na busara ni speed governor ya kuzuia kuropoka na kufoka, dhana ya matajiri na maskini ndani ya kanisa si yenye afya, kanisa ni pahala jumuishi, uchakataji wa jumbe za injili unahitaji maandalizi , busara, hekima na ukomavu katika madhabahu.

Yawezekana KKKT imemfanya Mch. Kimaro awe tajiri na ana enjoy raha na utamu wa kuwa sehemu ya kundi la watu matajiri.

Ni kwa neema ndio watu hupata vyote na vyote havigawiki.

Diversity is strength especially in a well coordinated way of thinking and looking at issues squarely.

How do you reach out the message may be so catastrophic.

Nyakati muhimu katika kuishi Imani maarifa yake Mungu ndani yetu yawe nguzo ya vinywa vyetu nyakati za uwakilisho na uwasilisho.

Wadiz
Yesu alikuja kwa ajili ya wanyonge
ambao wanyonge na maskini wakiwepo lakini utajiri sio mbaya ila usichukue nafasi kubwa ukamsahau
aliekupa .
 
Amewananga maskini na kuwapa sifa kubwa na nyingi matajiri wa kanisa lake, nadhani ndio waliompigania kwenye sakata lake la kibri, jeuri, na dharau kwa wakristo
Haikuwa dharau kwa wakristo ila aliongea ukweli tu
 
Elimu itolewe watu tuelewe. Kuwa tajiri sio dhambi. Kwa nini walala hoi tunakuwa na chuki na matajiri? Wao sio walio wanaosababisha tuwe na mafukara hivyo kuwa wenye chuki dhidi yao. Ni uvivu wetu umetufikisha hapa. Tuige mbinu gani halali wametumia kuupata utajiri nasi tuwe matajiri kama Wao.
Tunasahau kuwa matajiri ndio wanaotufanya kuonekana watu na maisha haya ya masikini jeuri. Tunavaa tunapendeza kwa viwanda vya nguo zao. Tunatumia simu za viwanda vyao kuingia jf . Tunatumia ndege na magari ya viwanda vyao kutanulia mjini. Maskini mimi hata vijiti vya kuchokonolea meno sijawahi kutengeneza. Naanzia wapi mkulima wa msata kumchukia tajiri.?

Kanisani mmezidi ubaguzi wa tajiri na maskini. Acheni ubishi. Ndio maana kimaro akamdiss petro na kumpamba tajiri.
 
Tafuta hela acha stress ndg

Akafanye ufisadi? Maana njia nyepesi ya kupata pesa ni ufisadi. Si ku hizi kanisani ni pesa tu hakuna injili. Kutukana watu wenye uwezo wa kawaida wakati nchi yetu ni maskini.
 
Inabidi tuukatae umasikini kwa nguvu zetu zote; ulishawahi kuona wapi, mazishi ya masikini yakaongozwa na askofu?
Maskini lazima wawepo tu, na ndio wengi. Nchi yenyewe maskini halafu mnataka kila mtu awe tajiri, huo ni unafiki. Kanisa linapotea kwa kasi limekuwa sehemu ya mipasho na sio kuutafuta uso wa Mungu.
 
Umasikini sio sifa wala si kitu cha kujivunia

Hakuna aliyesema ni sifa , lakini kumtukana maskini na kumuona hafai kwa umaskini wake hilo ni kosa kubwa. Nchi ya kimaskini halafu mnawadharau maskini huo ni unafiki. Tuache injili ya ubaguzi kanisani.
 
Maskini lazima wawepo tu, na ndio wengi. Nchi yenyewe maskini halafu mnataka kila mtu awe tajiri, huo ni unafiki. Kanisa linapotea kwa kasi limekuwa sehemu ya mipasho na sio kuutafuta uso wa Mungu.
Ukizifuatilia sana hizi dini utagundua, sehemu kubwa hutumika kama fursa za watu
 
Kimaro na mashabiki wake nawaona hawana maana. Wapo kanisani kama maagenti. Mtu kila siku ni kuongea maneno ya ukakasi. Mchungaji ni wa wote sio wa baadhi ya watu.
 
Back
Top Bottom