Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Ukiwa tajiri humlalamikii Mungu, wewe ukiomba ni unamshukuru Mungu tu.
 
Huyu jamaa hafai,sisi padri katuambia aliyepeleka habari za kufufuka Yesu aliyekuwa anajulikana Kama kahaba,Maria Magdalena ndio alikuwa wa kwanza kusambaza habari za ufufuko wa Yesu,so hata nasi tusijione wanyonge pamoja na madhaifu yetu tukitubu tunaanza upya na kuwa wasambazaji injili waziri🙏wajumbe wa Mungu,yeye kimaro anawasujudu matajiri na kuwadharau watunza makaburi🤔kila mmoja ana nafasi yake,moyo wake umejaa tamaa ya mali na amepotoka.

Maria Magdalena alikuwa kahaba?

Historia inayozunguka Maria Magdalena ni ngumu sana na kuijibu kwa hakika, kwani kuna habari mbalimbali ambazo zimekuja kuunganishwa na kusambazwa katika kipindi cha miaka mingi. Lakini kwa ufupi, hakuna ushahidi wowote wa moja kwa moja unaothibitisha kuwa Maria Magdalena alikuwa kahaba.

Maria Magdalena anajulikana katika Biblia kama mmoja wa wanafunzi wa Yesu na mwanamke aliyetolewa pepo saba. Pia anasemekana kuwa alikuwa mmoja wa wanawake waliomsaidia Yesu wakati wa huduma yake na alikuwa pamoja naye wakati wa kusulubiwa kwake na kufufuka kwake.

Hata hivyo, baadhi ya watafiti na waandishi wa historia wanaamini kuwa taarifa hizo zilichanganywa na hadithi za wanawake wengine katika Biblia, na ndipo zikazua uvumi kwamba Maria Magdalena alikuwa kahaba.

Kwa hivyo, kwa muhtasari, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa Maria Magdalena alikuwa kahaba, na hadithi hiyo inaweza kuwa ni uvumi tu uliozushwa kwa sababu za kisiasa au dini katika kipindi cha miaka mingi iliyopita
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama amesema Tajiri Yusuf wa Almathaya ndio aliyemzika Yesu katika kaburi lake la kifahari

Kimaro amesema Kanisa linawahitaji Matajiri kwa sababu ndio wanaoliondolea Kanisa aibu Wakati wa uhitaji

Hivyo tusiwape majina mabaya Matajiri kwa kuwaita Mafisadi, Wahujumu Uchumi au Freemason Kwani utajiri ni baraka hata katika level ya familia Kwani ndio wanaofuta aibu za familia, amesisitiza mchungaji Kimaro

Kimaro amesema Watu wengi ni walinzi tu wa makaburi kama wale Walinzi wa Pilato waliotumwa kulinda kaburi la Yesu, hivyo wewe kama mkristo usikubali kuwa Mlinda makaburi

Nawatakia Pasaka Njema!
Ni miongoni mwa wachungaji waliojaa kiburi&kukosa hekima katika kusema.
 
Mabuti ya kijeshi uyaone mafupi mepesi/
Yani kama vile simple toka nduki toka lesi/
Ka risasi ya bunduki au jeti/
No kunyuti no kuketi, wape nafasi wakushoot/
Kama Malcolm X usikubali kubaki/
Uwe pimbi upewe kesi/
Ikibidi jitose ndani ya dimbwi la kinyesi/
Sio suala la uoga,kuogopa ukunguru/
Ila Bora kurogwa kuliko kukosa uhuru/
Wapi Shemponda wapi Jenerali Komba/
Siri Kali Sera Kali cheza mbali na wajomba/
Kimbiaa, mitihani imevuja nyie hamjasikia!?/
Yanini kusoma huku elimu inanunuliwa/
Kimbiaa, Nchi imeshauzwa hii hamna kusikilizia/
TANESCO, Madini Hadi Air Tanzania/
Watoto wa uswazi hawana matumaini/
Ndoto zao ujambazi sababu ya umaskini/
Matapeli wenye shahada kila hatua tatu/
Makahaba wa miaka kumi na tatu/
Maskani kamsitu, vicheche na machatu/
Usipite pekupeku bila kuvaa viatu/
Aaaah Kimbiaaaaaaaa

Rest Easy LANGA (RIP)
Nashukuru kwa kunikumbusha moja ya verse Bora ktk muziki wa Hip-hop ya bongo.
 
Ndio maana sisali tena. Pale.

Jamaa anapotosha mandiiko.

Petro ndio msiingi wa kanisa. Na hakua tajiri.

Hiyo ya Arimathaya ni sadaka kama nyingine tu.

Hapo kijito washarika wana pesa na wanamhudumia hivyo lazima awapaishe.
Sasa wakiwa na pesa we kinakuuma nini? Si utafute za kwako?
 
Nadhani Mch. Kimaro anaendelea kukosa umakini. Sijui sababu ni nini Mungu wangu. Mtumishi aliyeonekana kusimamia neno nakuwa hivi. Bwana Yesu lisema kuwa kuwa tajiri kunakuingiza katika risk kubwa sana (hataari) ya kutokuingia Mbinguni. Yesu alikosea? Pia kulinusuru kanisa wakati wa uhitaji ndio kuingia Mbinguni? Kama mtu hana nia ya kwenda Mbinguni hapo ni sawa. Toa pesa nyingi sana kusaidia watumishi, jenga majengo ya makanisa , n.k. tutakusifu sana naa itaisia hapo. Je ni kwamba mtu aliyeiba akawa tajiri akatoa sadaka kanisani sifa ya wizi inaondoka? Mwanasiasa mmoja hapa TZ aliwahi kuwashangaa wezi wanaojaribu kumhonga Mungu kwa kutoa sadaka pesa waliyochuma kwa wizi, rushwa na ufisadi. Kumbe wanatiwa moyo na mahubiri kama haya. Kweli Mch. Kimaro umeniangusha sana
Una chuki zako na matajiri tu. Mchungaji yuko sahihi na hajapotosha popote
 
Maria Magdalena alikuwa kahaba?

Historia inayozunguka Maria Magdalena ni ngumu sana na kuijibu kwa hakika, kwani kuna habari mbalimbali ambazo zimekuja kuunganishwa na kusambazwa katika kipindi cha miaka mingi. Lakini kwa ufupi, hakuna ushahidi wowote wa moja kwa moja unaothibitisha kuwa Maria Magdalena alikuwa kahaba.

Maria Magdalena anajulikana katika Biblia kama mmoja wa wanafunzi wa Yesu na mwanamke aliyetolewa pepo saba. Pia anasemekana kuwa alikuwa mmoja wa wanawake waliomsaidia Yesu wakati wa huduma yake na alikuwa pamoja naye wakati wa kusulubiwa kwake na kufufuka kwake.

Hata hivyo, baadhi ya watafiti na waandishi wa historia wanaamini kuwa taarifa hizo zilichanganywa na hadithi za wanawake wengine katika Biblia, na ndipo zikazua uvumi kwamba Maria Magdalena alikuwa kahaba.

Kwa hivyo, kwa muhtasari, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa Maria Magdalena alikuwa kahaba, na hadithi hiyo inaweza kuwa ni uvumi tu uliozushwa kwa sababu za kisiasa au dini katika kipindi cha miaka mingi iliyopita
Hajui lolote huyu. Kajaa chuki tu
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama amesema Tajiri Yusuf wa Almathaya ndio aliyemzika Yesu katika kaburi lake la kifahari

Kimaro amesema Kanisa linawahitaji Matajiri kwa sababu ndio wanaoliondolea Kanisa aibu Wakati wa uhitaji

Hivyo tusiwape majina mabaya Matajiri kwa kuwaita Mafisadi, Wahujumu Uchumi au Freemason Kwani utajiri ni baraka hata katika level ya familia Kwani ndio wanaofuta aibu za familia, amesisitiza mchungaji Kimaro

Kimaro amesema Watu wengi ni walinzi tu wa makaburi kama wale Walinzi wa Pilato waliotumwa kulinda kaburi la Yesu, hivyo wewe kama mkristo usikubali kuwa Mlinda makaburi

Nawatakia Pasaka Njema!
Petro alimpigania Yesu akiwa hai

Hadi alitoa Kisu akakata sikio la mtu aliyemvamia Yesu

Yusuf wa Alimataya aliheshimu Maiti ya Yesu akina Petro walimpigania Yesu akiwa hai

Hawakuwa wakila na kulala tu

Petro alitoa hadi.mtumbwi wake Yesu autumie kuhubiria alimkuta akivua sanaki

Petro akatoa mtumbwi wake akahubiria maelfu akiwa kakaa kwenye mtumbwi

Kabla Kufa hatuoni huyo Yusufu wa Akimataya alitoa nini kama kwa Yesu akiwa hai

Waheshimu maiti mbona hadi leo wako wengi tu mtu akiumwa akalazwa hawatoi chochote akifa wa kwanza kutoa michango.mikubwa na kugharimia majeneza na Usafiri watu kama hao ni wafuasi wa Yusufu wa Alimataya
 
Najua hata hujala leo ulivyo maskini. Omba msaada tu usaidiwe
Mimi wewe hunisumbui kwakua nakufahamu vyema tu.

Namna ulivyopata hiyo ajira uliyonayo kwa Sasa hapo ofisi ya mawakili jinsi ulivyoo maskini.

Yaani kama sio yule Rafiki Yako aliyepo serikalini kukutafutia ajira bado ungebakia pale mwenge kwenye ile ofisi walikua wanakulipa laki tatu kwa mwezi wakili mzima.
 
Back
Top Bottom