Mchungaji Lusekelo pumzika, acha vijana wafanye kazi

Mchungaji Lusekelo pumzika, acha vijana wafanye kazi

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
3,417
Reaction score
6,149
Watu huwa wanazaliwa, wanakua na watu huwa wanazeeka na huwa wanafariki. Kwenye vipindi vya maisha ya mtu kuna wakati wa ujana ambao ni wakati wa kuhangaika sana lakini kuna wakati wa uzee ambao ni wakati wa kutulia na kuangalia kazi uliyofanya.

Wakati wa uzee ndio hasa wakati wa kuangalia taabu yako na matunda uliyopata. Kama ulilegea wakati wa ujana basi wakati wa uzee unakuwa na taabu sana.

Ukimuona mzee anahaingaika na vijana kwenye uzee wake basi ni dhahiri kuna kitu hakiko sawa kwenye maisha yake. Huu ni wakati wa mchungaji Lusekelo kupumzika na kuacha vijana wafanye kazi na sio wakati wa kugombana nao na huku akijua hata nguvu hizo hana.

Kwenye uzee huu ndio unawaza kurusha kutumia mitandao ya kijamii kupambana na vijana ambao wangekuletea sukari ukiwa unezeeka.

Hii inanikumbusha story na nabii kijana na nabii mzee. Wivu wa nabii mzee aliokuwa nao ulimpelekea kumtendea nabii kijana kwa hira na kumkosesha. Kubali tu kwamba Bwana hajasema na wewe lakini kasema na mwingine. Kumshambulia mwenzako kwenye mwili wa Kristo wala haikusaidii chochote... zaidi sana unajiumiza mwenyewe maana wote ni mwili mmoja yaani Kristo.

Acheni kutumika vibaya na hao wanaokutumia. Kama lengo ni kuhamasisha chanjo njia rahisi ni kuwaomba wizara ya afya wafungue kituo cha chanjo hapo kanisani kwako wachanje waumini wako wote. Hii itatoa mfano wa kuwa kiongozi sio kurusha clip. Wewe unajua kuwa hata unaowaongoza hawakubaliani na chanjo hizi za msaada.

Mwisho nikuombe uachane na hao wanaokutumia. Nasema hivyo maana najua kuwa wewe unajua kuwa unakosea. Unayemshambulia wala hana muda na wewe lakini sisi ambao tumekuona siku nyingi ukimtumikia Mungu tunapata tafsiri ya kwamba huenda unazeeka vibaya PUMZIKA.

Ukishasoma ujumbe huu mrushie na mzee mwenzako mwambie naye apumzike mambo hayo yanaabisha kanisa.

Ni mimi katika mwili wa Kristo
Nabii S.S Lolinga
 
Aliyeandika hapa sio bwana Gwaji kweli au nami nazeeka vibaya eti jamani???....eeenhe,Gwaji sio wewe kweli???
 
Nanyi mbona hamueleweki sasa kama yule askofu àlikataa waumini wake wasichanjwe, mwache na huyu awashauri waumini wake wachanjwe

Ukiona tabu na ww kafungue kanisa lako!
 
Ewe unayejiita nabii S.S Rolinga, TAFADHALI Usizidishe mazoea, ulileta unabii ule wa kwanza ukapata umaarufu.. sasa pumzika, rudi kwa Mungu Msihii Akutumie kwa HAKI na sio KUJITUMIA Kiukanjanja kama unavyofanya hapa.

Ukishupaza shingo, Adhabu ya Bwana Mungu Wa Majeshi ii karibu nawe.

Nimemaliza kaka.
 
Back
Top Bottom