Mchungaji Mbarikiwa: Kilichokutuma Christina Shusho ni umalaya tu hakuna huduma hapo

Mchungaji Mbarikiwa: Kilichokutuma Christina Shusho ni umalaya tu hakuna huduma hapo

1713698980748.png
 
(Luke 16:18)
Amwachaye mke/ mume.....azini.

Sorry kama una mama mwenye sifa hiyo.

Mchungaji Mbarikiwa ametumia maandiko.
Mkuu endelea kuwapa ukweli hao wanaokwambia tuachane nae wakati yeye ana kundi kubwa la watu anaowashawishi kwa huu upumbavu wake.
 
Jamaa Yuko sahihi , huyo manzi shape inamzuzua wahuni watapiga saaana
amekuwa na shepu nzuri sana na sura ipo, mashaallah kaumbika kisawasawa kila idara kakamilika, sijui kama fisi watamuacha!
 
Ndoa aslimia kubwa zimeshakufa, watu wanaishi tu eti kuogopa jamii. Ambao sio wanafiki ndio wamekua na ujasiri wa kuzivunja . Mimi sikutaka kuwa mnafiki nikaivunjilia mbali.
Ogopa sana kuishi kwa kufurahisha watu au kwa kufungwa na mikatale ya kijamii huku kinafsiya, kisaikolojia (na hata kimwili) unateketea. Kama ndoa kufa na ife ali mradi ubakie huru na salama.

Ulifanya jambo jema! 👏👏👏
 
Shape inamzuzua yeye na Marioo, werevu hatuwezi kubabaishwa na gari namba A ilihali namba E zimejaa tele mitaani "age gone/uhenga vs damu changa"

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
damu changa wenyewe wanamtaka, wale vijana ni walafi hawatamuacha
 
Mkuu endelea kuwapa ukweli hao wanaokwambia tuachane nae wakati yeye ana kundi kubwa la watu anaowashawishi kwa huu upumbavu wake.
Dhambi Huwa inakemewa, Si kuficha.

Na Kwakuwa ametumia media kujaribu kuhalalisha UZINZI, nasi tunatumia media hiyo hiyo.

Haya mambo ya kuficha dhambi ndiyo yamesababisha mtu ana nyumba ndogo, lakini anagombea uongozi na kushinda Eti kw.a kuwa ana pesa.

Neno la Mungu ni UPANGA ukatao kuwili,

UKWELI utasemwa bila kupindisha.

Hiyo ndiyo INJILI.
 
Hamna kupaka rangi maneno ni ukweli na uwazi.
Tukinyamazia haya, IPO siku mke ataaga kuwa anaenda kulala Kwa boyfriend kama walivyo wazungu,

Tufuate mwongozo wa neno la Mungu.

Ukimwacha mume au mkeo, unakosa ushuhuda wa kusimama madhabahuni.

Arudi kutengeneza, ndipo arudi kuhubiri kupitia nyimbo.
 
Huyo mchungaji anayejiita mbarikiwa na yeye ni mchungaji uchwara tu, nyuma ya pazia ana makando kando yake maovu mengi tu..

Yeye anafuatilia maisha ya wengine kama nani?

Mtu kaamua kuachana na mmewe yeye ina muhusu nini?

Hawa wachungaji uchwara wanojivika uungu mtu ndio waovu wakubwa.
pamoja na makandokando yake uyaonayo anastahili kuukemea umalaya/ukahaba.
 
pamoja na makandokando yake uyaonayo anastahili kuukemea umalaya/ukahaba.
Anashindwaje ku ukemea huo ukahaba bila kutaja jina/majina ya watu?

Kwa nini afanye personal attack ya kukemea ukahaba wa mtu mmoja mmoja na kumtaja jina kabisa?

Kwa nini asiende Riverside,
mwana nyamala au uwanja wa fisi akafanye kazi ya kukemea makahaba na malaya?

Mama yake au dada yake huyo "mchungaji uchwara anaye jiita mbarikiwa" kama na wao ni malaya, Ataweza kuwataja majina na kuwa kemea live kwenye ibada zake hizo?

Au anataka kiki tu kwa vile Christina shusho ni staa?
 
Ikiwa ameamua kukengeuka,

Aache kutumia madhabahu takatifu kuhalalisha UOVU wake,

Akiendelea kukaa hapo, lazima apigwe ipipasavyo.
Madhabahu takatifu ni yako? Wewe una utakatifu gani ndugu yangu?

➡️ Mpigaji wa haki na kweli ni Mungu pekee. Wewe hujui alichopitia na unaendelea kumhukumu na kumpiga. Kumbe mwenzio alishatubu na kusamehewa na Mungu wake. Ni hatari sana kujipa kazi ya Uungu na kuanza kuhukumu wengine bila kuelewa sawasawa madhila yao na vita vyao vya kiroho; na wakati huo huo wahukumuji nyinyi yawezekana mkawa ndo waovu zaidi kuliko hata yule mnayemhukumu.
 
Anashindwaje ku ukemea huo ukahaba bila kutaja jina/majina ya watu?

Kwa nini afanye personal attack ya kukemea ukahaba wa mtu mmoja mmoja na kumtaja jina kabisa?

Kwani asiende Riverside,
mwana nyamala au uwanja wa fisi akafanye kazi ya kukemea makahaba na malaya?

Mama yake au dada yake huyo "mchungaji uchwara anaye jiita mbarikiwa" kama na wao ni malaya, Ataweza kuwataja majina na kuwa kemea live kwenye ibada zake hizo?

Au anataka kiki tu kwa vile Christina shusho ni staa?
huoni anayetajwa jina kafanya uharibifu mkubwa kwa maadili ya ndoa?
 
Usipaniki.. hayo ni majina wanajipa kama wasanii wa muziki. Kuna mbarikiwa, kuhani, bulldozer, nabii mkuu, mzee wa upako, na wengine wengi.
Acha kupotosha..Mbarikiwa ni jina lake sio la kupachikwa,kwa wakristo ni jina la ubatizo,kama wengine wanavyoitwa John ,Christian, Jesus na wengine.
 
Back
Top Bottom