Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile wa Mbeya akagua simu za waumini hadharani akiwa madhahabuni

Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile wa Mbeya akagua simu za waumini hadharani akiwa madhahabuni

Jpili ijayo kila mtu inbox iko empty
Hata bwana Eliya alikua "ameisafisha" simu yake, ukisikiliza kwa makini utagundua kuwa mchungaji alikuta uwanja wa SMS umesafishwa, na whatsapp pia imesafishwa, ipo hiyo meseji moja tu, ambayo inaonekana pia iliingia wakiwa hapo hapo ibadani.
Huo utaratibu wa kukagua simu za waumini wake kwa ambush, hajauanza jumapili iliyopita, amekua nao muda mrefu.
 
I wish ningekuwa eliya, ningepata sabau hata huko kwa Mungu niwe na sababu ya kujitetea kwanini sikuwa naenda kanisani.

Ila kadri ya mapambazuko ya juwa ndio dini na imani za kimungu zinazidi kupotea miongoni mwa watu wengi, na sababu moja wapo kubwa ni hawa wachungaji wa mchongo!
 
Kwa nini umruhusu mchungaji akague chumbani kwako. Mambo yote ambayo hawezi kuona kwa macho yake wala kusikia kwa masikio yake hayamhusu. Kijana kakosea sana kumpa simu
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile jumapili iliyopita wakati wa ibada katika kanisa lake linalojulikana kama, 'Kikosi kazi cha injili', alimuita mmoja wa waumini wake kijana anayeitwa Eliya na kuamuru ampatie simu yake, ambapo aliikagua na kukuta meseji ya WhatsApp kutoka kwa binti.

Kisha akampigia huyo binti akiwa hapo hapo madhahabuni kwa simu ya Eliya, na mwisho alimtimua Eliya ibadani.

Tukumbuke kuwa huyu mchungaji ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kushinda rufaa yake ambapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila usajili.

Nimeambatanisha clip hapa chini.

Je, unazungumziaje, hii ni sawa Mchungaji kukagua simu za waumini wake tena hadharani?

Mimi naona ni unajisi wa wazi wa haki ya faragha kwa waumini wake, mbaya zaidi inakua kama udhalilishaji kwa kufanya haya hadharani.

Hii inasikitisha sana.

View attachment 2977744

Insanity, Hata Yesu hakufanya hivi, sasa ni dhahiri, huyu mtu ni kichaa, anapaswa kuwa controlled, atakuja kuua waumini huyu siku moja.
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile jumapili iliyopita wakati wa ibada katika kanisa lake linalojulikana kama, 'Kikosi kazi cha injili', alimuita mmoja wa waumini wake kijana anayeitwa Eliya na kuamuru ampatie simu yake, ambapo aliikagua na kukuta meseji ya WhatsApp kutoka kwa binti.

Kisha akampigia huyo binti akiwa hapo hapo madhahabuni kwa simu ya Eliya, na mwisho alimtimua Eliya ibadani.

Tukumbuke kuwa huyu mchungaji ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kushinda rufaa yake ambapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila usajili.

Nimeambatanisha clip hapa chini.

Je, unazungumziaje, hii ni sawa Mchungaji kukagua simu za waumini wake tena hadharani?

Mimi naona ni unajisi wa wazi wa haki ya faragha kwa waumini wake, mbaya zaidi inakua kama udhalilishaji kwa kufanya haya hadharani.

Hii inasikitisha sana.

View attachment 2977744
Hapo hamna kanisa
 
Back
Top Bottom