Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Katika muendelezo wa kutupa makombora, vijembe, hasira na kuonyesha namna CHADEMA ilivyojaa ubabaishaji na uhuni uhuni pamoja na kukosa viongozi wenye kuheshimika na kutoa muongozo.

Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa mbunge wa Iringa mjini na mwenyekiti wa kanda ya Nyasa na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA amesema ya kuwa, Hayati Magufuli alisemaga aende CCM na kwamba atampatia Ubunge, pesa pamoja na Uwaziri juu. Anasema alifuatwa hadi Segerea na wasaidizi wa Hayati Magufuli na kupewa simu ili azungumze na Rais lakini bado alikataa.

Anasema kwa sasa wapo ambao wakiitwa na Rais Wanakimbia mbiombio kwenda kwa Rais.lakini yeye alimkatalia Rais.amesema yeye akitaka kuondoka CHADEMA anaweza tu kuondoka bila kutafuta visingizio.anasema maana hakuna wa kumzuia.

Rai yangu ni kuwaomba wana CHADEMA wanaojitambua na wenye akili Timamu kuhama haraka sana ndani ya CHADEMA na kuingia CCM kwa kishindo, maana kwa sasa CHADEMA inaendeshwa kihuni huni sana na kibabe kibabe tu. CHADEMA imejaza vijana wa hovyo hovyo na ambao akili zao zilishavurugika na kukosa muelekeo, imejaa vijana malimbukeni waliokosa adabu na malezi mazuri ya wazazi wao, imejaa vijana waliozibuka kiakili na kuwa utafikiri wanatumia vitu vinavyoharibu mfumo wao wa ubongo na fahamu.

CHADEMA nzima limebaki kama genge fulani tu hivi la watu walioshindikana na kulaaniwa na walimwengu. Wao wenyewe tu hawana umoja wala mshikamano wala kuheshimiana. Uchaguzi tu unawatoa roho? Vipi wangekuwa na madaraka? Si wangetoana roho na kuuwana? CHADEMA kumejaa watu waropokaji na wenye mihemuko hovyo hovyo, ni watu wa kukurupuka tu na kutapika maneno machafu machafu tu yaliyokosa staha na adabu.

Mchungaji Msingwa nakukaribisha sana ndani ya CCM, huko CHADEMA fahamu ya kuwa utakufa kwa presha tu maana watakuwa wanakutenga na kukunyanyapaa muda wote. Kumbuka huko umechanganyikana na ma vijana yaliyokosa adabu na malezi mazuri, utatukanwa na kushushiwa heshima yako.utaporomoshewa matusi mpaka unuke. Njoo CCM chama chenye upendo, umoja na mshikamano.chama kinachoheshimu mawazo ya kila mtu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

===

Pia soma: Mch. Msigwa: Nikihamia CCM, wananchi chomeni moto nyumba na magari yangu
 
CHADEMA nzima limebaki kama genge fulani tu hivi la watu walioshindikana na kulaaniwa na walimwengu. Wao wenyewe tu hawana umoja wala mshikamano wala kuheshimiana. Uchaguzi tu unawatoa roho?
Hata magenge huwa wana Demokrasia.

Umewapa CHADEMA sifa kubwa sana, inayowastahili
=============
Ngoja mpambe(ERYTHROCYTE) wa Mabilionea wa washindi wa Uenyeviti wa Kanda aje.
 
Mchungaji peter Msigwa ameendelea kutoa maneno mbalimbali yanayoonyesha kukosa kifua cha uongozi pamoja na ukomavu wa kisiasa na uvumilivu, ndio maana siku zote nasemaga humu jukwaani kuwa ukiwa kiongozi unapaswa kuwa

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe kwa akili yako unaweza kufikia hata 1% ya uwezo wa akili ya Msigwa? Ni kweli Msigwa alikataa vishawishi vinono vya Magufuli kwa vile alikuwa na msimamo tofauti na wewe unayejaza machapisho yako uchwara yasiyokuwa na maudhui kwa matumaini tu ya kupewa uteuzi. Eti chawa umdharau Mchungaji Msigwa,jipige kifua huku ukijicheka kwa ukosefu wa akili timamu.
 
Nionyeshe huko kwenye chama la majizi nani sio mchumia tumbo.
Ndani ya CCM viongozi ni wazalendo na wanaofanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.Tofauti na huko CHADEMA mnakosaka matonge kwa ajili ya kulisha na kujaza matumbo yenu. Ona sasa uchaguzi tu unawatoa roho .vipi ingekuwa mmeshika dola? Si mngeuana ninyi kwa ninyi?
 
Wewe kwa akili yako unaweza kufikia hata 1% ya uwezo wa akili ya Msigwa? Ni kweli Msigwa alikataa vishawishi vinono vya Magufuli kwa vile alikuwa na msimamo tofauti na wewe unayejaza machapisho yako uchwara yasiyokuwa na maudhui kwa matumaini tu ya kupewa uteuzi. Eti chawa umdharau Mchungaji Msigwa,jipige kifua huku ukijicheka kwa ukosefu wa akili timamu.
CHADEMA ni wasaka Tonge tu uliojaa njaa kali
 
Ndani ya CCM viongozi ni wazalendo na wanaofanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.Tofauti na huko CHADEMA mnakosaka matonge kwa ajili ya kulisha na kujaza matumbo yenu. Ona sasa uchaguzi tu unawatoa roho .vipi ingekuwa mmeshika dola? Si mngeuana ninyi kwa ninyi?
Una tatizo la kutokujua tafsiri sahihi ya neno uzalendo.
 
Ndani ya CCM viongozi ni wazalendo na wanaofanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.Tofauti na huko CHADEMA mnakosaka matonge kwa ajili ya kulisha na kujaza matumbo yenu. Ona sasa uchaguzi tu unawatoa roho .vipi ingekuwa mmeshika dola? Si mngeuana ninyi kwa ninyi?
Hukuna jizi mzalendo. Labda uzalendo una maana tofauti huko kwenye chama la majizi.
 
Back
Top Bottom