Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Mliodhani nahama CHADEMA Mnajidanganya

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Mliodhani nahama CHADEMA Mnajidanganya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ujumbe wake huu hapa
---
1717436475941.png
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa amesema hana mpango wa kukihama Chama cha CHADEMA baada ya kutoshinda uchaguzi wa Kanda ya Nyasa.

Msigwa ameyasema haya kutokana na baadhi ya Watu kuamini kuwa kuitisha kwake mkutano na Wanahabari wa Iringa leo kulikua na nia ya kutangaza kukihama Chama hicho.

“Najua Wabaya wangu wengi leo walikuwa wanajua nahama, mimi siondoki niko CHADEMA mliokuwa mnafikiri na bado nipo ,sihami Chadema tunapambana humuhumu yule anayetaka kunyofoa Watu atanyofolewa mwenyewe na hatutoogopa Mtu”

PIA SOMA
 
Mama alishasema ndani mwao kuna fukuta tuendelee kunywa mtori mda si mrefu tutaona mengi
 
Ndio amesha kujubu hivyo
Yes, hata mimi nilikuwa na dhana hiyo.

Why? Hii ni fragile moment, siyo muda wa kuleta utengano kwa watu mnaotazamia kupambana na CCM/serikali ya CCM kutwaa dola/kupata wabunge wengi and the like
 
Mkuu 'Erythro', ujumbe muhimu alioutoa kwenye habari hiyo ni huu hapa:'

"... yule anayetaka kunyofoa watu atanyofolewa mwenyewe,...na hatuogopi mtu"

Mengine yote ni kelele tu za kupoteza lengo.
Ni wakati mwafaka sasa CHADEMA ijisafishe; hakuna njia nyingine zaidi. Kirusi kikuu ni Mbowe, bila ya kumung'unya maneno.
 
Back
Top Bottom