Hayo ni ya zamani, tugange ya sasa. CHADEMA ya sasa, adui mkuu ni Mbowe.Hakuna ushahidi wowote kuthibitisha hilo, kama unao tuwekee humu, tena Mbowe ndiye alipambana sana kuhakikisha Msigwa anakuwa Mwenyekiti wa Kanda kwa kumshawishi Ole Sosopi ajitoe kumpisha Kaka yake
Mwenyekiti anao uzito mkubwa sana ndani ya chama. Hawezi kuacha chama kinakuwa na sintofahamu ya aina hii iliyopo sasa asisimame na kuonyesha njia.
Mwenyekiti kajifunza mbinu toka kwenye "maridhiano"; sasa anatumia mbinu hizo hizo akidhani zitafua dau ndani ya CHADEMA.
Kunyamaza na kujifanya haoni kitu kinachotokea, akitarajia mambo yatajinyoosha yenyewe, huo siyo uongozi.
Tena mbaya zaidi anahusisha yeye mwenyewe, halafu kakaa kama hayupo?
Unataka chama kifikie ngazi gani ya kusambaratika ndipo ujue kwamba mwenyekiti kakengeuka!
Mbinu hii ya kukiwasilisha chama kwa Samia haitafanikiwa. Bado nasita sana kuamini kwamba Mbowe anaendeshwa na tamaa ya pesa juu ya jambo hili. Nasita sana kuliamini hili.