Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Mliodhani nahama CHADEMA Mnajidanganya

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Mliodhani nahama CHADEMA Mnajidanganya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama hataki kuhama basi afukuzwe, kuendelea kubaki chadema ni hatari kwa afya ya chama.
Watawafukuza wangapi ili kukisafisha chama kabla ya kukiwasilisha kwa CCM ya Samia? Mbona CHADEMA itakuwa imekufa tayari!
 
3035694_images.jpg
 
Itabidi mtafunane wenyewe kwa wenyewe
 
Attachments

  • FB_IMG_1644236040854.jpg
    FB_IMG_1644236040854.jpg
    15.8 KB · Views: 3
  • FB_IMG_1616545580714.jpg
    FB_IMG_1616545580714.jpg
    90.9 KB · Views: 2
  • JamiiForums2012770947.png
    JamiiForums2012770947.png
    68.8 KB · Views: 2
Yes, hata mimi nilikuwa na dhana hiyo.

Why? Hii ni fragile moment, siyo muda wa kuleta utengano kwa watu mnaotazamia kupambana na CCM/serikali ya CCM kutwaa dola/kupata wabunge wengi and the like
Bila ya '"moment'" hii sahau kabisa CHADEMA kutwaa serikali. This cleansing is necessary; and it is happening at the opportune moment.
 
Mwanasiasa akikwambia sasa hivi ni usiku na giza limeingia na umo ndani, toka nje ujiridhishe!
(1) .Lowasa kabla ya uchaguzi wa 2015 alisema asipoteuliwa kugombea uraisi ataenda kuchunga ng'ombe.
(2) . Baada ya jina lake kukatwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM akatangaza CCM siyo baba yake Wala CCM siyo mama yake Kisha akahamia CHADEMA.
(3) . Miezi au mwaka mmoja baada ya uchaguzi kupita akarudi CCM na waandishi wa habari walipomuuliza kitu gani kimerudisha CCM akasema ameamua kurudi nyumbani kwa hiyo mtu akirudi nyumbani Haina haja ya kumuuliza maswali.!!.
HIVYO NDIVYO WANASIASA WALIVYO.
 
Hamalizi hata mwezi,Kauli zake siyo za mtu anayejali chama tena.
Mbowe nae inatoshq,mwezi wa tisa apumzike.
Mkuu 'Erythro', ujumbe muhimu alioutoa kwenye habari hiyo ni huu hapa:'

"... yule anayetaka kunyofoa watu atanyofolewa mwenyewe,...na hatuogopi mtu"

Mengine yote ni kelele tu za kupoteza lengo.
Ni wakati mwafaka sasa CHADEMA ijisafishe; hakuna njia nyingine zaidi. Kirusi kikuu ni Mbowe, bila ya kumung'unya maneno.
Sasa tutaongea lugha Moja! Mbowe hakustahili muda mrefu kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm. Na hili nililisema muda mrefu baada ya blunder ya kumuokota Lowassa, na kumpa nafasi adhimu ya kugombea urais. Nashukuru lile nililoliona muda mrefu Sasa linaanza kueleweka kwa wengi.
 
Miaka yote nimemsapoti Mbowe na nakiri amefanya kazi kubwa lakini for the God's sake, asigombee tena. Hlafu CHADEMA nao walikosea sana kuweka utaratibu wa mwenyekiti wa kanda kupigiwa kura na watu wachache namna hiyo. Wangefanya kama chama cha Republican kinavyofanya.Wagombea wawe wanapita eg kata kwa kata, au tarafa au whatever watakavyoamua na kupigiwa kura na wanachama na baada ya mzungunguko, yule mwenye kura nyingi ndiye anakuwa mshindi. Hili la kura kupigwa na watu wachache sana linafanya rushwa iwe rahisi kutumikana kutoa matokeo yasiyo akisi hali halisi.
 
Mkuu, swala la Lowassa, pamoja na muda husika na mazingira ya wakati huo na sasa ni tofauti sana. Lakini hayo tuyaache huko huko nyuma, tusonge mbele sasa hivi.
Ni muda mwafaka kabisa Mbowe asije akakivuruga chama wakati huu. Akifanya hivyo, atakuwa kafuta kila kitu alichowahi kufanya kukiongoza chama hicho.
 
Bila shaka sasa hivi CHADEMA watakuwa wamepata funzo.
Lakini haya yanayosemwa chinichini ya Mwenyekiti kuwa na watu wake, kama ni kweli hili litamdhalilisha sana Mbowe.

Inaonekana Mbowe sasa anahaha zaidi Chama kukiwasilisha kwa wanaokitaka kikiwa na watu wanaowataka zaidi. Kazi hii inayofanyika siyo kazi ya kutafuta ushindi wa chama kushika madaraka.
 
Mkuu, swala la Lowassa, pamoja na muda husika na mazingira ya wakati huo na sasa ni tofauti sana. Lakini hayo tuyaache huko huko nyuma, tusonge mbele sasa hivi.
Ni muda mwafaka kabisa Mbowe asije akakivuruga chama wakati huu. Akifanya hivyo, atakuwa kafuta kila kitu alichowahi kufanya kukiongoza chama hicho.
Kila siku huwa nasema kiongozi mzuri hapaswi kukaa zaidi ya miaka 10. Na kipimo Cha kwanza kwangu kuwa huyo Mbowe anaanza kuharibu mazuri yake ni kumuokota Lowassa. Huwezi kuchukua mgonjwa ukampa nafasi ya kugombea urais. Hakuna mazingira yoyote yaliyofanya Lowassa astahili kugombea kupitia cdm zaidi ya fedha zake chafu.
 
Msigwa kasema huyo aliyezoea kunyofoa watu kwenye chama safari hii ananyofolewa yeye. 😆😆
Eti anamsema Msigwa kaongoza muda mrefu, miaka Saba!! Bila shaka Msigwa alikusudia kujilinganisha na Mwenyekiti hapa.😀😀
 
Kila siku huwa nasema kiongozi mzuri hapaswi kukaa zaidi ya miaka 10. Na kipimo Cha kwanza kwangu kuwa huyo Mbowe anaanza kuharibu mazuri yake ni kumuokota Lowassa. Huwezi kuchukua mgonjwa ukampa nafasi ya kugombea urais. Hakuna mazingira yoyote yaliyofanya Lowassa astahili kugombea kupitia cdm zaidi ya fedha zake chafu.
EEEeeenHEEEeeee!

Najuwa mkuu 'Tindo'. Nitasahau vipi nadharia yako hiyo!

Sasa tusonge mbele,kazi ni kubwa sana kuwaondoa CCM wanaotumia fedha za waarabu kutuchanganya akili.
 
Lakini haya yanayosemwa chinichini ya Mwenyekiti kuwa na watu wake, kama ni kweli hili litamdhalilisha sana Mbowe.
Kama yatabainika kuwa ni kweli itambidi ajiuzulu mara moja na Tundu Lissu akaimu ili tuingie kwenye Chaguzi ndogo na baadae mchakato wa kumpata Mwenyekiti ufanyike.
 
kuharibu mazuri yake ni kumuokota Lowassa. Huwezi kuchukua mgonjwa ukampa nafasi ya kugombea urais. Hakuna mazingira yoyote yaliyofanya Lowassa astahili kugombea kupitia cdm zaidi ya fedha zake chafu.
Nilisema tusonge mbele, lakini kipande hiki nilichonyanyua hapo kimenirudisha nyuma.
Binafsi sikudhani kuwa ujio wa Lowassa CHADEMA wakati ule, haikuwa sababu ya "pesa"; lakini kama ilikuwa hivyo, sina la kutetea hapa.
Kwa upande wa pili, ambao pengine wewe hukuutilia maanani: Lowassa wakati ule ilionyesha kuwa anao wafuasi wa kutosha ambao angewatumia kumpa ushindi dhidi ya CCM. Hii ni sababu pekee niliyoiona kuwa ya msingi kwa CHADEMA kumpa nafasi ndani ya chama chao.
Kwangu, njia yoyote a kuiondoa CCM madarakani, kama inafanikiwa, ninaiunga mkono, hata ujio wa huyo Lowassa wakati ule.
Ni kwa msingi huo pekee, niliouona na kuuvumilia wakati huo.
Sasa naomba tusonge mbele. CHADEMA iondokane na hivi vikwazo vinavyoletwa ndani ya chama chao toka nje.
 
Mkuu 'Erythro', ujumbe muhimu alioutoa kwenye habari hiyo ni huu hapa:'

"... yule anayetaka kunyofoa watu atanyofolewa mwenyewe,...na hatuogopi mtu"

Mengine yote ni kelele tu za kupoteza lengo.
Ni wakati mwafaka sasa CHADEMA ijisafishe; hakuna njia nyingine zaidi. Kirusi kikuu ni Mbowe, bila ya kumung'unya maneno.
Hakuna ushahidi wowote kuthibitisha hilo, kama unao tuwekee humu, tena Mbowe ndiye alipambana sana kuhakikisha Msigwa anakuwa Mwenyekiti wa Kanda kwa kumshawishi Ole Sosopi ajitoe kumpisha Kaka yake
 
Back
Top Bottom