Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Ningependa Tundu Lissu ashinde Uenyekiti CHADEMA kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa CCM yenyewe

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Ningependa Tundu Lissu ashinde Uenyekiti CHADEMA kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa CCM yenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shida yenu mnapenda majibu mepesi kwa maswali magumu.Tangu lini mfuasi wa dhati wa Chadema atakubali ushauri wa hao wawili kuhusu nani anastahili kupigiwa kura?

Wao kwa kumpigia debe Mbowe wanajenga hisia kuwa Mbowe ni kibaraka wa CCM hivyo kuwafanya watu wampigie kura Lissu.

Msigwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu kila mtu anajua anavyomchukia Mbowe.

Bahati mbaya wako watakaoingia mkenge na kumpigia kura Lissu ambae CCM wanamtaka. Lengo lao ni Lissu ashinde halafu Mbowe asuse. Ikitokea hivyo CDM itakuwa ICU by the time Uchaguzi Mkuu unafanyika.

Amandla...
Uongo
 
Ndio maana nasema mnapenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Unadhani watu watampigia kura Mbowe katika uchaguzi wa CHADEMA kwa sababu hao wanampigia debe? Au ndio wataona ni uthibitisho kuwa Mbowe ni mamluki wa CCM na hivyo watampigia kura Lissu?

Chadema wanaamini kuwa CCM wanamuogopa sana Lissu kwa sababu atawasemea ovyo jukwaani! Ukweli ni kuwa CCM hawamtaki Mbowe kwa sababu ya resilience kubwa aliyonayo. Pamoja na kutupiwa kila kitu (yeye na viongozi kufungwa, viongozi waandamizi kuunga mkono juhudi, biashara zake za Tanzania kuhujumiwa, account zake kufungwa) ameweza kuifikisha CDM hapa ilipo pamoja na kukataa kupokea ruzuku za masharti. Wakati huo baadhi ya hao mnaowaona kama mashujaa wakiwa ughaibuni wakichangia mapambano kwa remote. CDM wakimchagua Lissu wataipa CCM ushindi.

Amandla...
CCM kindakindaki hawamtaki Tundu Lisu wanamtaka mshirika wao Mbowe.
 
Omba kwa Katibu Mkuu uwe wakala wake ili mkipigwa msisingizie.
 
Mchungaji Msigwa ameeleza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akizungumza kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, amesema:

"Mimi nam-support Tundu Lissu, ningependa ashinde, lakini ni matatizo yao hayo. Mimi, yeyote atakayeshinda yaani sisi (CCM) tunataka chama kile tukishinde. Yeyote atakayeshinda bado tutakabiliana naye, awe Lissu, awe Mbowe, au mtu mwingine kutoka Burundi, Rwanda. Lakini kwa kuwa mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, nitakabiliana na yeyote. Hata hivyo, kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa faida ya CCM yenyewe, anayepaswa kuwa Mwenyekiti pale ni Lissu."
Soma, Pia: Tundu Lissu: Mchungaji Peter Msigwa ni rafiki yangu, lakini nitamkabili Kisiasa
Kwamba Simba iombe kukutana na Barcelona kwenye fainali na sio Namungo! Ahahahahaha!!
 
Hii kauli ndio itamfuta katika siasa za CCM. Mtu anayemtukana Samia ye ye ndio kamuona bora?
 
Kamwe na katu lissu hawezi kupita. Kwa hiyo Mchungaji Msigwa ajue tu kuwa Mwamba ndiye anayekwenda kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima. awe anapenda au hapendi ni lazima Mwamba ashinde tu.
 
Kamwe na katu lissu hawezi kupita. Kwa hiyo Mchungaji Msigwa ajue tu kuwa Mwamba ndiye anayekwenda kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima. awe anapenda au hapendi ni lazima Mwamba ashinde tu.
 
CCM kindakindaki hawamtaki Tundu Lisu wanamtaka mshirika wao Mbowe.
Una haki ya kuamini hivyo ila mimi sikubaliani na wewe. Naamini kuwa Strategists wa CCM bila shaka wanamuona Mbowe ni threat kuliko Lissu. Mashabiki na wafuasi wa kawaida wanaweza kuamini kama wewe.

Na sio vizuri kumuita Mbowe mshirika wa CCM. Ni yale yale ya kuacha mbachao....

Amandla...
 
Back
Top Bottom