Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Nitazunguka Nchi nzima kuelezea Uongo wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwambie asithubutu kabisa. Aachane na hayo mambo ya kuchafuana.
Yeye akae kwa kutulia apate uteuzi aiwezeshe familia yake.
CCM hawapendagi kabisa wenye viherehere
 
CCM inaazima Mamluki, wameisha hawana pa kushika mara Makonda,mara Makalla na sasa wanajaribu kukodi mamluki akina Pendo na Msigwa. Kwa kweli ccm amekwisha. hata akizunguka hana jipya zaidi ya vituhuma dhidi ya Mbowe,wacha atafune pesa ya walipa kodi kupitia ccm naye kwa sasa ni chawa na badhirifu tu kama wengine. wananchi siyo wale wa zamani. atapoteza muda
 
atakavyo amua........

..wiki iliyopita Msigwa alikuwa anawaambia wananchi Ccm imewapelekea umasikini, leo anataka kugeuza kauli yake?

..Je, Msigwa atakwenda kuwashawishi wananchi kwamba umasikini wao umesababishwa na Mbowe au Chadema?

..Huyu bwana amepotoka. Msigwa alipaswa kutafuta chama kitakachompa platform ya kusema yale aliyokuwa akisema alipokuwa Chadema. Sio chama kitakachomlazimisha ayakane yote aliyoyaamini na kuyasema kwa miaka 20+ na yakampa umaarufu, na uongozi.
 
Shetani akizeeka hujifanya malaika.
 
Atajisambaratisha yeye, hakuna wa kumuamini.
Kondoo wake hawamuamini sembuse wasio kondoo.
 
Ccm kazi yao ni kuchukua takataka(rubbish) wa upinzani waweke kwenye dustbin
 
ni bora akae kimya tu kuliko kutenda dhambi hiyo ya kusaliti wenzake waliokuwa pamoja wakifanya uongo huo. Usaliti haujawahi kumuacha mtu salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…