Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6

Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6

#HABARI Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

#EastAfricaRadioView attachment 2384832


Tuanze hapo kweny jina sio mpiga dili huyu?
Hilo jina ndilo lililompa kanisa na waumini.
Kuna baadhi ya madhehebu hupenda sana shuhuda, hivyo Ukienda kwao, unajiita Hamisi Bakari, sasa umeamua kubadili dini.

Ila hujabadili dini bure, bali una shuhuda zako, za kiuchawi.
Hakuna wa kukupinga kila siku ukienda dhehebuni tunga shuhuda zako mbili, wewe tayari mchungaji.
 
Kama ningekuwa na mamlaka, ningeunda sheria na taratibu maalum za kufuatwa ili kuanzisha makanisa especially hawa walokole,
Maana naona wanajisahau sana
Huko Moshi padri kafanyaje tena!!!
 
Hawa wasukuma ndio wanatuharibia DINI YA KIISLAM, wanatumia majina ambayo kiasili hutumiwa na WAISLAM na hao ndio unakuta wala kitimoto na ujinga mwingi.

Nimesoma na akina SHABANI, HAMISI, JUMA, ABDALA nk wakristo na wala kitimoto. Nilikuwa nawaambia ukitumia hayo majina acheni kula vitu vya kipumbavu maana mnachufua dini nyingine kisa majina.
Wewe ndo mpumbavu.
Yaani ukitaja jina kwa maneno ya kiarabu basi unalioanisha na uislam
 
Huyo afisa ustawi wa jamii,aliyekabidhiwa ni ME au KE?
Kama ni ME,isije ikaleta shida nyingine tena.
 
Wanyama wana akili kutuzidi sisi binadamu. Hivi kweli jitu linaweza kumuingilia mtoto wake wa kumzaa, halafu wa miaka sita?

Yawezekana kauli ya waziri wetu wa afya, mheshimiwa Ummy Mwalimu ni ya kweli. Unaweza kumwona mtu anaongea vizuri na wenzake, kumbe ana ugonjwa wa akili!

Angalia, huyu anajifanya mchungaji na waumini wanamwamini, kumbe akirudi nyumbani anambaka mtoto wake. Na inaonekana alimfukuza mkewe ili apate wasaa mzuri wa kumbaka mtoto. Mijitu kama hii ndio inayoleta laana katika uso wa dunia.

Nawashauri mamlaka husika (vyombo vya sheria), majitu kama haya yafungwe kifungo cha maisha, yasije tena uraiani maana ni laana. Na kabla ya kufungwa, yatandikwe viboko 30 vya nguvu matakoni, ili iwe fundisho kwa wengine wanaopanga kufanya ufedhuli huu.

Ikithibitika kweli (kisheria) alimuingilia huyo mtoto, napendekeza adhabu hii tungeanza na huyu anayejiita mchungaji wakati ni firauni. Hawa ndio wanaosababisha ukame kutokana na laana zao.
 
Hawa wasukuma ndio wanatuharibia DINI YA KIISLAM, wanatumia majina ambayo kiasili hutumiwa na WAISLAM na hao ndio unakuta wala kitimoto na ujinga mwingi.

Nimesoma na akina SHABANI, HAMISI, JUMA, ABDALA nk wakristo na wala kitimoto. Nilikuwa nawaambia ukitumia hayo majina acheni kula vitu vya kipumbavu maana mnachufua dini nyingine kisa majina.
Hata watu wa wambeya nilikuta jamaa anaitwa ally omary ni mkristo nikashangaa
 
Kalpana mama, tafadhali uje utie neno na hapa. Maana hali ni tete. Tukisema jinai haichagui mtu, muwe mnatuelewa.
 
Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

Chanzo: EA Radio


===================


Mchungaji Nurdin Mahakamani kwa kumbaka mtoto wake

Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

Ni Kesi namba 79 ya mwaka 2022, iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Erick Kimaro, katika Mahakama ya wilaya ya Magu inamkabili Mchungaji huyo anayedaiwa kumbaka binti yake wa kumzaa baada ya kumchukua kutoka kwa mama yake waliyeachana.

Inadaiwa kuwa mchungaji huyo aliachana na mke wake mwezi wa saba mwaka huu na mwanamke huyo akaondoka na kwenda kuishi wilayani Bunda mkoani Mara ndipo mchungaji akaamua kuishi na binti yake ambae inadaiwa amekuwa akimuingilia kimwili mara kwa mara hadi majirani walipogundua jambo hilo na kuamua kumuhoji mtoto huyo na kuwathibitishia kuingiliwa kimwili na baba yake huyo.

Aidha baada ya majirani kugundua kwamba binti huyo amefanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji walimpeleka kituo cha polisi na kufungua kesi kisha wakapewa fomu namba tatu ya polisi na kumpeleka hospitali na baadae binti huyo alikabidhiwa kwa afisa ustawi wa jamii wakati kesi ikiendelea.

Na leo hii Oktoba 12, 2022, mshtakiwa huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la kilokole lililopo Kisesa amewakilishwa mahakamani na mdhamini wake Bernard Mashauri aliyedai kuwa mshtakiwa Nurdin Abdalah anaumwa sehemu zake za siri zimevimba na kupelekea kushindwa kutembea.
Ushetani mwingine huu tunaupigia kelele.Lazima itakuwa ushirikina upo ndani yake.
 
Kabla ya kesi akapimwe afya ya akili. Uchungaji huenda ni mchongo.
 
Back
Top Bottom