Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6

Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6

Chanzo: Mwananchi

Mchungaji Nurdin Abdallah wa kanisa la kilokole lililopo Kisesa Mwanza amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu jijini humo kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka sita.

Mchungaji huyo mkazi wa Kisesa, amefikishwa Mahakamani Jumatano ya Oktoba 12, 2022 mbele ya hakimu Mwandamizi wa Wilaya hiyo, Erick Kimaro na kusomewa mashtaka ya kubaka.

Akisoma Mashtaka hayo ya kesi namba 76 ya mwaka 2022, Hakimu Kimaro amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa mke wa mchungaji huyo kabla ya kuachana.

Mchungaji huyo aliachana na mkewe Julai 2022 na kwenda kuishi Wilaya ya Bunda mkoani Mara huku yeye akibaki kuishi na mtoto wake huyo wa miaka sita ambaye anadaiwa kumuingilia kimwili mara kwa mara.

Majirani waligundua jambo hilo na walipomhoji mtoto huyo aliwathibitishia kuingiliwa na baba yake hivyo kuchukua uamuzi wa kumpeleka mtoto Kituo cha polisi kufungua kesi, na kupewa fomu namba tatu (PF3), akapelekwa hospitalini.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuwa mahakamani badala yake aliwakilishwa na mdhamini wake, Bernad Mashauri aliyedai mshtakiwa huyo amevimba sehemu zake za siri ameshindwa kutembea.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Kimaro aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, 2022 huku akimtaka kuhakikisha mshtakiwa huyo afike na vyeti vya hospitali kithibitisha kuumwa kwake.
 
Mchungaji anaitwa Nurdin Abdallah?

Na imekuwaje siku hizi habari za wanaojiita watumishi wa Mungu wamekuwa wabakaji watoto? Ni kwamba maisha yao ya kuigiza utakatifu yanawafanya washindwe kutongoza ama kuna kilichojificha nyuma ya pazia.

Huyu Bw. Nurdin apigwe kifungo cha maisha tu akawe mke wa watu jela huko, wamlawiti na yeye.
 
Ndio maana mimi binafsi hakuna kitu nisichopenda kama ngono!
Ngono imepelekea watu wengi kuwa kwenye wakati mgumu sana ,tamaa ya ngono kisha kukamata hata akili ya utambuzi inahama, ikija kurudi inarudi na kilio.

Kama hakuna propaganda kwenye hili nampa pole binti kwa kadhia hiyo maana hilo jeraha atakalo kua nalo kwamba baba yake mzazi amewahi kumuingilia halita mtoka siku zake zote.
 
Mchungaji anaitwa Nurdin Abdallah?

Na imekuwaje siku hizi habari za wanaojiita watumishi wa Mungu wamekuwa wabakaji watoto? Ni kwamba maisha yao ya kuigiza utakatifu yanawafanya washindwe kutongoza ama kuna kilichojificha nyuma ya pazia.

Huyu Bw. Nurdin apigwe kifungo cha maisha tu akawe mke wa watu jela huko, wamlawiti na yeye.
Kubaka ni jambo la kwanza... Kambaka mtoto wa umri wa miaka sita halafu mwanae wa kumzaa
Visa vya namna hii maranyingi sio tamaa za kingono bali ni masharti ya mganga
 
Visa vya namna hii maranyingi sio tamaa za kingono bali ni masharti ya mgang
Hamna cha masharti ya mganga wala nini. Ujinga tu umemjaa kichwani.
Mtu kazidiwa usiku halafu nje domo zege akaona ampelekee mtoto hilo dudu
 
Kubaka ni jambo la kwanza... Kambaka mtoto wa umri wa miaka sita halafu mwanae wa kumzaa
Visa vya namna hii maranyingi sio tamaa za kingono bali ni masharti ya mganga
Hivi mtu na akili yako mganga anakupa sharti ukambake mtoto wako,hivi yeye alishafanya hivyo,au akiambiwe afanye kitendo hicho Kwa mwanawe atafanya?
 
Hivi mtu na akili yako mganga anakupa sharti ukambake mtoto wako,hivi yeye alishafanya hivyo,au akiambiwe afanye kitendo hicho Kwa mwanawe atafanya?
Watu wamekariri mambo ya mwaka 47
 
Mchungaji wa kilokole anaitwa nurdin abdalah? huyu anaendelea kuongeza idadi ya wachungaji na manabii wa mchongo.
 
Jamani miaka sita ni katoto kadogo! kadogo sana..upaja wa mtu mzima kupenya pale ni ngumu sana.kitoto chenyewe kinalingana na oomb! Inakuwaje hapo sasa.......sawa bana!! msijesema hatukusema
 
Jamani hawa watu wangekua wanapelekwa kwenye kitanzi moja kwa moja haina haja ya kujaza kesi mahakamani wakati kila kitu kipo wazi.

Nachukia sana wababa wanaong'ang'ania kuishi na watoto wadogo kisha kuwageuza ndivyo sivyo
Lkn mbona mnawokomalia sana me???...wkt ke wanabaka sana me wadogo ambao hawatii mimba?......kweli ke Dunia ni yao.
 
Kuna KE kafungwa maisha kwa kubaka katoto ka kiume,uzi ulikua humu na msimamk ule ule wale kitanzi tu mbakaji ni mbakaji tu
Lkn mbona mnawokomalia sana me???...wkt ke wanabaka sana me wadogo ambao hawatii mimba?......kweli ke Dunia ni yao.
 
Kweli, Yaani fikiria eti Muislamu anatoka kwenye Uislamu wake huko anazuga anaanzisha kanisa, kumbe mbakaji, hii ni too much
Tembelea nchi za kiarabu wakristo wa kiarabu wana majina ya kiislamu,karibia wote ukiuliza wanasema,hawajawahi kuwa waislamu,ni wakristo toka asili ya mababu na mabibi.
 
Wewe ndo mpumbavu.
Yaani ukitaja jina kwa maneno ya kiarabu basi unalioanisha na uislam
Wapo wakristo wengi,tumesoma nao,wana majina ya kiislamu.Waarabu wakristo pia,wana majina ya kiislamu,lakini ni wakristo,nchi nyingi za kiarabu wapo.
 

Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

Chanzo: EA Radio
====


Mchungaji Nurdin Mahakamani kwa kumbaka mtoto wake

Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

Ni Kesi namba 79 ya mwaka 2022, iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Erick Kimaro, katika Mahakama ya wilaya ya Magu inamkabili Mchungaji huyo anayedaiwa kumbaka binti yake wa kumzaa baada ya kumchukua kutoka kwa mama yake waliyeachana.

Inadaiwa kuwa mchungaji huyo aliachana na mke wake mwezi wa saba mwaka huu na mwanamke huyo akaondoka na kwenda kuishi wilayani Bunda mkoani Mara ndipo mchungaji akaamua kuishi na binti yake ambae inadaiwa amekuwa akimuingilia kimwili mara kwa mara hadi majirani walipogundua jambo hilo na kuamua kumuhoji mtoto huyo na kuwathibitishia kuingiliwa kimwili na baba yake huyo.

Aidha baada ya majirani kugundua kwamba binti huyo amefanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji walimpeleka kituo cha polisi na kufungua kesi kisha wakapewa fomu namba tatu ya polisi na kumpeleka hospitali na baadae binti huyo alikabidhiwa kwa afisa ustawi wa jamii wakati kesi ikiendelea.

Na leo hii Oktoba 12, 2022, mshtakiwa huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la kilokole lililopo Kisesa amewakilishwa mahakamani na mdhamini wake Bernard Mashauri aliyedai kuwa mshtakiwa Nurdin Abdalah anaumwa sehemu zake za siri zimevimba na kupelekea kushindwa kutembea.
Huyu alipewa Maelekezo aje akichafue huku kwetu ili asomeke mchungaji wakati inafahamika Kwa majina yake alitumwa ahamishie fedheha huku, si ana jina la maorthodox wa Galilaya ndio hutumia haya majina kwenye uchungaji wao.
 
Back
Top Bottom