MCL: DPP kurudisha fedha za 'plea bargain' kwa waliodhulumiwa

MCL: DPP kurudisha fedha za 'plea bargain' kwa waliodhulumiwa

Wengi hii habari hamjaielewa mnakurupuka tu. Wataorudishiwa ni wale ambao wameathiriwa na hao waliofanya na kukiri makosa. Zingine zitabaki serikalini.
Mfano ulidhulumu watu, ukapelekwa mahakamani ukakiri kosa. Hivyo pesa itarudishwa kwa waliodhulumiwa
Pesa unazozisema wewe zina utaratibu tofauti za kesi za madai.

Pesa zinazozungumziwa hapa ni zile za plea-bargain ambazo hazijatungiwa sheria ya matumizi yake
 
Duuh, huyu "SHUJAA WA AFRIKA" alikuwa kiboko balaa....!!

Huyu shujaa gani aliyekuwa anahusudu dhuluma to that extent..?

Shujaa aliyedhulumu mpaka uhai wa watu. Hawa nao warudishiwe uhai wao..!!
Shujaa mvurugaji
 
Wakina nani wamedhulumiwa? ni vyema hao watako rejeshewa wakawekwa wazi na tukajua walivyo dhulumiwa na walikuwa na makosa gani?
naona huyu flamingo anataka kutupiga.
 
Duuh, huyu "SHUJAA WA AFRIKA" alikuwa kiboko balaa....!!

Huyu shujaa gani aliyekuwa anahusudu dhuluma to that extent..?

Shujaa aliyedhulumu mpaka uhai wa watu. Hawa nao warudishiwe uhai wao..!!
Upande wa pili wa shujaa wa Afrika ndo tunaanza kuuona
 
Ile dhuluma ya Uchaguzi wa 2020 ndio ilikuwa dhuluma kuu, Majimbo mengi wamewekwa Wabunge bila ridhaa ya Wananchi.
unawaza ubunge watu wamedhurumiwa pesa zao wewe mstaafu pambana na hali yako.
 
Biswalo Mganga naye akamatwe na kuhojiwa juu ya kudhulumu pesa hizo.
 
Yaani nyumbu humu ni wengi sana. Yaani hukumu ya mahakama anaweza akaibadirisha DPP. Jaribu kusoma sheria kidogo ili unyumbu upungue kidogo.
Wewe yatima wa kuonewa huruma, hebu weka sheria hiyo hapa. Mpaka sasa ni kwamba hata Mahakimu wenyewe wakiamua kumwaga siri za hukumu walizokuwa wakizitoa kwa shinikizo za dhalimu mwendakuzimu, huo uso wako utauficha wapi?

Acha kabisa kutetea dhuluma za wazi zilizokuwa zikifanyika nchini mchana kweupe. Mahakama hazikuwa huru kama unavyotaka kudai kwani nao walilazimika kushiriki katika ujambazi wa dola. Kama ulimpenda nenda kanywe naye chai jehanum!
 

DPP kuachia mabilioni ya fidia​



SUNDAY JUNE 20 2021​

dpppic

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu akizungumza na waandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd wakati wa mahojiano maalumu Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Picha Sunday George

Summary

  • Wakati baadhi ya wanasheria na wadau mbalimbali wakihoji kuhusu akaunti ya malipo ya fedha za fidia zinazolipwa na washtakiwa wa makosa ya jinai wanaokiri mashtaka yao, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amesema yuko katika hatua ya mwisho kuzitoa katika akaunti hiyo ili zigawiwe kwa wahusika.


By James Magai
More by this Author
adijapic

By Hadija Jumanne
More by this Author

Dar es Salaam. Wakati baadhi ya wanasheria na wadau mbalimbali wakihoji kuhusu akaunti ya malipo ya fedha za fidia zinazolipwa na washtakiwa wa makosa ya jinai wanaokiri mashtaka yao, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amesema yuko katika hatua ya mwisho kuzitoa katika akaunti hiyo ili zigawiwe kwa wahusika.

Akaunti hiyo maalumu iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilifunguliwa na DPP mstaafu, Biswalo Mganga kwa lengo la kupokea na kuhifadhi fedha za fidia zinazolipwa na washtakiwa wanaokiri mashtaka yao kwa kufuata utaratibu wa makubaliano ya kumaliza kesi hizo baina ya pande hizo mbili (Plea-bargaining).

Hata hivyo, wadau mbalimbali, wakiwemo wanasheria wamekuwa wakihoji pesa hizo kulipwa katika akaunti hiyo wakiita kuwa ni akaunti ya mtu binafsi na hivyo kutilia shaka matumizi yake.

Wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Aprili 28, mwaka huu, waziri wa wizara hiyo, Profesa Palamagamba Kabudi alisema kuwa jumla ya Sh35.07 bilioni zilikuwa zimesharejeshwa na washtakiwa mbalimbali waliokiri makosa yao.

Lakini pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dk Charles Kichere katika taarifa yake ya ukaguzi ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020 alieleza kuwa mpaka wakati huo wa ukaguzi akaunti hiyo ilikuwa na pesa kiasi cha Sh52 bilioni.

Hata hivyo, CAG akasema kuwa pesa hizo zimekaa tu huko kwa sababu hakuna Sheria ya Matumizi ya Pesa hizo.




Katika mahojiano maalumu na Mwananchi juzi, DPP mpya, Sylvester Mwakitalu, pamoja na mambo mengine alizungumzia akaunti hiyo na fedha zilizomo na akautoa umma hofu akisema ziko salama na kwamba yuko katika mchakato wa kuzihamisha ili ziende mahali panakohusika.

DPP Mwakitalu alisema kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kuzitoa katika akaunti hiyo kwa ajili ya kuwalipa wahanga wa uhalifu na zile za Serikali zitaingia katika mfuko mkuu.

“Serikali ilifungua akaunti kwa ajili ya kuweka fedha hizo ambazo zinatokana na makubaliano hayo ya pre-bargain, hiyo akaunti iko Benki Kuu ya Tanzania na fedha zimekuwa zikiingizwa huko,” alisema na kuongeza:

“Sasa kuna changamoto kidogo kwenye hiyo pre-bargain, hususan malipo ya hizi fidia zinazolipwa kwenye hiyo akaunti. Wahanga au waathirika wa hayo makosa ya uhalifu, wakati mwingine wamekuwa ni individual (watu binafsi au taasisi binafsi).”

Alisema kuwa wahanga wa matukio ya uhalifu wamekuwa wakifika ofisini kwake wakiuliza namna ambavyo wataweza kupata pesa zao hizo.

“Kwa hiyo tunakamilisha utaratibu wa kuzitoa kwenye hiyo akaunti ili fedha za hao wahanga zilipwe kwa wahanga na zile ambazo ni za Serikali basi ziingie serikalini.

“Hilo tunaendelea nalo, tunalifanyia kazi na soon (karibuni)tutalikamilisha. Lakini fedha hizo ziko salama kabisa,” alisisitiza DPP.



Kufuta kesi na kuondoa mashtaka yasiyodhaminika

Katika mahojiano hayo pia DPP Mwakitalu alitangaza habari njema kwa mahabusu akisema ameshaanza na anaendelea na mchakato huo wa kuwafutia kesi washtakiwa na wengine kuwaondolea mashtaka yasiyodhaminika kulingana na aina ya ushahidi uliopo, kama moja ya hatua za kupunguza msongamano wa mahabusu magerazani.

Akizungumzia msongamano wa mahabusu magerezani, DPP Mwakitalu kwanza alisema zipo sababu nyingi zinazosababisha msongamano magerezani na kubainisha hatua hizo ambazo ameshaanza kuzichukua.

Alisema msongamano magerezani unatokana na sababu nyingi, akiainisha kuna watuhumiwa wanaoshtakiwa kwa makosa ambayo yana dhamana lakini wanakosa mtu wa kuwadhamini au wanashindwa kutimiza vigezo vya dhamana, na hivyo wanapelekwa mahabusu.

Pia alisema wako mahabusu wanatuhumiwa kutenda makosa ambayo hayana dhamana, kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Sasa haya ni mambo ambayo mengine yanahitaji hatua tu za kiutendaji na mengine yanahitaji marekebisho ya sheria,” alisema DPP Mwakitalu na kuongeza:

“Kwa hiyo ili kupunguza msongamano wa mahabusu, nitafanya yale ambayo yanaihusu ofisi yangu na nina uwezo nayo kisheria.”

Alisema kwa sasa anapitia majalada yote kuangalia yale ambayo yana ushahidi wa kutosha kuthibitisha kosa, ambayo ataendelea nayo na ataomba mahakama isaidie yasikilizwe haraka.

“Pengine tutahitaji hata vikao maalumu pale ambapo mahakama itakuwa na uwezo huo,” alisema DPP Mwakitalu na kufafanua zaidi:

“Kesi ni ya muda mrefu, tumepata mashahidi wetu, tunaweza tukaomba isikilizwe siku mbili tatu nne mfululizo ili izipunguze.”

Kuhusu makosa ambayo hayana dhamana na watu wako mahabusu na akiona kwamba kwa ushahidi uliopo bado hautoshi atayafanyia uamuzi kuyaondoa na kuacha mashtaka mengine ambayo yanadhaminika.

“Upelelezi ukikamilika na tukapata ushahidi basi tutaendelea nayo.”

Alisema kwa mashauri ambayo upelelezi utachukua muda mrefu kwa sababu kuna kesi nyingine ambazo upelelezi unahitaji muda au unahitaji kushirikisha taasisi nyingine, au unahitaji ushahidi kutoka nje, hayo watashauriana cha kufanya.

“Tunaweza kuamua kuyaondoa kwanza mahakamani. Tukikamilisha upelelezi tunajiridhisha kuwa upelelezi unatosha basi tunayarudisha,” alisema.

Miongoni mwa mahabusu ambao wameshaanza kufikiwa na neema hiyo ya DPP Mwakitalu ni pamoja na viongozi wa Uamsho, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya ugaidi ambao walikuwa wameshakaa mahabusu kwa takribani miaka saba.

Viongozi hao wa Uamsho walianza kuachiliwa huru kutoka mahabusu kuanzia Jumanne wiki hii kwa awamu tofautitofauti, baada ya DPP kuwafutia kesi ya ugaidi iliyokuwa ikiwakabili, ambapo kundi la mwisho lilitoka jana baada ya kukamilisha taratibu za kimahakama na za kimagereza.

Hata hivyo, licha ya DPP kuwafutia kesi washtakiwa wote katika kesi hiyo namba 121 ya mwaka 2020, wawili miongoni mwao walikwama na kulazimika kusalia gerezani kwa kuwa wanakabiliwa na kesi nyingine tofauti jijini Mwanza.

Hadi wanaachiliwa huru juzi, viongozi hao walikuwa wameshakaa mahabusu kwa miaka saba kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ya ugaidi ambayo ni miongoni mwa makosa yasiyo na dhamana kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Kwa muda mrefu wadau na wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakipaza sauti za kutaka viongozi hao waachiwe, kutokana na kukaa muda mrefu bila kesi yao kusikilizwa, huku Serikali ikieleza kuwa kuchelewa kusikilizwa kulikuwa kunatokana na kuchelewa kukamilika kwa upelelezi, ambao ulikuwa unafanyika mpaka nje ya nchi.
 
Wewe yatima wa kuonewa huruma, hebu weka sheria hiyo hapa. Mpaka sasa ni kwamba hata Mahakimu wenyewe wakiamua kumwaga siri za hukumu walizokuwa wakizitoa kwa shinikizo za dhalimu mwendakuzimu, huo uso wako utauficha wapi?

Acha kabisa kutetea dhuluma za wazi zilizokuwa zikifanyika nchini mchana kweupe. Mahakama hazikuwa huru kama unavyotaka kudai kwani nao walilazimika kushiriki katika ujambazi wa dola. Kama ulimpenda nenda kanywe naye chai jehanum!
Hujui kitu nyamaza wewe ni sawa na yule mnyama wa bunga za Serengeti na Ngorogoro mkuu!
 
Back
Top Bottom