Pre GE2025 MDAHALO: Freeman Mbowe amekacha, Tundu Lissu na Odero Charles Odero kushiriki

Pre GE2025 MDAHALO: Freeman Mbowe amekacha, Tundu Lissu na Odero Charles Odero kushiriki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bezecky

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
494
Reaction score
897
IMG-20250117-WA0106.jpg

Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utakuwa leo Ijumaa 17/01/2025 kuanzia saa 3:30 Usiku, katika Ukumbi wa Rwegechura Hall katika ofisi za TANGANYIKA LAW SOCIETY (TLS) Mikocheni Mtaa wa CHATO DSM, Ghorofa ya pili.

Kwa wanaotaka kuhudhuria mdahalo huo watume majina yao kupitia Whatsapp namba 0766662533 na waje na vitambulisho vyao, mwisho wa kuingia ukumbini ni saa mbili kamili usiku.

Pia soma: - Mbowe: Ilikuwa ghafla sana Lissu kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

NB: Mpaka muda huu wagombea waliothibitisha kushiriki mdahalo ni hao wawili wanaonekana pichani, KARIBUNI SANA.
 
Nilishawahi kusema hapa kwamba nitashangaa sana kama Mbowe atashiriki huu mdahalo.

Na nikisema akishiriki nitamuina hajitambui kuliko nilivyofikiri.

Naona kajua atagalagazwa na Lissu vibaya sana.
Kufanya mdahalo au mahojiano na Lissu inabidi uwe umejipanga na uko vizuri kichwani.

Kile kidada cha Clouds kimejitia aibu baada ya kujaribu kufanya mahojiano na Lissu bila kujipanga.

Kwangu mimi EA naona watu wawili kufanya nao mdahalo au mahojiano hujajipanga utapata aibu ni Lissu na Miguna Miguna.
 
Lissu na Miguna wana uwezo wa asili halafu wamejiongeza kwa kusoma sheria halafu wanafanya mazoezi ya ubishi wa kifalsafa kila siku.

Lissu kabla ya kufanya ubishi kwanza anakuletea ubishi kuhusu mazingira ya kubishana huo ubishi 😂😂😂.
 
1737106619467.png

Niliwaambia hata kama Mbowe hajaenda shule lakini si kilaza kiasi hiki cha kukubali kufanya Mdahalo na Tundu Lissu.

Nakupongeza Mbowe kwa kuukwepa mtego. Walikuwekea mtego ama ni kwa makusudi au kwa kutokujua. Kuwa ukae ukashindane hoja na Tundu Lissu. Umewashtukia. Tundu Lissu usikubali kukaa naye kwenye mdahalo. Atakuchana chana halafu watu watakuchambia.

Pia soma: - Uchaguzi 2025 - Mbowe: Ilikuwa ghafla sana Lissu kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

Hongera sana kwa kuamua kutoshiriki maana ndo ilikuwa unaenda pigiliwa msumari wa mwisho kwenye jeneza lako.
 
Odero Odero yuko vizuri sana, leo kamwaga sera zake kwenye kipindi cha kumepambazuka cha radio one
 
Nakupongeza Mbowe kwa kuukwepa mtego. Walikuwekea mtego ama ni kwa makusudi au kwa kutokujua. Kuwa ukae ukashindane hoja na Tundu Lissu. Umewashtukia. Tundu Lissu usikubali kukaa naye kwenye mdahalo. Atakuchana chana halafu watu watakuchambia.

Hongera sana kwa kuamua kutoshiriki maana ndo ilikuwa unaenda pigiliwa msumali wa mwisho kwenye jeneza lako.
Kwa hiyo mgonjwa akafie nyumbani sio? 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom