MDAHALO: M4C, Hatima ni Mageuzi au Mapinduzi?

MDAHALO: M4C, Hatima ni Mageuzi au Mapinduzi?

Baada ya kukusoma , nimegundua kwamba we ni mwoga wa mabadiliko. Mtu yeyote anayeogopa kubadilika kutoka sehemu moja kwenda nyingine hawezi kupata maendeleo.

Umemgundua Shayu mapema kuwa ni Mwoga aliyekata tamaa! Shayu bado analalamika wakati watu wengi wameshatoka tumeshatoka kwenye hiyo stage.

Kuandika maneno mengi ya kulalamika hayasaidii kitu zaidi ya kuchosha macho kufuatilia ujinga wa mtu! Ameshindwa kuona kwa macho yake kuwa, ameshindwa kutambua kuwa tatizo ni mfumo. Kumbuka, tumeona mabadiliko kadhaa kwenye uongozi wa nchi chini ya CCM.
1: Angalia uongozi wa awamu ya kwanza chini ya JK. Nyerere alijali wanyonge zaidi.
2: AH. Mwinyi aka-anza
kuubadili Uongozi na kuwa Utawala katika awamu ya pili.
3: Katika awamu ya Tatu chini ya BW. Mkapa akabadili neno NDUGU na kuwa MHESHIMIWA
kwa viongozi wa kisiasa! Akakumbatia mabepari nao wakamtumia kama tambara la deki kunyonya rasilimali za nchi, yeye aliwawadharau wananchi masikini wa nchi hii hata walipo piga kelele kulalamika-aliwaita majina mbali mbali ya kebehi na dharau!
4. Chini ya mfumo wa ki-CCM hiyo hiyo katika awamu ya nne ya JK. Kikwete, tumeshuhudia ni tofauti na awamu zingine zote. Awamu hii kila mwenye macho anaendelea kushuhudia gap la walionacho na wasio nacho linazidi kupanuka, pia sarakasi za Serikali katika kukandamiza walala hoi, kuwaua, kuwajeruhi wanaopiga kelele, kuhujumu rasilimali za nchi, kuwafukuza wananchi kwenye maeneo yao na kupewa matajiri na Serikali ilivyowekwa mfukoni na wenye nazo. Serikali kujipambanua kuwa ni dhaifu haiwezi kupambana na mafisadi!

Watanzania wanataka sasa kubadili MFUMO kutoka ule wa ki-CCM kwenda mwingine nao si mwingine bali wa KI-CHADEMA!
 
Umemgundua Shayu mapema kuwa ni Mwoga aliyekata tamaa! Shayu bado analalamika wakati watu wengi wameshatoka tumeshatoka kwenye hiyo stage.

Kuandika maneno mengi ya kulalamika hayasaidii kitu zaidi ya kuchosha macho kufuatilia ujinga wa mtu! Ameshindwa kuona kwa macho yake kuwa, ameshindwa kutambua kuwa tatizo ni mfumo.Kumbuka, tumeona mabadiliko kadhaa kwenye uongozi wa nchi chini ya CCM.
1: Angalia uongozi wa awamu ya kwanza chini ya JK. Nyerere alijali wanyonge zaidi.
2: AH. Mwinyi aka-anza
kuubadili Uongozi na kuwa Utawala katika awamu ya pili.
3: Katika awamu ya Tatu chini ya BW. Mkapa akabadili neno NDUGU na kuwa MHESHIMIWA
kwa viongozi wa kisiasa! Akakumbatia mabepari nao wakamtumia kama tambara la deki kunyonya rasilimali za nchi, yeye aliwawadharau wananchi masikini wa nchi hii hata walipo piga kelele kulalamika-aliwaita majina mbali mbali ya kebehi na dharau!
4. Chini ya mfumo wa ki-CCM hiyo hiyo katika awamu ya nne ya JK. Kikwete, tumeshuhudia ni tofauti na awamu zingine zote. Awamu hii kila mwenye macho anaendelea kushuhudia gap la walionacho na wasio nacho linazidi kupanuka, pia sarakasi za Serikali katika kukandamiza walala hoi, kuwaua, kuwajeruhi wanaopiga kelele, kuhujumu rasilimali za nchi, kuwafukuza wananchi kwenye maeneo yao na kupewa matajiri na Serikali ilivyowekwa mfukoni na wenye nazo. Serikali kujipambanua kuwa ni dhaifu haiwezi kupambana na mafisadi!

Watanzania wanataka sasa kubadili MFUMO kutoka ule wa ki-CCM kwenda mwingine nao si mwingine bali wa KI-CHADEMA!

Katika Afrika ni mapinduzi mangapi yamefanyika? Ni vyama vingapi vimetolewa madarakani? na walioingia hawakuleta mapinduzi yeyote kwasababu nia yao ilikuwa tu kuingia madarakani na sio kuleta mabadiliko kwa watu na kwa Taifa kwa Ujumla? Bila program makini wataenda kufanya nini Ikulu? Tuache uchama tujadili ''ideas''
 
M4C ni kiini macho cha kupata dola fullstop. hamna mikakati mahsusi ya kubadilisha serikali na mifumo yake kadhaa wa kadhaa ikiwemo. Kwa mfano hii theme ya ufisadi inayotawala siasa zetu kwa sasa, si Mbowe wala Dr Slaa aliyediriki kwenda hatua moja mbele na kusema hatua gani mahsusi zitachukuliwa kwa wahusika hawa pindi wakipata dola na hii ni uvugu vugu usioendana na matakwa ya watz wengi. Kwenye kura za maoni za katiba mpya wapo wananchi wengi wanadiriki bila haya wala kuulizwa kwamba wasisahau katiba kuwashughulikia mafisadi kwa adhabu kali ikiwemo kunyongwa, sasa CDM hawako page moja na kiu ya mageuzi hapa Tz namna hii.

A movement ni mass mobilization ya wananchi ili kupata nguvu kubwa ya kuwawakilisha hawa watu na mawazo yao na kutekeleza kiu yao ya muda mrefu, bila CDM kuoanisha taswira ya jamii (siyo lazima wawanyonge wahusika wa ufisadi ili kuuzika ufisadi wenyewe ) na yao inayolalia kwenye mantiki ya kua Taifa linahitaji kua tune up kidogo tu kwa kubadilisha vipaumbele na chama, kwa hili CDM naweza kusema siyo msemaji wa wanachi wa ukweli.

Ili M4C iwe ni mageuzi halisi ni lazima CDM wachore mstari chini waseme watabadilisha kabisa-a total overhaul of a system na siyo kua vugu vugu kama walivyo wenyewe. Change hapa siyo tu kubadilisha chama na sura zile za juu, ni kufukia kabisa mfumo ulioshindwa na wahusika wake waliopita. Kwa nini hatusikii marekebisho ya mikataba ya madini, kurudisha nyumba za serikali, kufilisi wahusika wa ufisadi, sheria za ardhi kwa wazawa, makazi mijini na nyumba za NHC kwa watz wakima cha kati (mnaogopa misaada ya Sabodo), mapinduzi ya kielimu (labda kutumia kiswahili mashuleni), mahakama maalumu kwa ajili ya kesi za ardhi n.k haya ni machache tu tunayotaka sisi wapenda mabadiliko na siyo kubadili rangi za chama na sura, mifano hii ndiyo mageuzi ya ukweli na siyo kupita pita kuikosoa serikali bila kuonyesha kwa kina nyinyi mtaleta nini.
 
Kigarama,

Hapa kidogo sijakuelewa; Maana yako ni kwamba sio watanzania wengi wenye mwamko wa kupigania mabadiliko ya mfumo? Au maana yako ni kwamba kwa kawaida mabadiliko ya mfumo huwa hayapiganiwi na walio wengi?

Mapinduzi ni kweli yataanzia vijijini, lakini hili la mapinduzi kuanzia vijijini sijakuelewa vizuri; wananchi wa vijijini watajiletea vipi mabadiliko kupitia mageuzi? Au maana yako ni kwamba ili mageuzi yawe na tija kwa walio wengi, basi ni muhimu yalenge kuboresha hali za wananchi walio vijijini?

Kwenye blue mimi naamini watu wengi huwa hawapendi kubadili kile walichokizoea hata kama kinawadhuru. Angalia Mexico ambapo watu zaidi ya 40,000 wameuawa kwa kuwa tu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Felipe Calder'on' alianzisha vita dhidi ya wauza madawa ya kulevya na makundi yao. Wamexico wengi walikuwa wamezoea kuishi maisha ya kinyana chini ya magenge ya wauza madawa ya kulevya. Mwisho wa siku Calder'on' akashindwa na Enrique Mena Nieto ambaye alipoingia tu madarakani akasema yeye ataepusha watu wengi kuuawa kwa kuzuia makundi ya ndani ya nchi yasisambaze madawa Mexico na siyo kuzuia makundi hayo kupeleka madawa hayo kwenye nchi nyingine!!

Na kisa kingine ni cha yule muuza madawa ya kulevya wa Jamaica Christopher "Dudus" Coke ambaye wananchi walikuwa wakizuia asikamatwe kwa kuwa tu alikuwa anawapa "huduma za kijamii" kama vile maji na madawa Hospitalini. Mfumo hata ukiwa mbovu kiasi gani ni lazima waathirika wa mfumo huo wafikiri kichanya (Positive thinking) kwa kutenda matendo chanya kwa lengo la kupata matokeo chanya!!

Kwangu mimi napata shida sana ninapomuona mtu anabomoa daraja na kuuza vyuma vya daraja hilo kama chuma chakavu, lakini hapo hapo kuna watu wengine wanamtetea mtu huyo kuiba vyuma hivyo kwa hoja kwamba ana "haki" ya kuiba kwa kuwa tu walioko madarakani hawajamtafutia mtu huyo kazi ya kufanya!!

Kwenye Red ndugu yangu si tu ni imani yangu bali pia ni Historia inaonyesha kwamba Mapinduzi yote hutokea pale watu wa mashambani wanapoasi dhidi ya mfumo ulliopo na kuamua kuchukua mamlaka ya kuongoza mageuzi kwani Mapinduzi maana yake ni Mabadiliko kamili ya mfumo.
 
Mkuu nimekupata except hapo chini,hivi kuna aina ya mrengo ulioutaja hapo chini?Na uliberali ndo unamaanisha "Liberalism"?Maana sijawahi kusikia "mrengo wa kulia wa liberal",naomba tuelimishane.
Mchambuzi said:
hii sio asili ya itikadi yao ya mrengo wa kulia wa kiliberali,

Pia hilo hapo chini unaweza kuniletea mifano hai?Ninavyojuwa mimi,hata hao waliokuwa wakimiliki watumwa,walikuwa wakitumia dini ku justify hilo.
Mchambuzi said:
watumwa walikuwa in revolts, viongozi wa kidini walikuwa wanapinga, philanthropists wanafanya kila aina ya lobbying kumaliza dhambi hii

Pia hapo chini naomba kupishana na wewe,aliyosema huyo mwandishi ni hisia zake?Kwamba Lincolin hakusimamia abolition on moral grounds?Kuna ushahidi gani kuwa aliamini they where no equals na wakati dhana yake iliyowaingiza kwenye civil war ambayo ilikuwa very destructive ni hiyo imani kuwa "all men are created equal"?Nakubaliana na sababu za kisiasa na pia kulinda muungano wa marekani kuwa mojawapo ya manufaa ya slavery abolition na sababu za Lincolin kuja na ile "Emanicipation Proclamation",however hilo la kiuchumi unaweza kunieleza ni kivipi abolition ilitekelezwa ili kusaidia uchumi?Maana kiukweli,waliingia kwenye civil war(zaidi ya watu 650,000 walipoteza maisha yao kwenye vita hivyo), kwasababu watu wa South walikuwa wananufaika kiuchumi na utumwa,si watu wa South peke yake,bali mfumo mzima wa dunia ulikuwa ukinufaika na utumwa kiuchumi.Karl Max aliwahi kusema hayo hapo chini...
Karl Marx wrote, "Without slavery, there would be no cotton, without cotton, there would be no modern industry. It is slavery which has given value to the colonies, it is the colonies which have created world trade, and world trade is the necessary condition for large-scale machine industry."
Mchambuzi said:
Kuna kitabu kimoja by Zinn: A People's History of the United States…, kinaelezea unachozungumza kwa undani sana; Kwa mfano, mwandishi huyu anaelezea jinsi gani Rais Lincoln (ambae anasifiwa kama kiongozi aliyeua utumwa Marekani), alivyokuwa na malengo tofauti kabisa – not on moral grounds, bali kwa sababu za kisiasa, lakini hasa kiuchumi ; Zinn anaeleza kwamba "Lincoln was against slavery but still did not believe blacks were equals." Pia anamnukuu Lincoln akitamka kwamba: "What I do about Slavery and the colored race, I do because it helps to save this Union.
 
1. Mchambuzi, wakati najiunga na JF; my expectation was to read and discuss post kama hii... well, matarajio hayakufikiwa lakini nadhani ilikuwa nina unrealistic expectation, sikjua by then jamiii yenyewe inapenda kusikia vitu vya namna gani?

2. Mimi naomba nitumie maneno ya Kiingereza kutofautisha concept au mirengo hiyo miwili MAGEUZI vs MAPINDUZI... mimi naitai
3. EVOLUTION vs REVOLUTION; sasa kujibu moja ya swali lako... reality ni Kwamba waTanzania wanataka improvement of social services etc... na kwa njia ya EVOLUTION... ingawa ukiwasikia wanasiasa wetu wachanga wanayoongea na kusisitiza ni REVOLUTION... wengine pia hawajui wanachosema.

Reality ni kwamba Revolution ni ngumu ku-catch up hata kwa viongozi wa chama chenyewe kinacho-advocate REVOLUTION... kwa sababu ina maana kubadilisha mifumo mingi including to themselves... this is not what WaTanzania wanachotaka... nina imani coming November 2015, Bado wanapenda shule na waalimu wawe wale wale, vijana wa majeshi yetu watakuwa wale wale ispokuwa viongozi wachache juu, watumishi wa umma kwa kiasi kikubwa watakuwa wale wale... Mifano midogo kama ya kuondoa wakuu wa wawilaya etc na hata majimbo still ni evolution... there is no real big change...

Cha kusikitisha hata wao viongozi wenyewe wanaotamka Mapinduzi/Revolution hawazungumzi mifumo bali kuwaondoa watu fulani [a.k.a Mafisadi] ambayo mpaka leo... kuna confusion na kuweka watu fulani this is just typical evolution... so hakuna jipya... wanaendeleza sera zile zile za CCM. Mfano mabadiliko yaliyofanyika Kenya bado yako kwenye context ya Evolution sio Revolution.
 
Mchambuzi: Nimetumia muda wa dakika kadhaa kupitia uchambuzi wako ambao pia umejikita katika utafiti (ambao unaonesha marejeo "Reference" hafifu kitaaluma). Kwa uchache nataka kusema kuwa sehemu kubwa ya uchambuzi wako umejikita katika kuwatia hofu wafuasi wa M4C kwa kutaka kuwaaminisha kuwa kile wanachokishabikia aidha hawakijui kabisa au wale viongozi wao wanawatumia wafuasi wao huku wakiwa na lengo tofauti lililo nyuma ya pazia kwa maana ya “Mass Movements for Revolutions not for Reforms ". Kitu ambacho binafsi sikubaliani nacho!
Hivyo basi kwa kuwa sitataka kujadili hadidu zako zote, kwangu naomba nijibu kwa ufupi tu sehemu ya Nne ya uchambuzi wako.

SEHEMU YA NNE INASEMA: UFUNGUZI WA MDAHALO;

"Baada ya kuweka mdahalo huu katika Muktadha Sahihi (Right Context) na Kujaribu kujenga Hadidu Rejea (terms of reference), yafuatayo ni masuala muhimu ya kujadili

KWANZA, Je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya
MAGEUZI NA MAPINDUZI?

Jibu: Kwanza kabisa naomba nikujulishe kuwa asilimia kubwa ya wale wanataka na kushabikia M4C ni vijana moto na wenye upeo mkubwa katika uwanja wa siasa na si ajabu umekaa nao darasa moja au ni walimu wako….. (Tzm: Maprofesa na wengineo)

PILI, Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?
Jibu: Kiu wanayo! Ndiyo maana nilieleza hapo juu kuwa yawezekana unachokiandika, aidha unakijua kwa kuwa unakiona uhalisia wake au unajaribu kupima ni kiwango gani cha uelewa walichonacho wale wanaotaka mabadiliko ya utawala na wala si MAPINDUZI kama wewe unavyotaka kuwaaminisha. Kwa ujumla wake watu wanahitaji kupata mikakati mbadala na sura tofauti hasa ikiwa na ile tabia ya kuendesha nchi kama kampuni ya kifamilia.
Lakini kubwa katika hali ya sasa nchi zote zenye maendeleo ni zile zenye utawala wa zaidi ya chama kimoja; anza na Marekani, Uingereza, Ujerumani,Uholanzi Japani Russia na kweingineko….!

TATU, Je: Viongozi wanaoendesha “Mass Movements” wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi “Mass Movements” wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi?

Jibu: Ili kuonesha kuwa CCM sasa hivi inafanya kazi kama chama cha upinzani; kwanza ni hali yake ya kufanya kazi zake kwa kutekeleza matakwa ya Chadema, mpaka hapo utaona kuwa tayari chadema ipo madarakani hivyo kilichobaki ni kuthibitishwa kwa wananchi tu. Jambo la pili ni lile la IMF na WB kuiburuza nchi kana kwamba haina watawala wenye fikra ya kusema hiki ni sawa au la! Kama hivyo mbona kuna mambo ambayo nyerere alikuwa akiwakatalia?!! Utaifa kwanza.

NNE, Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
Jibu: CCM imekuwepo madarakani kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitano sasa! Kama imeshindwa kwenda mbele kwa kipindi chote hicho na badala yake inarudi nyuma kwa kasi ya ajabu! Je, leo itaweza kufanya Reforms ndani ya miaka hii miwili iliyosalia? CCM imebaki ikifanana na baba mlevi ambaye pindi arudipo nyumbani watoto hukimbilia kukaa jikoni na mama yao badala ya kumshangilia na kumkumbatia. Hivyo hata mtoto akikuta amelala sebuleni hatamuamsha. Jipange upya kwani watu wanajua wanchokitaka.
ANGALIZO: kinachoonekana kwa sasa CCM ndiyo inayojiandaa kufanya Mass Revolutions pindi wakishindwa kutokana na jinsi kinavyotumia nguvu nyingi katika kudhibiti wanamageuzi.

Nawasilisha jamvini.

Mkuu hoja zako ni sahihi kabisa na naziunga mkono kwa asilimia mia.

CCM yenyewe inakatisha watu tamaa, Inaelekea siku zote wanajua wanakotaka kufika kutokana na kauli zao lakini wanakuwa hawajui njia (right strategy) ya kufika huko! Mfano rahisi 'rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa' lakini rushwa ndani ya CCM inafanyika waziwazi kama tunavyoshuhudia kwenye chaguzi mbalimbali, au CCM inavyopitisha na kuwapa mafisadi nyadhifa za uongozi katika chama ilhali wakijua kwamba mafisadi ndio wanaoendelea kuisukuma nchi hii kwenye dimbwi la umasikini kwa manufaa yao binafsi na familia zao na marafiki zao... Labda kwa kufafanua hapo, ufisadi ndio unafanya rasilimali zetu sisiweze kutusaidia watanzania kwani hawa mafisadi huingia mikataba isiyo na maslahi kwa nchi na makampuni kama ya dhahabu ambapo huyapa makampuni haya dhahabu karibu zote na sisi kubakiwa na mashimo.

Ni kitu cha ajabu na aibu kubwa nchi yenye dhahabu na madini mengine lukuki serikali ishindwe kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kama vile madaktari na walimu nk

Kwa mantiki hii, Kama wangekuwa wanajua na kufuata njia ya kuondokana na ufisadi, kwa nini wasiwafukuze mafisadi au kuacha kuwapa nafasi za uongozi? Hata hivyo sasa tunajua bila shaka yoyoye kwamba ufisadi ni moja ya 'sera bubu za CCM' Na kwa misingi hiyo pamoja na ahadi nyingi za uongo ambazo hutolewa kwa wananchi wakati wa uchaguzi, maisha bora kwa Kila mtanzania yataendelea kuwa ndoto chini ya CCM.
 
Kasheshe,

Nashukuru kwa mchango wako mzuri wenye kuamsha akili; Kimsingi nakubaliana na wewe lakini mimi mtazamo wangu katika hili kidogo ni tofauti na wa kwako na nitajaribu kujieleza.

Dhana hizi mbili: EVOLUTION & REVOLUTION zinafanana – ni watoto wa tumbo la mama mmoja; vile vile matumizi yake complement each other, na muhimu zaidi, these two concepts are not antagonist to each other; Kwa upande mmoja, katika mazingira ya mjadala wetu au tukitazama dhana ya EVOLUTION kijamii na kisiasa zaidi, maana ya evolution ni gradual and continuous development of ideas and morals (e.g. what is right and what is wrong in the society); Kwa upande mwingine kama tulivyokwisho ona, REVOLUTION ni sudden change ya mfumo; Ni kutokana na character hii ya SUDDEN or ABRUPT Change, ndio maana the term REVOLUTION becomes Very Fearful kwa watu fulani fulani, hasa wale wasioelewa au wale waelewa lakini wanao amini katika Status Quo;

Iwapo kuna tofauti baina ya baina ya dhana hizi mbili - EVOLUTION & REVOLUTION, basi ni katika "TIMING"; naomba nirejee mara moja kwenye maelezo yangu ya awali juu ya dhana ya mapinduzi. Nilisema hivi:

… mapinduzi ni mabadiliko makubwa katika mpangilio na uendeshaji wa maisha ndani ya jamii husika. Mara nyingi mapinduzi hupelekea mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa mahusiano ya jamii, kisiasa, kiuchumi, na mara nyingine kiutamaduni. Mapinduzi hutofautiana kwa:

  • Mbinu;
  • Muda/Duration kufanikisha mapinduzi; na
  • Msukumo/hamasa, mfano kiitikadi n.k;

Ebu tutazame haya masuala matatu kwa undani kidogo Mbinu, Muda, na Msukumo; Kama tunakubaliana kwamba EVOLUTION involves Gradual and Continuous development of morals and ideas, then, Mapinduzi ni Suala tu la "MUDA"; Kwa maana nyingine rahisi, overtime, the gradual and continuous development of ideas vichwani mwa watu in reflection to what is happening to them socially, economically and politically, ndio upelekea UMMA kutaka mabadiliko, na hata ikiwezekana, kwa "MBINU" MAPINDUZI; Vile vile, "MSUKUMO" au "HAMASA" towards change, mfano kwa MBINU ya Mapinduzi, EVOLVES over TIME;

Mimi nadhani, kama wapo watu wenye Uwoga wanaposikia neno "REVOLUTION", basi aidha ni kwa sababu hawaelewi maana halisi ya neno hili au ni wanafiki; Kwa mfano unaweza kuta wanasiasa/viongozi kutwa wanahubiri umuhimu wa mabadiliko ili kuletea wananchi maisha bora, lakini hapo hapo, viongozi hawa wanajisikia uchungu sana iwapo mabadiliko hayo yanaenda kinyume na kile wanachotaka, hata kama mabadiliko hayo ni ya GHAFLA na yana manufaa kwa wananchi walio wengi; Iwapo change ni kwa manufaa ya umma, na viongozi hawa kutwa wanahimiza umuhimu wa change kuboresha maisha ya UMMA, inakuwaje wanakuwa na tatizo iwapo mabadiliko haya yanatokea Suddenly (revolution) lakini hawana tatizo mabadiliko haya kuja Gradually (Evolution)?

Huu ni unafiki - kwa sababu – viongozi hawa wanaona kabisa hali mbaya za wananchi na wanakubali kwamba mabadiliko yanahitajika lakini bado wanapendelea to preserve hali ile ibakie kama ilivyo, unless ibadilike kwa matakwa yao; Kwanini? Kwa sababu, hali zile mbaya za wananchi zinawapa wakubwa hawa comfort, wealth and power. Lakini viongozi hawa wanajisahau kwamba, gradually and continuously, ideas are building up/evolving ndani ya vichwa vya UMMA, na baada ya muda fulani, Evolution of the MIND Will turn into Revolution by the MASS;

Vinginevyo, nadhani viongozi wa CCM wanapenda maisha ya wananchi yabadilike for the better, LAKINI as long the Viongozi KEEP THE TIME, while UMMA KEEP THE CLOCK.
 
Mkuu jmushi1,

Mkuu nimekupata except hapo chini,hivi kuna aina ya mrengo ulioutaja hapo chini?Na uliberali ndo unamaanisha "Liberalism"?Maana sijawahi kusikia "mrengo wa kulia wa liberal",naomba tuelimishane.

Upo sahihi, sikuliweka vizuri; nilicho maanisha ni kwamba: Kwa mujibu wa katiba ya Chadema - Chama hiki kinafuata itikadi ya Uliberali, mrengo wa kati; Uliberali una mirengo mikuu mitatu, mrengo wa kushoto, kati na kulia; Chadema wao ni mrengo wa kati; CUF pia itikadi yao ni ya kiliberali, lakini haielezei mrengo gani, which means ni ile classical liberalism; tuachane na CUF ingawa nadhani wapo watu watakaoshangazwa kidogo na mfanano huu wa ki-itikadi baina na Cuf na Chadema; ni kwamba suala hili halijionyeshi kitatizo kutokana na ombwe la kiitikadi linalkabili siasa zetu, kwani following and support ya vyama vyetu vya siasa ni kwa masuala ya mpito zaidi kama vile personalities, and the only thing permanent may be ni umaskini wa watanzania kwa miaka 50, hence kufanya hili kuwa mtaji wa kisiasa; Vinginevyo itikadi ya mrengo wa kati (uliberali) ambayo Chadema inaifuata, inafahamika (worldwide) kuwa na features kuu zifuatazo:

  • Ongezeko la kodi linaloenda sambamba na ongezeko la vipato vitokanavyo na shughuli za uchumi (progressive taxation); Umiliki binafsi wa mali;
  • Uhuru na haki ya wananchi mbele ya sheria;
  • Uliberali wa kiuchumi;
  • Uliberali wa kijamii.

Maana ya uliberali wa Kiuchumi na Kijamii ni nini?

Uliberali wa kiuchumi kwa maana ipi:

· Kuwapatia wananchi uhuru wa kujiendeshea shughuli zao bila ya kuingiliwa na serikali; Umiliki wa mali binafsi; Serikali kuratibu/rekebisha (regulate) uchumi, lakini wanapinga serikali kukwaza uhuru wa biashara na ushindani katika soko; wanaunga mkono sera za serikali za kuondoa ukiritimba binafsi (private competition) kwa imani kwamba ukiritimba huu unaumiza wananchi maskini;

Uliberali wa jamii kwa maana ipi?
· Haki ya kijamii na uhuru kwa watu wote; Wajibu wa serikali kuinua hali za maisha ya wananchi kwa njia kama vile – ajira, afya, elimu, huku haki za wananchi zikizidi kuimarishwa.

Je wanachama wa Chadema na UMMA kwa ujumla unaelewa haya? Je yanachangia kwa kiasi gani kukiunga Chadema mkono?

Pia hilo hapo chini unaweza kuniletea mifano hai?Ninavyojuwa mimi,hata hao waliokuwa wakimiliki watumwa,walikuwa wakitumia dini ku justify hilo.

Pia hapo chini naomba kupishana na wewe,aliyosema huyo mwandishi ni hisia zake?Kwamba Lincolin hakusimamia abolition on moral grounds?Kuna ushahidi gani kuwa aliamini they where no equals na wakati dhana yake iliyowaingiza kwenye civil war ambayo ilikuwa very destructive ni hiyo imani kuwa "all men are created equal"?Nakubaliana na sababu za kisiasa na pia kulinda muungano wa marekani kuwa mojawapo ya manufaa ya slavery abolition na sababu za Lincolin kuja na ile "Emanicipation Proclamation",however hilo la kiuchumi unaweza kunieleza ni kivipi abolition ilitekelezwa ili kusaidia uchumi?Maana kiukweli,waliingia kwenye civil war(zaidi ya watu 650,000 walipoteza maisha yao kwenye vita hivyo), kwasababu watu wa South walikuwa wananufaika kiuchumi na utumwa,si watu wa South peke yake,bali mfumo mzima wa dunia ulikuwa ukinufaika na utumwa kiuchumi.Karl Max aliwahi kusema hayo hapo chini...

Mimi nadhani ili tuwe na mjadala mzuri zaidi juu ya suala zima la utumwa in the context of social reproduction, tujadili:

Je, The Overriding Reason for the Abolition of Slavery was Economic or Non - Economic?
 
Kwenye blue mimi naamini watu wengi huwa hawapendi kubadili kile walichokizoea hata kama kinawadhuru. Angalia Mexico ambapo watu zaidi ya 40,000 wameuawa kwa kuwa tu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Felipe Calder'on' alianzisha vita dhidi ya wauza madawa ya kulevya na makundi yao. Wamexico wengi walikuwa wamezoea kuishi maisha ya kinyana chini ya magenge ya wauza madawa ya kulevya. Mwisho wa siku Calder'on' akashindwa na Enrique Mena Nieto ambaye alipoingia tu madarakani akasema yeye ataepusha watu wengi kuuawa kwa kuzuia makundi ya ndani ya nchi yasisambaze madawa Mexico na siyo kuzuia makundi hayo kupeleka madawa hayo kwenye nchi nyingine!!

Na kisa kingine ni cha yule muuza madawa ya kulevya wa Jamaica Christopher "Dudus" Coke ambaye wananchi walikuwa wakizuia asikamatwe kwa kuwa tu alikuwa anawapa "huduma za kijamii" kama vile maji na madawa Hospitalini. Mfumo hata ukiwa mbovu kiasi gani ni lazima waathirika wa mfumo huo wafikiri kichanya (Positive thinking) kwa kutenda matendo chanya kwa lengo la kupata matokeo chanya!!

Nakubaliana na wewe na nimependa mtazamo wako huu; kwa kuongezea tu, kada zote katika jamii - maskini kwa matajiri, huwa na maslahi inayoyatazama,na hutaka mabadiliko pale tu wanapoona maslahi yao yapo katika hatari; umaskini ni suala secondary katika kutafuta mabadiliko, kilicho primary ni maslahi individually, na UMMA unatumika tu kama daraja kwa mwendo wa Umoja ni nguvu, lakini umoja huo ukishafanikiwa, tunarudi kwenye ubinafsi wetu; ndio maana ni kawaida kwa watu wengi ambao wakifanikiwa kuondokana na umaskini, wanasahau hali zao za awali, na mara nyingine huwatemea hata mate maskini wakiwasogelea karibu yao;

Kwangu mimi napata shida sana ninapomuona mtu anabomoa daraja na kuuza vyuma vya daraja hilo kama chuma chakavu, lakini hapo hapo kuna watu wengine wanamtetea mtu huyo kuiba vyuma hivyo kwa hoja kwamba ana "haki" ya kuiba kwa kuwa tu walioko madarakani hawajamtafutia mtu huyo kazi ya kufanya!!

Ni kweli, lakini kingine cha ajabu ni kwamba - mtu yule ana ufahamu kabisa kwamba daraja lile lipo kwa ajili ya kurahisisha maisha ya watu - KIJUMUIYA, na limetokana na kodi za wananchi, lakini huyo huyo yakitokea maandamano kwamba serikali haitumii kodi ipasavyo, anakuwa mstari wa mbele; ndio maana nadhani watu wengine wanapo jenga hoja kwamba watanzania wanahitaji mapinduzi ya fikra kwanza kabla ya kitu kingine chochote, wana hoja ya msingi;

Kwenye Red ndugu yangu si tu ni imani yangu bali pia ni Historia inaonyesha kwamba Mapinduzi yote hutokea pale watu wa mashambani wanapoasi dhidi ya mfumo ulliopo na kuamua kuchukua mamlaka ya kuongoza mageuzi kwani Mapinduzi maana yake ni Mabadiliko kamili ya mfumo.

Ni kweli, lakini unadhani mapinduzi yanaweza kukamilika bila kada ya wakulima, wamachinga na wafanyakazi kuungana?
 
Mchambuzi,

Asante kwa mawazo yako; ambayo uko sahihi kwa maana fulani ila tu nikurudishe kwenye context yangu ili tuwe pamoja zaidi!

Kuna definition nyingi za neno "Revolution" lakini mimi kwenye context yangu nilikuwa namaanisha hii hapa!

"Revolution: an
overthrow or repudiation and the thorough replacement of an established government or political system by the people governed.
"

Definition hii inakubaliana na maneno ya Mgalama "Mapinduzi maana yake ni Mabadiliko kamili ya mfumo", Revolution ni mabadiliko kamili ya mfumo.

Wanatoa mapovu leo hii; wanaonyesha wazi kwamba hawatabadili mfumo wote! In reality narudia hata wenyewe wengine hawajui wanachosema, wafuatilie Bungeni ambapo wamekuwa na uhuru kusema kila kila kitu they never real talk about overwhole of our systems and how... bali wanasema improve (huisha) sheria, mikataba etc.
 
Kwa kweli mfumo umedhihirisha uchovu wake watu tunaowaita viongozi wamepoteza dira
na kuwa watawala hawatuongozi tena badala yake wamekua wanaendeleza undugu, kujuana
na rushwa pamoja na matumizi mabaya ya dola na nk.hivi vyote vinaonesha kwamba
nyoka amekua na anatakiwa kujivua
 
kwa kweli mfumo umedhihirisha uchovu wake watu tunaowaita viongozi wamepoteza dira
na kuwa watawala hawatuongozi tena badala yake wamekua wanaendeleza undugu, kujuana
na rushwa pamoja na matumizi mabaya ya dola na nk.hivi vyote vinaonesha kwamba
nyoka amekua na anatakiwa kujivua
nimefuatilia mjadala huu tokea mwanzo nimeupenda
 
am sure na nakubaliana na wachangiaji wengi hapa jamvini kwamba watz wamechoka, lakini pia naamini kwamba si wote wanaoitikia kiitikio cha M4C wanaelewa maana yake, wengine ni just mob psychology inawapelekwa huko kwa walichokiaminishwa kwamba cc.m haina mwelekeo tena, but swali moja hawajajiuliza ni kwamba kama cc.m imekosa mwelekeo basi huo mwelekeo unapatikana wapi? Am not sure kama mwelekeo umekosekana cc.m basi outomatically utapatikana pale cdm. I beg to differ, kwamba cdm wao waongeze tu majimbo ya uwakilishi ili kuongeza usimamizi wa serikali ila kwa sasa bado sioni kama wanaweza kushika usukani wa hiki chombo cha nchi na tukapata mwelekeo tunaoukosa kwa cc.m. Ni maoni yangu tu, just mtazamo.
 
Katika Afrika ni mapinduzi mangapi yamefanyika? Ni vyama vingapi vimetolewa madarakani? na walioingia hawakuleta mapinduzi yeyote kwasababu nia yao ilikuwa tu kuingia madarakani na sio kuleta mabadiliko kwa watu na kwa Taifa kwa Ujumla? Bila program makini wataenda kufanya nini Ikulu? Tuache uchama tujadili ''ideas''
Ndugu Shayu, wachangiaji watakupa majina mengi kutokana na mada yako.
M4C lengo lao ni kukamata dola pasipo kuwa na mipango thabiti. Ni sawa na watoto nyumbani waliokinaishwa na nyama ya kuku watamuomba mama awapikie dagaa na kusema" ma kuku kila siku".
Jiji la Mza ilikuwa ndio angalizo la kwanza kuona uwezo wa CDM ktk kushika dola.Walikamata council ya mza city- Meya.
Baada ya miaka takribani 2 na ushee dola ya Mwanza imewasahinda wamefukuzana, na hatimaye CCM wamekomboa tena himaya yao.
Maana yake kubwa ni nn? Mbio za kukamata dola bila maandalizi na mwishowe DIRA INAKOSEKANA. Nakumbuka kauli ya DR Slaa" JIJI LA MZA ITAKUWA DIRA YETU YA UONGOZI ULIOTUKUKA"
NENDENI IKULU LAKINI TAFADHALI JIPANGENI.
 
... but swali moja hawajajiuliza ni kwamba kama cc.m imekosa mwelekeo basi huo mwelekeo unapatikana wapi? Am not sure kama mwelekeo umekosekana cc.m basi outomatically utapatikana pale cdm.

Hii ni hoja ya msingi sana na ni muhimu kwa Chadema kujipanga kama tulivyokwisha jadili elsewhere - mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu na uuzwe kwa umakini kwa uma, vinginevyo umma utaelekea 2015 with wrong expectations na iwapo CDM itashinda, hizi wrong expectations zitakigharimu Chadema in 2020 if not before;

...Cdm wao waongeze tu majimbo ya uwakilishi ili kuongeza usimamizi wa serikali ila kwa sasa bado sioni kama wanaweza kushika usukani wa hiki chombo cha nchi na tukapata mwelekeo tunaoukosa kwa cc.m. Ni maoni yangu tu, just mtazamo.

Mwelekeo wa sasa chini ya CCM ni kuendesha serikali kwa mfumo wa soko huria na ubepari kwa kutekeleza mageuzi makuu manne kama nilivyoyajadili kwenye Post Number Moja; kwahiyo upo sahihi kwamba CDM hawataenda kufanya mambo yoyote tofauti, zaidi ya kusimamia vyema na kwa ufanisi zaidi mageuzi yanayoletwa kwetu na wahisani, kupitia World Bank na IMF; Ufanisi mzuri zaidi katika utekelezaji wa mageuzi haya definitely uta make a difference kwa maisha ya watanzania, lakini hasa iwapo Chadema itafanya mambo makuu mawili: Kwanza to reorient itikadi yao ili ipate meno kidogo ya kukemea soko huria na ubepari pale unapogeuka kuwa gharama au mzigo kwa maskini; na pili ni suala nilo jadili awali - umuhimu wa chadema kuuzia umma mkakati wake wa muda mfupi, kati, na muda mrefu ili kuepuka umma kukiingiza cdm ikulu with over expectations, only kuigeuka tena Chadema in 2020, if not before;
 
Mchambuzi mimi naamini mapinduzi ya kweli yataletwa na kada za watu wa chini kuungana. Tatizo langu ni kama kipo kiunganishi cha kuziunganisha kada hizo. Mimi bado sijakiona!!
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi: Nimetumia muda wa dakika kadhaa kupitia uchambuzi wako ambao pia umejikita katika utafiti (ambao unaonesha marejeo "Reference" hafifu kitaaluma). Kwa uchache nataka kusema kuwa sehemu kubwa ya uchambuzi wako umejikita katika kuwatia hofu wafuasi wa M4C kwa kutaka kuwaaminisha kuwa kile wanachokishabikia aidha hawakijui kabisa au wale viongozi wao wanawatumia wafuasi wao huku wakiwa na lengo tofauti lililo nyuma ya pazia kwa maana ya “Mass Movements for Revolutions not for Reforms ". Kitu ambacho binafsi sikubaliani nacho!
Hivyo basi kwa kuwa sitataka kujadili hadidu zako zote, kwangu naomba nijibu kwa ufupi tu sehemu ya Nne ya uchambuzi wako.

SEHEMU YA NNE INASEMA: UFUNGUZI WA MDAHALO;

"Baada ya kuweka mdahalo huu katika Muktadha Sahihi (Right Context) na Kujaribu kujenga Hadidu Rejea (terms of reference), yafuatayo ni masuala muhimu ya kujadili

KWANZA, Je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya
MAGEUZI NA MAPINDUZI?

Jibu: Kwanza kabisa naomba nikujulishe kuwa asilimia kubwa ya wale wanataka na kushabikia M4C ni vijana moto na wenye upeo mkubwa katika uwanja wa siasa na si ajabu umekaa nao darasa moja au ni walimu wako….. (Tzm: Maprofesa na wengineo)

PILI, Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?
Jibu: Kiu wanayo! Ndiyo maana nilieleza hapo juu kuwa yawezekana unachokiandika, aidha unakijua kwa kuwa unakiona uhalisia wake au unajaribu kupima ni kiwango gani cha uelewa walichonacho wale wanaotaka mabadiliko ya utawala na wala si MAPINDUZI kama wewe unavyotaka kuwaaminisha. Kwa ujumla wake watu wanahitaji kupata mikakati mbadala na sura tofauti hasa ikiwa na ile tabia ya kuendesha nchi kama kampuni ya kifamilia.
Lakini kubwa katika hali ya sasa nchi zote zenye maendeleo ni zile zenye utawala wa zaidi ya chama kimoja; anza na Marekani, Uingereza, Ujerumani,Uholanzi Japani Russia na kweingineko….!

TATU, Je: Viongozi wanaoendesha “Mass Movements” wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi “Mass Movements” wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi?

Jibu: Ili kuonesha kuwa CCM sasa hivi inafanya kazi kama chama cha upinzani; kwanza ni hali yake ya kufanya kazi zake kwa kutekeleza matakwa ya Chadema, mpaka hapo utaona kuwa tayari chadema ipo madarakani hivyo kilichobaki ni kuthibitishwa kwa wananchi tu. Jambo la pili ni lile la IMF na WB kuiburuza nchi kana kwamba haina watawala wenye fikra ya kusema hiki ni sawa au la! Kama hivyo mbona kuna mambo ambayo nyerere alikuwa akiwakatalia?!! Utaifa kwanza.

NNE, Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
Jibu: CCM imekuwepo madarakani kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitano sasa! Kama imeshindwa kwenda mbele kwa kipindi chote hicho na badala yake inarudi nyuma kwa kasi ya ajabu! Je, leo itaweza kufanya Reforms ndani ya miaka hii miwili iliyosalia? CCM imebaki ikifanana na baba mlevi ambaye pindi arudipo nyumbani watoto hukimbilia kukaa jikoni na mama yao badala ya kumshangilia na kumkumbatia. Hivyo hata mtoto akikuta amelala sebuleni hatamuamsha. Jipange upya kwani watu wanajua wanchokitaka.
ANGALIZO: kinachoonekana kwa sasa CCM ndiyo inayojiandaa kufanya Mass Revolutions pindi wakishindwa kutokana na jinsi kinavyotumia nguvu nyingi katika kudhibiti wanamageuzi.

Nawasilisha jamvini.

Big up nimekukubali mkuu kwa majibu sahihi sina cha kuongeza hapo
 
Mchambuzi mimi naamini mapinduzi ya kweli yataletwa na kada za watu wa chini kuungana. Tatizo langu ni kama kipo kiunganishi cha kuziunganisha kada hizo. Mimi bado sijakiona!!

Kwa mtazamo wa wengi, kiunganishi hicho ni M4C;
 
Back
Top Bottom