Kasheshe,
Nashukuru kwa mchango wako mzuri wenye kuamsha akili; Kimsingi nakubaliana na wewe lakini mimi mtazamo wangu katika hili kidogo ni tofauti na wa kwako na nitajaribu kujieleza.
Dhana hizi mbili:
EVOLUTION &
REVOLUTION zinafanana – ni watoto wa tumbo la mama mmoja; vile vile matumizi yake complement each other, na muhimu zaidi,
these two concepts are not antagonist to each other; Kwa upande mmoja, katika mazingira ya mjadala wetu au tukitazama dhana ya EVOLUTION kijamii na kisiasa zaidi, maana ya evolution ni gradual and continuous development of ideas and morals (e.g. what is right and what is wrong in the society); Kwa upande mwingine kama tulivyokwisho ona, REVOLUTION ni sudden change ya mfumo; Ni kutokana na character hii ya SUDDEN or ABRUPT Change, ndio maana the term REVOLUTION becomes Very Fearful kwa watu fulani fulani, hasa wale wasioelewa au wale waelewa lakini wanao amini katika Status Quo;
Iwapo kuna tofauti baina ya baina ya dhana hizi mbili - EVOLUTION & REVOLUTION, basi ni katika "TIMING"; naomba nirejee mara moja kwenye maelezo yangu ya awali juu ya dhana ya mapinduzi. Nilisema hivi:
… mapinduzi ni mabadiliko makubwa katika mpangilio na uendeshaji wa maisha ndani ya jamii husika. Mara nyingi mapinduzi hupelekea mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa mahusiano ya jamii, kisiasa, kiuchumi, na mara nyingine kiutamaduni. Mapinduzi hutofautiana kwa:
- Mbinu;
- Muda/Duration kufanikisha mapinduzi; na
- Msukumo/hamasa, mfano kiitikadi n.k;
Ebu tutazame haya masuala matatu kwa undani kidogo Mbinu, Muda, na Msukumo; Kama tunakubaliana kwamba EVOLUTION involves Gradual and Continuous development of morals and ideas, then, Mapinduzi ni Suala tu la
"MUDA"; Kwa maana nyingine rahisi, overtime, the gradual and continuous development of ideas vichwani mwa watu in reflection to what is happening to them socially, economically and politically, ndio upelekea UMMA kutaka mabadiliko, na hata ikiwezekana, kwa "
MBINU" MAPINDUZI; Vile vile,
"MSUKUMO" au
"HAMASA" towards change, mfano kwa MBINU ya Mapinduzi,
EVOLVES over
TIME;
Mimi nadhani, kama wapo watu wenye Uwoga wanaposikia neno "REVOLUTION", basi aidha ni kwa sababu hawaelewi maana halisi ya neno hili au ni wanafiki; Kwa mfano unaweza kuta wanasiasa/viongozi kutwa wanahubiri umuhimu wa mabadiliko ili kuletea wananchi maisha bora, lakini hapo hapo, viongozi hawa wanajisikia uchungu sana iwapo mabadiliko hayo yanaenda kinyume na kile wanachotaka, hata kama mabadiliko hayo ni ya GHAFLA na yana manufaa kwa wananchi walio wengi; Iwapo change ni kwa manufaa ya umma, na viongozi hawa kutwa wanahimiza umuhimu wa change kuboresha maisha ya UMMA, inakuwaje wanakuwa na tatizo iwapo mabadiliko haya yanatokea Suddenly (revolution) lakini hawana tatizo mabadiliko haya kuja Gradually (Evolution)?
Huu ni unafiki - kwa sababu – viongozi hawa wanaona kabisa hali mbaya za wananchi na wanakubali kwamba mabadiliko yanahitajika lakini bado wanapendelea to preserve hali ile ibakie kama ilivyo, unless ibadilike kwa matakwa yao; Kwanini? Kwa sababu, hali zile mbaya za wananchi zinawapa wakubwa hawa comfort, wealth and power. Lakini viongozi hawa wanajisahau kwamba, gradually and continuously, ideas are building up/evolving ndani ya vichwa vya UMMA, na baada ya muda fulani, Evolution of the MIND Will turn into Revolution by the MASS;
Vinginevyo, nadhani viongozi wa CCM wanapenda maisha ya wananchi yabadilike for the better,
LAKINI as long the Viongozi KEEP THE TIME, while UMMA KEEP THE CLOCK.