Uchaguzi 2020 MDAHALO: Mtoto amelilia wembe, CCM mpeni

Uchaguzi 2020 MDAHALO: Mtoto amelilia wembe, CCM mpeni

moshdar

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
2,418
Reaction score
1,223
Wana-CCM dawa ya Lissu ni moja tu, Mtoto akililia wembe mpe; chambeche Wahenga.

Huyu Lissu analilia mdahalo na mtukufu Rais, asizubaishwe. Kwa kuwa mdahalo ni kipimo bora cha wagombea na kwa kuwa mdahalo utaonesha kiwango na ubora wa maono waliyonayo wagombea kupitia sera watakazozielezea na kufafanua.

Kwa kuwa Mtukufu Rais amekuwa katika utekelezaji wa mipango mikubwa na dhabiti na kwa kuwa anao uwezo mkubwa na maono mapana unaodhirishwa na kiwango kikubwa cha elimu yake ya Phd anayoimiliki na ambayo huyo Lissu hata haifikii; kumbe basi dawa yake huyu Lissu ni kumkutanisha kwenye mdahalo wa wazi ili mropokaji Lissu anyooshwe hadharani kupitia "arguments" za uhakika za Mtukufu Rais na hapo ndipo Watanzania na ulimwengu utakapoona kwa uwazi kabisa uwezo mkubwa wa Mtukufu Rais na ukilaza wa huyo Lissu.

Wahenga walonga kuwa mtoto akililia wembe mpe; Jamani CCM sasa mtoto Lissu kalilia wembe huyu asizubaishwe, apewe umkate. Hivi huyu ana uwezo gani wa kupanga hoja mbela ya PhD?
 
[emoji23]wewe unataka kazi yako iishie leo?? Magu akitokea au hata kusema tu anaenda kwenye mdahalo basi kura yangu ntampa!!, Maana najua ubatizo atakaoupata sio wakawaida.
Hata mimi kama Jiwe akikubali mdahalo na Lissu ntampatia kura yangu. Jamani mwiteni Jiwe huku aje kuongeza kura japo sidhani kama anaweza kuja hata kwa utani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
HATUNA HAJA YA KUMPA MDAHALO NYOMI ZA MAJUKWAANI NI ZAIDI YA MDAHALO
WATANZANIA BADO WANA IMANI KUBWA SANA NA MATUMAINI NDANI YA CCM
1600701156156.png
 
Hiyo Phd FAKE ya kuokotwa jalalani!? [emoji15]
Hakuna bwana! Alisema yule RPC aliyekufa juzi "Magu ni mwanasayansi hodari duniani hadi korona imemkimbia" [emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa kweli huyu jinsi alivyo genius Lissu atamuweza kweli?

Nawashauri CCM wamuingize ulingoni akatetee taji lake dhidi ya Lissu ili amchakaze kwa point za kiPhd hadi Lissu aombe maji.
Jee mdahalo uwe lini maana Magufuli yuko tayari!
 
Mkuu hivi unajua siri kuu ya kiongozi kutokwenda nchi za nje na kutafuta kila aina ya kisingizio ili kukwepa jambo hilo? Kwa taarifa yako ni ili kukwepa midahalo ama kukutana na maswali ya wanahabari huru wenye iweledi mkubwa na kiu ya kudodosa ukweli wa mambo, na hata kuuliza maswali yenye kuchochea majibu ya kina ili kupima uelewa wa kiongozi juu ya mambo muhimu ya kimataifa.

Sasa hapo katika suala la mdahalo, hivi ni kweli mtu anaulilia wembe ama mtu atapelekwa kwa shingo upande ili aweze kukatwa na kiwembe.
 
PhD iogope mdahalo sijawahi ona kitu kama hichoo
... PhD hutetewa mbele ya jopo la maprofesa wakiongoza hadhara ya kisomi na hutetewa kwa lugha ya kisomi mbele ya wasomi wanaojua kutafsiri hadi nukta na semi-colons na kuhoji maswali fikirishi tena magumu. Ni ajabu sana PhD ikimbie mdahalo wa kisiasa tena hoja zisizo na "format" yoyote. Ajabu sana.
 
Yani MaCCM nikama wana wagombea wawili wa uraisi kwenye chama chao

Kuna mmoja ana sema maendeleo hayana chama kuwa yeye ni raisi wa woote! na kuna mwingine anasema mkichagua upinzani sahauni, maendeleo hatuleti kama vile MaCCM pekee yao ndio yana lipa kodi.
 
Back
Top Bottom