Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Wazee mmesikia hiyo, eti maeneo mengi ya kanda ya ziwa umeme umekatika. Tunawaomba sana tena sana Mzee Mengi na timu yake waturushie mahijiano hayo recorded ili watanzania wengi wamwone rais wao mtarajiwa. Kama ni gharama ya kurusha inaweza kuendeshwa harambee ili kipindi kirushwe mara nyingi na kutoa fursa kwa watanzania kuelewa sera za rais wetu mpendwa wa tano. Mnaonaje jamani?
 
Kuhusu katiba,
Mchakato unaanza ndani ya siku 100, inawezekana kabisa na watu waelewe hivyo, amesema kinana aelewe vizuri hilo!
Anasema wadau wote wanahusika kutengeneza katiba ya nchi yao, watu wote, viongozi wote kutoka chini mpaka juu
Anaongelea bilioni 21 za Kikwete, anasema pesa hizo si za kikwete ni za serikali

Kuhusu wafanya biashara na Siasa.
Si kwamba mfanya biashara asifanye siasa, ukiamua unaingia kwenye siasa, unaingia ila unaepuka conflict of interest. (kuna utaratibu wake ameusema)
Anasema CCM walianzisha bila kujipanga vizuri jinsi ya kufanya swala hilo, ndio maana maji yaliwafika shingoni wakashindwa kutekeleza, Chadema italifanyia kwazi kwa kufata misingi ya kidomokrasia

Swala la mishahara ya wafanyakazi,
Liko wazi kwenye Ilani ya chadema
Wataanzisha utaratibu mpya wa mishahara, watakuwa sensitive na mfumuko wa bei. Imefika mahali watu wanashindwa kulipia mlo wa siku, serikali inasema itakwenda kuwapiga virungu.
Imefika mahali walimu wanatengeneza maandazi, wanawapa watoto wauze, utaratibu huu unasababisha rushwa
Lazima serikali ihakikishe inflation inaondoka na haiwaathiri wafanyakazi, Chadema imefanya utafiti wa kisayansi, kuna watu wanafanya kazi lakini hawafaidiki chochote na mishahara yao.
Ameongelea wazee, watapewa protection scheme ambayo itawasaidia
Swala la Africa mashariki, Swala sio kujitoa,
Chadema inaimarisha Elimu ili watanzania waweze kushindana vyema.

Kuhusu kushinda au kushinda.
Mpira ni Dakika 90, ila ikifika kabla ya dakika tisini refa anasema leo mpira ni sare, there must be a question mark? Why????
Japo mashindano ni kushinda au kushindwa, ikiwa referee ametangazaa matoke kabla ya dakika tisini je tukubali tu kushinda, Makofi kwa wingi saaaana
Mchezo ukichezwa kwa msingi na kanuni za michezo watakubali, ila goli likifungwa kwa mkono huo ni upuuzi na hauwezi kukubaliwa.

More answers coming please…..
 
Kiravu unaona???? we wachokoze tu akina Slaa
 
Wazee mmesikia hiyo, eti maeneo mengi ya kanda ya ziwa umeme umekatika. Tunawaomba sana tena sana Mzee Mengi na timu yake waturushie mahijiano hayo recorded ili watanzania wengi wamwone rais wao mtarajiwa. Kama ni gharama ya kurusha inaweza kuendeshwa harambee ili kipindi kirushwe mara nyingi na kutoa fursa kwa watanzania kuelewa sera za rais wetu mpendwa wa tano. Mnaonaje jamani?

Wanajiabisha tu, magazeti yataandika, si utani kama vipi michango impitishwe kulipia matangazo kwa wiki hii yote!!!!
 
Wazee mmesikia hiyo, eti maeneo mengi ya kanda ya ziwa umeme umekatika. Tunawaomba sana tena sana Mzee Mengi na timu yake waturushie mahijiano hayo recorded ili watanzania wengi wamwone rais wao mtarajiwa. Kama ni gharama ya kurusha inaweza kuendeshwa harambee ili kipindi kirushwe mara nyingi na kutoa fursa kwa watanzania kuelewa sera za rais wetu mpendwa wa tano. Mnaonaje jamani?
Du kumbe ni kanda zima. Wanahofia maana wapiga kura wengi wapo kanda hiyo.
 
tupo zaidi ya hapo......chonde chonde wananchi tukimpoteza rais Slaa tumekwisha

hahah kwanza mkwere akipita wafanyakazi tuna hali ngumu..go......go Slaa pamoja na mambo mengi Sekta ya madini itabidi iangaliwe upya
 
mhhh hapa kwenye mambo ya kuiba kura ..huyu mzee kaongea kwa ufasaha sana
 
Anaongelea Tatizo la tume kutangaza kuwa wamenunua machine za kuchapa makaratasi ya kura, na kasha baadaye kutangaza kuwa karatasi zimekuja kutoka Uingereza, anasema Kiravu asiwachezee watanzania, watu wanauelewa na asijibu kwa staili za miaka ya nyuma.
Anaongelea issue ya Kontena la kura za kufoji zilizosemekana ziko Tunduma, anasema kuwa inawezekana ni kweli, nab ado wanalifuatilia.
Anatoa mfano jinsi kura zilivyoibiwa wakati wa uchaguzi kwenye jimbo lake la karatu, anasema mahakama ilidhibitisha jinsi kura zilivyoibiwa na wala si siri. Kwa hiyo anawaasa watanzania walinde kura zao.

Vigezo vya umaskini. Anasema vigezo vipo vya kimataifa, na hivyo ndio vinavyotumika kuzipima nchi zote,
Kuhusu raslimali, Anasema hili ameshaliongelea kule awali.
 
Maswali yanaendelea, swali kutoka kwa mwanachama mfu wa CCM dokta Lweitama.
 
dr lwaitama kajiita mwanachama mfu wa CCM, MI KANIMALIZA KWA KICHEKO
 
Natamani waongeze masaa mengine zaidi tuendelee kupata ufafanuzi wa mambo muhimu
 
Inatia raha eeeehh, MUNGU ametuona mwaka huu, SIO mwaka wa shetani tena heeheeheeeeee, mbavu zangu mie jamaa leo ataomba apewe ugali kwa mlenda!!!!!
 
Back
Top Bottom