Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Well, Kuzungumza sio kuongoza... kuongoza ni zaidi ya kuwa na nia... kama kuna mtu alikuwa na nia nzuri huku duniani alikuwa JK 2005... but you all know....

Kuna mengi sana ameyajibu vizuri kama debate lakini practically mmhhh... only people who know how to lead will understand... otherwise washabiki wa JK in 2005 they have just got another one to shabikia...

Huyu Dr wa ukweli Slaa ana mifano ya mafanikio ya uongozi katika jimbo la Karatu; na pia kama mwenyekiti wa kamati mojawapo ya bunge.

Vote for Slaa!
 
ASANTE gq NA mm! Tupo Ughaibuni lakini tunamsikia

Nimeamua kulipia paundi 5.5 kwa paypal tv4africa.com nimsikilize slaa.Hakika nimejipongeza kwa kufanya hili.Huyu jamaa ni another level.He's on another planet of thought.A real Tanzanian.I will mobilize every human being I know in Tanzania who can vote,to go and vote him in.This is a life time opportunity,a Messiah whatever you can call it.
Come on Tanzanians,can't we see?Can't we hear?This man is visionary.
Ni mara yangu ya kwanza kumsikiliza Dr. Slaa akiongea kwa zaidi ya saa nzima.Nimetaka kulia kwa jinsi Dr. Anavyoshusha facts,na hizi facts zinatia hasira si utani.Niliwahi kumsikliza kikwete ana kwa ana,I felt so pity for my beloved country,but I had nothing I could do at that time because everything was sweeping on his way....Let's do us proud,let's change the course of our nation,let's mobilize voters,let's head to the poles!
 
Amanifurahisha sana, pale alipojibu kuhusu kukubali au kukataa matokeo, kwamba HATUTAKUBALI IKIWA JK ATAFUNGA GOLI KWA MKONO, NA REFA ATAKAA KIMYA!!! Kweli filosofia tamu sana.
hALAFU NILIVYOKUWA NIKIMWONA DAKTARI, YAANI PALE ALIKUWA ANA'ENJOY' SANA KUJIBU MASWALI, yaani ilikuwa kama vile ni mteremko. Sipati PICHA wangemleta yule jamaa mwingine, leo hii wakakaa pamoja, nadhani ingeshakuja hapa mada kuhusu AFYA yake, (angedondoka chali pale kwenye zulia :A S 39::A S 39::A S 39🙂
 
Katika maswali yote nilihisi lile la mgombea mwenza lingemtia kigugumizi, ila nilishangaa kwa namna Dr. alivyolijibu kwa ustadi mkubwa. It was hot for real, natamani this time ndio mdahalo ungekua unaanza. For real he deserve to be the 5th president of URT. Nina mdogo wangu kajiandikisha kupiga kura mbeya, I had no plan for him na kila siku alikua analalamika kwamba yeye peke yake hatakua sehemu ya mabadiliko kwa kutopiga kura! Leo after Dr's debate kanijia juu anataka nauli aende tena anataka akaconvice na wenzie wa kule wampigie Dr. For sure sina hiana, ijumaa anaenda Mbeya for that, What's 60,000/= for an issue tounching a number of people's lives. Go Dr. Slaa gooo
 
ukiona jf wamewacha kupost kupitia you tube huu mdahalo wa slaa ujue slaa ameboronga sana!!!
We si leta? unasubiri nani akuletee? Alafu huyo ni msomi bwana. Sio kama Jakaya...... Aiseeeee
 
Mie nimefurahia jinsi Dokta alivyokuwa anatoa Broad issues kuelezea vision yake.

Ni tofauti na ukimsikiliza Mkwere, yeye anatumia muda wote kudanganyia project ndogondogo ntaleta bomba la maji, ntaleta meli, ntajenga zahanati. Mambo hayo si issues za kampeni ya urais, ni mambo ya bajeti.

Dokta amenikumbusha zile kampeni za akina Obama, na juzijuzi za kina Cameron an Cleg. Tunataka hivyo Mgombea Urais tupe vision yako.

Well done Dokta, umevuna kura nyingi leo!!!

Umesahau alisema ataleta wataalamu wa kulima nyanya toka ISRAEL
 
:frusty😀uhh! Wadau wengi wa jamii forum naona wako nje ya nchi sasa nani atapiga kura?:smash:

You are wrong my friend, wengine tumesharudi TZ kupiga kura, tumerudi strategically, na watu kama sisi ndio tunawafanya serikali/majeshi wafikirie kusogeza mbele tarehe yenyewe ya uchaguzi, ikitokea basi ujue na wao wamefanya hivyo strategically ili kudili na watu tulio-plan strategically!!!!
 
Any update?


Hakika kwa Watanzania waliomsikiliza Dr Slaa leo, nina imani watafanya maamuzi sahihi ya kumchagua. Nimejionea mwenyewe Dr Slaa akiongea live na Watanzania.Jamani huyu ndiye raisi wa ukweli. Anaongea mpaka unavuta hisia,amejibu maswali yote kwa ufasaha zaidi bila kubabaika,unangoja nini ndugu mwenye shahada ya kupiga kura,Watanzania tumuunge mkono Dr wa ukweli na raisi ambaye ni tegemeo la Tanzania ya kesho. Tarehe 31 October 2010,fanya maamuzi sahihi. Lakini pia kura ni zaidi ya shati lako,fanya kazi ya kuilinda kura yako. Namkubali,hata wana CCM wenyewe wanamkubali.Chagua raisi mwenye uchungu na rasilimali za nchi.Huyu ndiye Dr. Slaa.
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA,TANZANIA NA Raisi DR Slaa INAWEZEKANA.
 
Nipo ukumbini hapa DR SLAA na Mbowe wameshaingia Hotelini pamoja na viongozi wengine wa chadema kama Kitila Mkumbo na Mabele Marando maandalizi yanaenda vizuri kwa walinzi kukagua vitu kadhaa vya kiusalama; mafundi wa ITV wakijaribu mitambo yao pamoja na maongezi ya hapa na pale.

Hapo nje kuna T-shirts za Dr Slaa, ilani ya CHADEMA pamoja na vitabu kadhaa vilivyoandikwa na vijana vinavyohusu maisha ya Dr Slaa pamoja na kingine kinachojaribu kumfananisha Dr Slaa na Nyerere kutokana na matukio na matendo

Asante sana kwa updates zote
Nimependezwa sana na mdahal huu kiasi cha kuahirisha kulala mpaka saa kumi na mbili hii asubuhi huku Asia.
Barikiwa tafadhali kwa jambo hili...Upande wa pili na washinde na walegee.
Dr. Slaaa ndiye Daktari wa kweli.
 
Jamaa akiwa anaongea utafikiri NABII, sipati picha star tv na kale kamdahalo kao kakuchakua na KINENA, NYAMBAF ZAO, aibu zimewajaa, mimavi pwaaah!!
 
Nimekubali Slaa is a presidential material has got vision and mission maana urais tunaoonyeshwa na Kikwete ni ujanja ujanja wa kuahidi kuleta walima nyanya toka Israeli kuahidi kununua meli vitu ambavyo vinaweza kufanywa na ofisi ya mipango, urais ni zaidi ya hapo ni uwezo wa kuiongoza hiyo mipango na kuisimamia, big up Slaa.
 
si bure Kikwete kakacha mdahalo manake Slaa ni noma, kwa hayo maswali ya papo kwa papo na points za kummaliza nahisi angetundikiwa drip. Vote kwa real Dokta na si udokta wa Kuzawadiwa, mtu na kidigrii atafanyanye mdahalo na Dokta Slaa??ndo maana kala kona mapema.
 
Dogo ananiambia home Ifakara watu wamelipuka kushangilia utadhani Asoamoah Gyan kasawazisha goli ile siku ya Ghana na Uruguay

Kigogo,
U make me feel like i am in heaven, yaani leo nimefurahi mno Dr Slaa is everything kwa wa tanzania in present time, nimeambiwa kila mahali, Arusha, moshi, Rukwa, mbeya, mtwara, songea, moro, Dom, singida, mwanza, dar, bukoba, manyara, iringa, ......... watu utazanwanashangilia i mkoloni kafukuzwa Tz, like uhuru day, Pipooooooooooooooooz poweeeeeeeeeeeeeeeeeer, sijui siku ya kura itakuwaje, kama hawa watu wote anashangilia hivyo, Mungu bless Dr Slaa, Mungu ibariki Tz na watu wake,
 

Mzozaji,

Umenifaa mno yaani. Asante sana. Leo nitapata usingizi mzuri na wa amani kwa kuwa sina shaka kwamba Mungu amesikia kilio cha Watanzania na kuwaletea mkumbozi Dr Slaa. Octoba 31 nikiamka tu nitakwenda kituoni kupiga kura kumthibitisha Dr. Slaa kuwa rais wa wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakika kuanzia Nov. 1, Tanzania itarudi mikononi mwa wenye nchi, Wakulima na Wafanyakazi.

Sijui badaa ya mdahalo huu wale wenzetu mashabiki wa chama ambacho muda mfupi ujao kitakuwa chama cha upinzani wanajisikiaje? Nadhani wakipita mitaani watakwenda kwa kuficha nyuso zao kwa aibu! Kama ni majasiri wajitokeze na kumleta "mwali" wao naye ajibu maswali kwenye mdahalo kama huu. Naamini akisikia tu kuwa anahitajika kwenye mdahalo atapata kale ka ugonjwa ka kuanguka.
 
Sikubahatika kusikia mahojiano ya Dr.Slaa lakini hata hivyo nina imani kubwa sana naye toka nimsome hapa JF. Na maadam kaweza kuwapa dawa Watanzania wenzangu ambao pengine walikuwa na mashaka naye, tunawaomba jumuikeni nasi hiyo siku ya siku kusherehekea ushindi kwani huu hautakuwa ushindi kwa Chadema bali ushindi wetu sote.

Wapo wengi waliotubeza hapa JF ya kwamba kijiwe hiki hakiwezi kuwafikia Watanzania wengi walioko vijijini. Hakika tumewadhirihishia mchango wetu kwani umetimia na nawashukuru sana waanzilishi wa JF kwani pasipo nyie sisi wengine huku tusingeweza kumsifia Dr.Slaa wala kuweka matumaini kwa chama Chadema kuweza kuweka historia mpya. Maadam Dr.Slaa alikuwa na bado ni mwanachama wa JF ushindi wake utahesabiwa kama ushindi wa JF kwa ujumla - Mungu ashukuriwe!

Ahsante sana Dr.Slaa, rais mtarajiwa umeweza kuwakilisha!
 
Thanks to you all comrades who facilitated this thru updates, radio websites, discussions, and all that made this mdahalo interesting. Senkis za kumwaga kwa Dr. Slaa majibu na maelezo mazuri ya hoja na sera zake. Tanzania needs a visionary leader like you.
Together we can bring changes.
 
Back
Top Bottom