Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014


du kaumbuka
 
Naona kuna watoto wamevalishwa kezi za ccm wako upstairs ya nkurumah
 
Profesa Gaudence Mpangala wa RUCO Iringa ameanza kuzungumza.Anasema mara baada ya wabunge wa UKAWA kutoka nje ya BMK yeye,Prof .PLO Lumumba na Prof. mwingine wa UDSM walifanya utafiti.Utafiti wao ulihusu chanzo cha mkwamo huo na utatuzi wake ni nini?.Waliuliza wadau mbali mbali na wakagundua chanzo ni sababu 5.Sababu hizo ni 1. kutozingatia misingi ya sheria inayoelekeza mchakato wa uundaji wa katiba mpya 2. Kuibeza na kuiponda Tume pamoja na uzinduzi wa BMK kwa rais kuzindua 3.Mazingira ya mjadala yalighubikwa na kubeza na kukashifiana 4.Kutokana na sababu hizo 3 UKAWA walitoka nje 5.Mapungufu ya sheria iliyounda mabadiliko ya katiba ambapo bunge maalum limejaa wanasiasa. Kuhusu UTATUZI amesema vitu vitano 1.Rasimu iliyotokana na wananchi wa Tanzania ndiyo ijadiliwe2.UKAWA warudi bungeni na wajadili rasimu iliyoletwa na Warioba 3.Wabunge wote watakaorejea waweke utaifa mbele na waache kujali vyama na kubezana.TANESCo wamechukua umeme
 

Huu mdahalo utakuwa mzuri kuliko yote iliyowahi kutokea, Jaji Warioba na wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiko ya Katiba mtatueleza Watanzania Ukweli tofauti na Matusi na kejeli za CCM.
 
Hivi hawa Ccm hizo pesa za kukodi Uda si wangetumia kuchimba visima wananchi wapate maji
 
Hivi Wassira anajiskiaje anapoona mzee mwenzie Prof Mpangala anavyoshusha nondo za ukweli na uhakika.

Serikali 3 nikuboresha demokrasia.
 
naona makofi yamepungua baada ya Prof. Mpangala kugonga kichwa

Mkuu lazima yapungue maana ccm kama mnaona kupitia luninga zenu wameleta wanachama wao na gari za UDA ndo wamekaa kwabele.

Pili wamekuja na watoto wao wote ili kujaza nafasi za mbele wale wenye hoja wasipate nafasi kabisa. Lakini Mungu yuko pamoja nasi Prof.Mpangala ndo kamaliza hakika amegusa pale wananchi walio wengi wanapataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…