Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

kama tundu lisu yuko hamna cha maana zaid ya matusi tu

Sawa Mwigulu

Haya ona maccm yanavyobeba watu

attachment.php



attachment.php



attachment.php
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naona hivi sasa umegeuka kuwa mtetezi wa CCM mzuri sana.

Nakumbuka siku si nyingi sana nawe ulikuwa unakosoa utawala huu huu.

Nanukuu posts zako ambazo si za zamani sana.











Nina maswali kidogo kwako.

1. Hivi CCM imebadilika nini hasa ambacho kimekufanya uanze kuona nia njema kwao, nia ambayo mwanzoni hukuiona?

2. Nini kimetokea kwako hata ukabadili msimamo mara moja na kuanza kuwaunga mkono hao uliowaona mwanzo ni wakandamizaji?

3. Ni mabadiliko yako mwenyewe binafsi, au kuna ushawishi wa watu wengine?

Majibu ya maswali haya yatatusaidia hata sisi wengine tunaoona ukandamizaji wa CCM mpaka sasa.

du kaumbuka
 
Naona kuna watoto wamevalishwa kezi za ccm wako upstairs ya nkurumah
 
Profesa Gaudence Mpangala wa RUCO Iringa ameanza kuzungumza.Anasema mara baada ya wabunge wa UKAWA kutoka nje ya BMK yeye,Prof .PLO Lumumba na Prof. mwingine wa UDSM walifanya utafiti.Utafiti wao ulihusu chanzo cha mkwamo huo na utatuzi wake ni nini?.Waliuliza wadau mbali mbali na wakagundua chanzo ni sababu 5.Sababu hizo ni 1. kutozingatia misingi ya sheria inayoelekeza mchakato wa uundaji wa katiba mpya 2. Kuibeza na kuiponda Tume pamoja na uzinduzi wa BMK kwa rais kuzindua 3.Mazingira ya mjadala yalighubikwa na kubeza na kukashifiana 4.Kutokana na sababu hizo 3 UKAWA walitoka nje 5.Mapungufu ya sheria iliyounda mabadiliko ya katiba ambapo bunge maalum limejaa wanasiasa. Kuhusu UTATUZI amesema vitu vitano 1.Rasimu iliyotokana na wananchi wa Tanzania ndiyo ijadiliwe2.UKAWA warudi bungeni na wajadili rasimu iliyoletwa na Warioba 3.Wabunge wote watakaorejea waweke utaifa mbele na waache kujali vyama na kubezana.TANESCo wamechukua umeme
 
Humphrey Polepole
******MDAHALO MDAHALO MDAHALO MDAHALO MDAHALO*******

UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI SASA KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA

SIKU:

JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014 UKUMBI: HOTELI YA BLUE PEARL UBUNGO PLAZA

SAA:

MJADALA UTAANZA SAA 7 MCHANA KWA ELIMU YA MCHAKATO NA RASIMU

NA UTARUSHWA LIVE NA ITV KUTOKA SAA 9 HADI 12 JIONI

WAZUNGUMZAJI WAKUU:

MWENYEKITI WA TUME YA KATIBA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA,

DR. SALIM AHMED SALIM WAZIRI MKUU MSTAAFU

NDUGU JOSEPH BUTIKU- MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE

PAMOJA NA,

MWATUMU MALALE- MTUMISHI WA UMMA MWANDAMIZI MSTAAFU

PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI- SHULE KUU YA SHERIA, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

AWADH ALI SAID- RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR

NA,

HUMPHREY POLEPOLE- KIJANA MDAU WA MAENDELEO

MDAHALO UMEANDALIWA NA:

TAASISI YA MWALIMU NYERERE

USIKOSE KUSHIRIKI KATIKA MDAHALO MUHIMU

Huu mdahalo utakuwa mzuri kuliko yote iliyowahi kutokea, Jaji Warioba na wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiko ya Katiba mtatueleza Watanzania Ukweli tofauti na Matusi na kejeli za CCM.
 
Hivi hawa Ccm hizo pesa za kukodi Uda si wangetumia kuchimba visima wananchi wapate maji
 
Hivi Wassira anajiskiaje anapoona mzee mwenzie Prof Mpangala anavyoshusha nondo za ukweli na uhakika.

Serikali 3 nikuboresha demokrasia.
 
naona makofi yamepungua baada ya Prof. Mpangala kugonga kichwa

Mkuu lazima yapungue maana ccm kama mnaona kupitia luninga zenu wameleta wanachama wao na gari za UDA ndo wamekaa kwabele.

Pili wamekuja na watoto wao wote ili kujaza nafasi za mbele wale wenye hoja wasipate nafasi kabisa. Lakini Mungu yuko pamoja nasi Prof.Mpangala ndo kamaliza hakika amegusa pale wananchi walio wengi wanapataka
 
Back
Top Bottom