Pre GE2025 MDAHALO: Wagombea Uenyekiti wa CHADEMA kuhojiwa na Chief Odemba. Ni tarehe 18.01.2025 Jumamosi

Pre GE2025 MDAHALO: Wagombea Uenyekiti wa CHADEMA kuhojiwa na Chief Odemba. Ni tarehe 18.01.2025 Jumamosi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe atakuwa ni mpuuzi kushiriki mdahalo ambao atakuwa anashambuliwa Mwanzo mwisho
kwani kama anashambuliwa kwa tuhuma au mambo ya kweli hauoni ni afya kwa ustawi wa siasa zetu na taifa?

Tunataka mijadala ya namna hii zaidi na zaidi,sio mambo za mitano tena!
Njoo ueleze umefanya nini na utafanya nini, period!
 
Mbowe na ccm yake hawapendi midahalo kwa sababu hawana hoja
Hapana, mkuu. Sisi hoja zetu ni bora kuliko vijembe na vijimaneno maneno vya majukwaani visivyokuwa na tija. Tunafokasi kwenye maendeleo zaidi.

Nasemaje? Tukutane kwa boksi hiyo tarehe 21 Jan. 2025!
 
Mdahalo unaweza kuwa mchungu kwa Mbowe. Unawaambia ni watu kwanini unataka kuendelea kuwa Mwenyekiti baada ya kukalia kiti kwa miaka 21?

Una jipya gani? Lipi ambalo hujafanya kwa miaka yote na sasa unataka mitano mingine?

Huu Mdahalo zaidi utakwenda kukivua nguo Chama. CCM watarecord mwanzo mwisho na hizo missiles watazi unleash huko mbele mwezi wa tisa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu
 
Kumekucha ila ngoja tuone Miamba hii miwili ya CHADEMA itakavyomenyana mbele ya Wananchi,

Tuendelee kumwomba Mungu ili sote tufike salama 2025.

====
Mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema Taifa utafanyika tarehe 18/01/2025, siku ya jumamosi kuanzia saa 3:30 Usiku hadi saa 6:00 Usiku, mahali mtajulishwa. Mpaka sasa wagombea wawili wamethibitisha kushiriki mdahalo huo, tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wote wanashiriki katika mdahalo, Asante.

=====

View attachment 3186218

Merry Xmas and Happy New year 2025.
Nashauri Mbowe usiende utakuja kunishukuru
 
Yale tukiyaitisha hayawi hayawi yamekuwa:

IMG_20241228_145008.jpg


Bila shaka mwamba atakuwapo kunadi sera zake!

Gfn6YE-XkAATunC.jpeg


Hii ikiwa ni kwa sababu chuma msimamo wake ni wazi:

IMG_20241226_071102.jpg


🔥🔥

Asiyekubali kushindwa si mshindani!

Pia soma: Uchaguzi wenyeviti taifa Chadema, Debates za wazi ziandaliwe kwa wagombea tuzione mbivu na mbichi zao, itapendeza zaidi!

Pia soma: Kuelekea 2025 - Tuzijue "Sera za Mbowe" dhidi ya "Sera za Lissu," uchaguzi mwenyekiti CHADEMA 2025
 
Yale tukiyaitisha hayawi hayawi yamekuwa:

View attachment 3187016

Bila shaka mwamba atakuwapo kunadi sera zake?

View attachment 3187014

Hii ikiwa ni kwa sababu chuma msimamo wake ni wazi:

View attachment 3187018

🔥🔥

Asiyekubali kushindwa si mshindani!

Pia soma: Uchaguzi wenyeviti taifa Chadema, Debates za wazi ziandaliwe kwa wagombea tuzione mbivu na mbichi zao, itapendeza zaidi!

Pia soma: Kuelekea 2025 - Tuzijue "Sera za Mbowe" dhidi ya "Sera za Lissu," uchaguzi mwenyekiti CHADEMA 2025
Tupe nukuu ya majibu ya mwenzake
 
Hata kama ni energy nitakunywa tu ili nisilale hiyo siku.

Mdahalo sio wa kukosa, na hapo ndipo Lissu atakapochukua point zote za ushindi.
Litakuwa somo kwa greens maana midahalo huwa sumu kwao
 
Back
Top Bottom