Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

MAMBO YA KUFUFUA NI IMANI YA DINI.LIVE PIE AS PIE..CHET KINATAKIWA


Kama kufufua n iman ya dini kwa hyo dini ya kikristo n feki imeshindwa kufufua kupitia kwa mchungaji wao gwajima

Je Roman nao hawafufui je wale hawana iman ya dini???
 
Alichozungumza ni sahihi kabisa na mimi namsifu kwa ujasiri alionao, ishu ya vyeti ni suala la yeye na mwajiri wake na kwakuwa nafasi aliyopewa sio ya kupigiwa kura sidhani kama kunahajaya watu kushikia bango kiasi hicho ati aonyeshe vyeti ili kiwe nini? na kwavyovyote vile ingekuwa ya ni nafasi ya kushindaniwa yawezekana asingetia mguu. Hatahivyo shida kubwa watu wameamua kujitoa ufaham kwenye jambo la msingi la madawa ya kulevya kwa sarakasi za gwajima. Yaani watu na elimu zao kila siku wamekalia vyetivyeti mdaini vyeti akigombea ubunge au udiwani hii aliyoteuliwa na Rais atajuana na bosi wake. Tuwe serious jamana watanzania please for the seck of our country
Elimu ni jambo muhimu sana,huwezi ongea hayo kama hauna tatizo la elimu.

Mosi,suala la madawa ya kulevya halishughulikiwi na Makonda,lipo chini ya Tume ya Sianga,na chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu.Makonda hata sio mjumbe wa tume hiya.

Pili,Kutumia cheti cha mtu mwingine ni kosa kisheria na yeyote mwenye akili timamu hawezi kuchukizwa na jambo hili.Kelele hizi ni kudai haki sawa kwa wote kwa mujibu wa sheria.Kuna watu sass wapo jela kwa kosa la kuiba cheti kwanin wengine waachwe?

So haya mambo mawili hayana uhusiano kabisa,ni mtu tu asiyejishughulisha kusoma anayeweza kudhani kuwa eti Makonda ndiye vita dhidi ya madawa ya kulevya.Wrong.
 
Uuuhhh gwajima hajawah kufufua hata panyaaa maneno kuntu hayo......

mchungaji gan ana mipasho kanisa limegeuka eneo la mipasho...nlcheka baada ya kuamuru pepo liende kwa makonda waumin wakashangalia hapo utajua hata waumin wa gwajima n mazombie akil zao mgando ndomana wanadanganywa gwajima anafufua...

baada ya pepo kugoma kumuingia makonda akisema haingiliki waumin kimyaaaa...

ile n fedhea kwa gwajima kadhilishwa na pepo lake
Ukisikiliza vizuri maneno kwenye clip ni ya kupandikizwa!
Hata hivyo hilo hata kama ni kweli halimpi nafuu Bashite kwenye uhalifu wa kutumia cheti cha mwingine!
Daudi wa Bashite weka vyeti mezani!
 
Kashawahi kukufufulia hata ndugu/jamaa yako mmoja?, ama kila siku utamuamini anaweza fufua wakati huo kuhudhuria misiba na msemo "bwana ametwaa"..
Hayo hayatuhusu wanahusika waumini wake. Sisi tunataka vyeti vya huyu anaye lipwa mshahara kwa pesa za kodi zetu.
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.


hatutaki mihadarati na hatutaki vyeti vya kugushi. wacha longolongo mwambie aweke vyeti.
 
Hilo tamko limeandaliwa wapi na nani? Je, hoja ya msingi ya forgery ni kweli au sio kweli? Hayo mengine wala watanzania hawahitaji kuyajua. Nguvu zooote anazotumia hapo si angeweka vyeti mezani akammaliza kabisa Gwajima forever and ever? Vinginevyo, this is another justification ya tuhuma za wizi wa vyeti. Yaani ndio anazidi kummaliza kabisa Bashite! Ha ha ha; kuna watu wapumbavu sijawahi kufikiria.

Unajua watz wengi humu kwenye mitandao wanalalama hata hawajui wanachotaka, ukiwemo wewe! Makonda hajafoji vyeti, vyeti vyake ni halisi na vinatambulika na mamlaka husika!! Sasa wewe hoja yako ni nn????
 
Sidhani kama Kuna mtu mwenye chuki na RC, kweli kafanya mazuri mengi ya kupigiwa mfano,na vile vile kafanya mabaya mengi ya kukemewa, kama kweli katumia cheti ambacho sio chake, sheria ichukue mkondo wake. Afikishwe mahakamani haki itendeke!! Ata kama atafungwa ndo haki yake.
 
Kapewa kidogo huyo sio bure. Ila ngoja tuone koz kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho, na haki huwa haipotei. Transparency ni kitu muhimu sana. Nadhani mtakuwa mmenielewa.
 
Acha kujitoa ufahamu.. Kinachozungumzwa hapa sio utapeli wa Gwajima.. Kilicho mezani ni tuhuma za Mkuu wa Mkoa kutumia vyeti vya elimu ambavyo sio vyake.. Hamna uhusiano hapo hata kidogo.. Na kwa sababu mtukufu alishatangaza vita dhidi ya uhalifu huu, ni budi sie wananchi tushiriki kumsaidia mtukufu, kwa kuwafichua wote ambao wanatumia vyeti vya kughushi au vya watu wengine..
Kwanini ishu ya vyeti ianze baada ya vita vya madawa?

Kama ana ushahidi wa hivyo vyeti kwa nini asiweke mezani watu waone?
 
Ok kama nikweli mdogo wake,tumsubiri Gwajima amjibu! Lakin ninaimani huyu kamtumwa
 
Back
Top Bottom