brasy coco
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 1,489
- 900
MAMBO YA KUFUFUA NI IMANI YA DINI.LIVE PIE AS PIE..CHET KINATAKIWA
Elimu ni jambo muhimu sana,huwezi ongea hayo kama hauna tatizo la elimu.Alichozungumza ni sahihi kabisa na mimi namsifu kwa ujasiri alionao, ishu ya vyeti ni suala la yeye na mwajiri wake na kwakuwa nafasi aliyopewa sio ya kupigiwa kura sidhani kama kunahajaya watu kushikia bango kiasi hicho ati aonyeshe vyeti ili kiwe nini? na kwavyovyote vile ingekuwa ya ni nafasi ya kushindaniwa yawezekana asingetia mguu. Hatahivyo shida kubwa watu wameamua kujitoa ufaham kwenye jambo la msingi la madawa ya kulevya kwa sarakasi za gwajima. Yaani watu na elimu zao kila siku wamekalia vyetivyeti mdaini vyeti akigombea ubunge au udiwani hii aliyoteuliwa na Rais atajuana na bosi wake. Tuwe serious jamana watanzania please for the seck of our country
Sasa mimi hapa huwa siwaelewi. Kama wanauza si wakamatwe? Au kutangaza ndio vita vyenyewe? Na kama huyo Daudi si kolomije kweli, si angeshaonesha vyeti?
Ukisikiliza vizuri maneno kwenye clip ni ya kupandikizwa!Uuuhhh gwajima hajawah kufufua hata panyaaa maneno kuntu hayo......
mchungaji gan ana mipasho kanisa limegeuka eneo la mipasho...nlcheka baada ya kuamuru pepo liende kwa makonda waumin wakashangalia hapo utajua hata waumin wa gwajima n mazombie akil zao mgando ndomana wanadanganywa gwajima anafufua...
baada ya pepo kugoma kumuingia makonda akisema haingiliki waumin kimyaaaa...
ile n fedhea kwa gwajima kadhilishwa na pepo lake
Hayo hayatuhusu wanahusika waumini wake. Sisi tunataka vyeti vya huyu anaye lipwa mshahara kwa pesa za kodi zetu.Kashawahi kukufufulia hata ndugu/jamaa yako mmoja?, ama kila siku utamuamini anaweza fufua wakati huo kuhudhuria misiba na msemo "bwana ametwaa"..
hatutaki mihadarati na hatutaki vyeti vya kugushi. wacha longolongo mwambie aweke vyeti.Kwa ufupi
Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.
Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.
Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.
Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.
Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.
Haa ha ha hahuyu ni "Gwajima rapa "
Hilo tamko limeandaliwa wapi na nani? Je, hoja ya msingi ya forgery ni kweli au sio kweli? Hayo mengine wala watanzania hawahitaji kuyajua. Nguvu zooote anazotumia hapo si angeweka vyeti mezani akammaliza kabisa Gwajima forever and ever? Vinginevyo, this is another justification ya tuhuma za wizi wa vyeti. Yaani ndio anazidi kummaliza kabisa Bashite! Ha ha ha; kuna watu wapumbavu sijawahi kufikiria.
hatutaki mihadarati na hatutaki vyeti vya kugushi. wacha longolongo mwambie aweke vyeti.
Mdogo wake asiyekuwa na jina. Vidudumtu kama hivi askofu waka hajisumbui navyo. Mchungaji yeye anataka vyeti. Baaaashahahaha natamani gwajima ashike kipaza sauti amjibu HUYO MDOGO WAKE
Thibitisha!Unajua watz wengi humu kwenye mitandao wanalalama hata hawajui wanachotaka, ukiwemo wewe! Makonda hajafoji vyeti, vyeti vyake ni halisi na vinatambulika na mamlaka husika!! Sasa wewe hoja yako ni nn????
Kwanini ishu ya vyeti ianze baada ya vita vya madawa?Acha kujitoa ufahamu.. Kinachozungumzwa hapa sio utapeli wa Gwajima.. Kilicho mezani ni tuhuma za Mkuu wa Mkoa kutumia vyeti vya elimu ambavyo sio vyake.. Hamna uhusiano hapo hata kidogo.. Na kwa sababu mtukufu alishatangaza vita dhidi ya uhalifu huu, ni budi sie wananchi tushiriki kumsaidia mtukufu, kwa kuwafichua wote ambao wanatumia vyeti vya kughushi au vya watu wengine..
Bhas sawa kisubirie hicho cheti mkuu.Hayo hayatuhusu wanahusika waumini wake. Sisi tunataka vyeti vya huyu anaye lipwa mshahara kwa pesa za kodi zetu.