Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Naona umeweka namba yako ya simu kabisa mahususi kwa uteuzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bashite.
 
Mchungaji gani anarusha makombora? mchungaji gani anawarushia watu mapepo?
 
Kwani wewe nyani?? Nenda mahakamani...wale wanasheria makamanda watakusaidia.
 
Wanasiasa wenye uwezo wa kifedha hawashindwi kutengeneza sanaa yenye kuaminisha watu kesho sitashangaa Mch. Gwajima akimkana huyu mtu kuwa hamjui na utashangaa mtu hyu naye akiingia mitini. La maana hapa ni Bashite kuweka vyeti mezani ambavyo vina uzito mwepesi hata nusu kilo haifiki
 
Kumuunga mkono Bashite inahitaji kuwa mjinga kweli kweli...
 
Dawa ya kumaliza mng'ang'ane huu ni Bashite kuonyesha vyeti bila hivyo aishie huko Bondeni alipo hatuwezi kuongozwa na mtu mpiga domo lakini kwenye taaluma ni sifuri kabisa
 
Ilitosha kuhukumu huyu mtu siku alipobandika orodha anayodai ya wauza unga alipoandika neno "Petrolium badala ya Petroleum"na hii inamaanisha huyu ni kilaza asiyejua chochote kazi yake ni ujanja mwingi wa mdomoni
 
Hoja ya msingi si forgery mkuu. Hoja ya msingi ni madawa ya kulevya. Msitutoe katika reli.
 

Mkuu una ugomvi binafsi na mchambuzi nn maana wanaodai vyeti ni wengi hata wale wa upande wa pili
 
Mi mpaka sasa bado sijaona hiyo vita ya madawa ya kulevya Bashite anapigana na nani!..
 
We we sio mdogo wake mch Gwajima Ni mnafiki unaeingoja jehanam ya moto kwani kweli kama ni kaka yako usingeongea hayo kwenye hadhara ulishindwa nini kama kweli ni ndg yako kuongea nae faragha we ni mnafiki mbaya sana
Alivyochafuliwa Gwajima na madawa ya kulevya jambo ambalo hata ushahidi haukupatikana uliona ni sawa? We sio ndg yakeee.
 
Jamaa nimesoma naye pia. Sikujua jina lake lingine ni Gwajima.

Ila kuna mtoto mmoja wa kidosi alikuwa karibu naye. Sidhani kama yule binti alipona.
 
Kama gwajima ni WA kuzungumza kwenye media Hata huyo anaruhusiwa usiforce watu wafanane,,,, acha tupate mautamu ya makavu live bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…