Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mimi naona naye anatafuta Kiki, hapo alipo anapata attention kwakuwa ni mdogo wa gwajima.... If it wasn't for his brother, angebaki na vyeti vyake vya IJA mtaani
 
Wasituondoa kwenye hoja ya msingi wajinga hawa, Bashite na vyeti ndio jambo la msingi
 
Tunataka vyeti tu, mengine yooote ni CD tu, wliweka CD ya mama Salma ili tupotezee la fyeti ila bado tumeendelea kung'oja fyeti, sasa na hii CD isha-scratch......... Malipo ni hapa hapa duniani, acha yale matusi ya kuwatukana wenye vyeti vyao orijino imuandame.
 
Kama kweli yeye ni mdogo wa Gwajima bila shaka nae ni mkazi na mzaliwa wa Kolomije, naomba kujua je hilo jina la Daudi Albert Bashite ni la kweli au LAA!?
Exactly that was the question supposed to be asked. Habari za yaachiwe mamlaka, ni mamlaka hipi hiyo na toka hizi kelele zimeanza kupigwa inamaana hiyo mamlaka imelala au bado inatafuta tu?
 
Ha ha ha!! Umenichekesha kweli. Hajawahi kufufua hata panya!!!! Ila hapa vyeti tu!!!! Mpaka kieleweke.
Swala la kufufua atajuana na waumini wake wanaojazana hapo kanisani. Swala la madawa limeshapata aliebobea na ukitaka kujua ana weledi hatujamuona akiuza sura, yuko ofisini anachapa kazi. Sasa suala la cheti limekuwa kindumbwendumbwe kazi ambayo haitachukua hata nusu saa imeanza kusababisha mpaka watu kuanza kupiga hela kama huyo kibaka mwingine anaetumwa kumsafisha mwizi wa taaluma.
 
Me sija ajiriwa na mtu mkuu, Mkuu wa mkoa ni mtumishi wa wananchi kwani kuna ubaya akituonesha vyeti?
Sio mwanasiasa huyo kusema labda kachaguliwa na wananchi. Ni mteuliwa na aliyemteua ndio anapaswa kuona vyeti vyake. Sasa wewe kama ni whistleblower si tayari umeishatoa taarifa???

Kiherehere cha nini mwanaume mzima...tuache kuendekeza ujinga.
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Issue ni vyeti hayo yanayohusu ufufuo na uzima ni Mambo ya kiiman zaidi si wengine hayatuhusu huko.
 
Kusema kweli kazi ya Mhe. Paul Makonda katika vita dhidi ya madawa ya kulevya haiwezi kupuuzwa! Amefanya jambo jema na hakika amejiongezea thawabu kwa kiwango kikubwa. Ameliokoa taifa, na hakika amejitoa mhanga. Lakini ukweli huu hauwezi kufuta tuhuma dhidi ya vyeti vya elimu yake. Ajisafishe kwa hoja na kama ana ushahidi autoe. Hoja itafungwa, haiwezi kufungwa kwa mapungufu ya Mchungaji Gwajima au Mbowe na Wema Sepetu. Kila mmoja awajibike kwa tuhuma iliyo elekezwa kwake.

Haitawezekana askari aliyeua maadui wengi wa Taifa lake asamehewe kosa la kumuua mtoto mdogo wa jirani yake.

Kama kaka yake Mchungaji Gwajima, anazotuhuma nyingine dhidi ya Mchungaji azitoe hadharani na uthibitisho wake. Tuhuma hizo zitashughulikiwa bila kujali anachokieleza kuhusu Mhe. Makonda.
 
Huyo, siyo ndg. Yake.nikama wale ndg, waliomuuza ndg, yao kwa uroho wa pesa.nahuyo ni mganga njaa tu.ccm wafitini mpaka mnafitinisha ndg.
 
Kuna mtu anamjua kasema hivi "boya huyo namjua alikuwa katibu wa CCM Nzega na sio ndugu wa Gwajima, alihamishiwa Singida. Na alikuwa antembea na mke wa mtu anaitwa Mary.......!!!"
 
A mwambie aliemtuma kabugi,hana undugu nae ni kutafuta kiki tu,alikuwa wapi kumtetea tuhuma za unga,km anacho cheti cha Jamaa atuonyeshe.
 
watanzania wa sasa hivi hawatoki nje ya reli,hapa ni BASHITE TU,MAMA ONGEA NA MWANAO AONYESHE VYETI
 
Sisi watz tumechoka na ujinga wenu hoja ya msingi hapa ni.madawa ya kulevya ni siyo ujinga wenu .
Issue ya madawa ya kulevya sasa anayo mwenye weledi,uwezo,nia ya dhati na nyenzo za kuipigana,Mzee Sianga. Ni utahira tu unaofanya mtu afikiri kuwa vita ya madawa ya kulevya inapiganwa kama "team kiba v/s team diamond",kwenye media.
 
Hawa wazaliwa wa Koromije hivi kwanini hawapendani? Yaani hata ndugu wa tumbo moja nao waanza kuchambana hadharani!
Yaelekea hakuna upendo wa kutosha kwa baadhi ya familia za KOROMIJE
 
Back
Top Bottom