Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Angezungumza kwa vitendo,,,, kwa maana ya kuweka vyeti vya bashite mezani... full stop 😵 🙁
 
Huyo anayejiita mdogo wa Gwajima badala ya kuwapotezea watu muda na huo upuuzi aliouongea si angemshauri Daudi Albert Bashite anayejiita Paul Makonda ampe vyeti ili awaonyeshe hao waandishi wa habari halafu habari za kufufua panya au watu, Gwajima na waumini wake watamalizana, wengine hazituhusu!
 
Huwa nasema kila siku upinzani hawajitambui!

Yani mwanafamilia kaja kuthibisha kwamba Gwajima ni tapeli, wewe msukule unaemuona kupitia tv unakuja hapa na porojo zako!

Acha kujitoa ufahamu.. Kinachozungumzwa hapa sio utapeli wa Gwajima.. Kilicho mezani ni tuhuma za Mkuu wa Mkoa kutumia vyeti vya elimu ambavyo sio vyake.. Hamna uhusiano hapo hata kidogo.. Na kwa sababu mtukufu alishatangaza vita dhidi ya uhalifu huu, ni budi sie wananchi tushiriki kumsaidia mtukufu, kwa kuwafichua wote ambao wanatumia vyeti vya kughushi au vya watu wengine..
 
Swala la kufufua atajuana na waumini wake wanaojazana hapo kanisani. Swala la madawa limeshapata aliebobea na ukitaka kujua ana weledi hatujamuona akiuza sura, yuko ofisini anachapa kazi. Sasa suala la cheti limekuwa kindumbwendumbwe kazi ambayo haitachukua hata nusu saa imeanza kusababisha mpaka watu kuanza kupiga hela kama huyo kibaka mwingine anaetumwa kumsafisha mwizi wa taaluma.
Nabii hakubaliki kwao ndiyo imekula kwao sasa. Kwetu sisi tunamkuba. Lete vyeti yote hayo hatuyahitaji.

Hawa wazaliwa wa Koromije hivi kwanini hawapendani? Yaani hata ndugu wa tumbo moja nao waanza kuchambana hadharani!
Yaelekea hakuna upendo wa kutosha kwa baadhi ya familia za KOROMIJE
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Hivi inakuwaje Mpaka unakubali kutumika against ndugu yako?
 
sijui wengi wetu tuna akili za kushikiwa!, ndugu wa makonda kajitokeza mmewaamini waloyasema ila ndugu wa gwajima kujitokeza hamumuamini kazi kumponda!, haya ndo kashasema hajawahi fufua hata panya rubbish!..
Nabii hakubaliki kwao. Imekula kwenu.
 
Nabii hakubaliki kwao. Imekula kwenu.
Kashawahi kukufufulia hata ndugu/jamaa yako mmoja?, ama kila siku utamuamini anaweza fufua wakati huo kuhudhuria misiba na msemo "bwana ametwaa"..
 
Asante sana ndugu wewe ndio askofu wa kweli
Tuwe wakweli hakuna kiumbe aliekamilika
Nguvu nyingi itumikayo kudai vyeti hiyo hiyo nguvu tuitumie kupiga vita bwimbwi
 
Uuuhhh gwajima hajawah kufufua hata panyaaa maneno kuntu hayo......

mchungaji gan ana mipasho kanisa limegeuka eneo la mipasho...nlcheka baada ya kuamuru pepo liende kwa makonda waumin wakashangalia hapo utajua hata waumin wa gwajima n mazombie akil zao mgando ndomana wanadanganywa gwajima anafufua...

baada ya pepo kugoma kumuingia makonda akisema haingiliki waumin kimyaaaa...

ile n fedhea kwa gwajima kadhilishwa na pepo lake
 
MAMBO YA KUFUFUA NI IMANI YA DINI.LIVE PIE AS PIE..CHET KINATAKIWA
 
Uuuhhh gwajima hajawah kufufua hata panyaaa maneno kuntu hayo......

mchungaji gan ana mipasho kanisa limegeuka eneo la mipasho...nlcheka baada ya kuamuru pepo liende kwa makonda waumin wakashangalia hapo utajua hata waumin wa gwajima n mazombie akil zao mgando ndomana wanadanganywa gwajima anafufua...

baada ya pepo kugoma kumuingia makonda akisema haingiliki waumin kimyaaaa...

ile n fedhea kwa gwajima kadhilishwa na pepo lake
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Mapandikizi hayo
 
M
Dah! huyu ndiye ndugu yake anayemfahamu in and out " hajawaki kufufua hata panya" ila waliokutana naye bongo ndio wanajifanya kumuamini. Kamrarua ile mbaya
Masuhala ya imani na Uaskofu wa Gwajima ni mambo binafsi lkn vyeti vya mteule wa Rais huyu ni mtumishi wa umma. Analipwa mshahara kwa kodi zetu. Tunataka vyeti msituingize ktk ubashite wenu!
 
Back
Top Bottom