Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanasemaga mchawi ndugu.Huyo sio mdogo wake kwakweli...yani ndugu yako wa dam kabisa anatuhumiwa kuuza unga anadakwa na kulala central ...badala ya kumsaidia unasema ujinga kama huo..ety serikali inamlea sana Gwajima....ety anatuhumiwa vingi sana...hajamfufua baba wa watoto yatima ....huyu ni mjinga....kwaiyo anaisapport serikali imkandamize kaka yake...imfunge...imtuhumu kwa kuuza unga...huyu dogo anabidi akapimwe akili...Na sidhani kama ni mdogo wake wa kweli
Kwa ufupi
Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.
Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.
Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.
Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.
Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.
Hiyo sio hoja, siku zote walikuwa wapi? hiyo ni akili ndogo kutawala akili kubwa-Kwani Makonda ameteuliwa2 baada ya madawa ya kulevya? Haya ni majungu2Nawe usiwe kipofu na kujilazimisha kuziba maskio hoja iliyopo ni ya madawa ya kulevya na na suala la kujua jina halisi la mkuu wetu Wa mkoa ni makonda au ni bashite aweke vyeti kwanza
Umebeba nafsi ngapi za watanzania hapo ambao hawataki kujuaHilo tamko limeandaliwa wapi na nani? Je, hoja ya msingi ya forgery ni kweli au sio kweli? Hayo mengine wala watanzania hawahitaji kuyajua. Nguvu zooote anazotumia hapo si angeweka vyeti mezani akammaliza kabisa Gwajima forever and ever? Vinginevyo, this is another justification ya tuhuma za wizi wa vyeti. Yaani ndio anazidi kummaliza kabisa Bashite! Ha ha ha; kuna watu wapumbavu sijawahi kufikiria.
Wewe vyeti vya makondo vinakuhusu nini na vina msaada gani ktk maisha yakoWote tunajua kuwa hajawahi kumfufua hata panya, lakini ukweli unabaki kuwa HAYO HAYATUHUSU. Movie inayotuhusu ni hii ya kutaka kumfufua David Alubeto Tarantini Bashkoooooolite.
Huyo anatafuta umaarufu tu, hana lolote.
Yaani mwl.nyerere, baba wa taifa alijitahidi kweli ila nashangaa mijitu ilivyo mijinga nchi hii, hivi kweli hata kama ni yeye, awe ni public figure kama gwajima tena watu wanakuangalia ili wakufuate, halafu uchafuliwe tu kipuuzi bila evidence ukubali tu,Huyu naye ana matatizo; yaani Gwajima atuhumiwe hadharani kuwa drug-dealer halafu anyamaze tu? How? Very very wrong approach ya kujisafisha na tuhuma za wizi wa vyeti ... Tuhuma za kugushi vyeti zinasafishwa kwa kuweka vyeti hadharani na sio kwa kum-attack Gwajima personally.