Nimemsikiliza kwa makini huyu Mwanasheria, lakini bado nimeshindwa kuelewewa ni akina nani waliojitokeza hadhani wakaipinga hii vita ya madawa ya kulevya. Je ni kaka yake mchungaji Gwajima, au ni hawa wanaojadili mitandaoni?
Ni kitu cha ajabu kwamba, kila anyelijadili swala la vyeti la mheshimiwa RC wa Dar es salaam, sasa anaonekana ANAIPINGA hii vita ya madawa ya kulevya!
Mheshimiwa amejaribu kutuonyesha pia kuwa sisi watanzania, hatuwezi kutofautisha maswala haya mawili yaliyojitokeza hivi karibuni? Anajaribu kuonyesha kwamba, ukianzisha vita kama hii yenye umuhimu kabisa kwa jamii, si muda muafaka wewe kujadiliwa.
Counsel Gwajima akumbuke kwamba, Mheshimiwa RC alipanda jukwaani na kupaaza sauti, na akawatuhumu watu kadhaa. Vivyo hivyo, watu wamejitokeza na swala la vyeti, wamepaaza sauti dhidi yake, akiwemo mchungaji Gwajima ambaye ni mhanga wa zoezi lake. (What goes around, comes around, na dhambi ni dhambi tu)
Sina uhakika, lakini kwa mawazo yangu, nadhani kwamba vita ya mheshimiwa Makonda, imewagusa watu wengi, baadhi yao ambao walikuwa na historia yake, lakini hawakuwa na sababu za kuizungumzia.
Lakini ukweli utabakia kwamba, kuzungumza kwao kuhusu swala la vyeti vya RC, hakuwaondolei tuhuma hizo za RC, na hapa ndipo asipopaona, au asipotaka kupaona, Counsel Gwajima!
Eti anauliza watu walikuwa wapi siku zote wasiongelee swala la vyeti vya Makonda? Lakini pia hajiulizi siku zote Makonda alikuwa wapi asianzishe hii vita mapema? (Everything happens for a reason!) Counsel Gwajima, amenikumbusha kuhusu mwanasheria mwenzake anayesadikika kutaka kufungua kesi dakika za mwisho, ili kuusimamisha uchaguzi wa TLS.
Akumbumke kuwa, kila tukio lina mvuto wake, na kila zoezi lazima liwe na matokeo yake, na si lazima yawe yale yaliyotarajiwa na mhusika. Na kila raia ana haki ya kujadili, ilimradi havunji sheria.
Swali langu ni moja tu hapa kwa Counsel Gwajima:-
Mimi naamini kabisa kwamba ni watu wa kawaida sana wanoliongelea swala hili na vyeti, na hawana madaraka yoyote yale ya kiutendaji ya kuweza kuchukua hatua zozote zile stahiki. Je, kujadili, au kuongea kuhusu maswala ya vyeti vya RC, kunamzuiaje RC kuendeleza vita aliyoianzisha? Sitaki kujadili kama vita hiyo ilikuwa halali, au la!