Mdogo wa mke wangu (binti) amenidharau na kunitukana mbele ya mke wangu

Hilo nalo la kuuliza ningekua mimi ningemfungashia vitu vyake siku hiyo hiyo na huyo mkeo inaonekana hakueshimu anamletaje baba yake bila kujadiliana au kuomba ruhusa kwako??? Mmmmmh [emoji849] kuwa makini bro kuna jambo laja
 
Kaka hao ni wajita Amna mkurya wa hivyo aisee. Hizo ni tabia za kijita ndo baba mkwe anaweza kwenda kwa binti yake akakaa ata mwaka lakini sio mkurya

Sema nini na wajita ninao wajua Mimi wanatabia ya kuroga wanaume sio mkurya

Sas fanya hivi mkalishe mkeo umuulize nilichokisikia kutoka kwa ndugu yako ni sahihi na wew unaitaji iwe Ivo tena ongea nae kwa upole tu

Akikujibu ndio basi usipoteze mda achana nae, akikujibu hapana mpige marufuku kukanyaga dukani tena ikibidi ilo duka uza si umesema wew ni mwajiliwa uqezi kukuosa pesa ya matumizi nyumbn. Yeyeabaki kuwa mama wa nyumbani tu aleee watoto
 
Hapa shida ipo kwako mkuu, unaonekana unachukulia poa mambo, sasa mpaka wamekupanda kichwani, You need to act like a Man, usije ruhusu disrespect ndani ya nyumba yako hata siku 1.

Chukua hatua huyo mwenye degree yake akalime kwao, na mkeo alichokifanya uwajibike vile vile.
 
Warudishe wote Kwao. MI mkurya naowajua dada zetu viburi sana Hao. Ndo maana sisi tunawapigaga vitasa ili wakae sawa. Sasa wewe mchaga unaleta diplomasia ya Washington..... Ingetakiwa now unaandika na yeye shavu limevimba.
 
Kila kitu mshirikishe Mungu maana ndio atakusaidia nakumbuka familia yeti tuliamini Mungu nalituwezesha sana akatusaidia kwa jambo hili mshirikishe Mungu.

Jingine mke wako hakuolewa kwao atakuja kujuta sana pale huyo mdogo wake akimdhihaki pale ambapo ameshatia dosari ndoa yake.
Ukioa au kuolewa umehakikisha kuwa unamuweza basi alishindwa nini kukuambia ukweli??

Jingine hatuna uwakika kama hauna shida tunamdis mke wako tu so ndio hayo basi nadhani unajua mwenyewe.

Na yule dada mdogo wa mkeo kata fimbo tandika peleka kwa mwenye kiti mpandishe kwa basi arudi home kwa ndoa ni ya watu wawili sio watatu.

Kingine mkeo anakitu kachukia kamwambia dogo basi
 
Hiyo biashara ishaanza kumtia kiburi mkeo, fukuza huyo shemeji hapo nyumbani kwako, mkeo mpeleke akapumzike kwao kwa muda usiojulikana ,dukani weka mtu japo risk mpaka utakapoamua arudi, na atakaporudi hilo duka usimpe madaraka kama ni duka lake iwe tu kama msimamizi
 
jumatatu mbali, huyo anatakiwa kusepa leo au kesho. sio kwa ubaya wala nini, huyo ni mtu hatari sana, pia yafaa umwambie na babamkwe juu ya hilo na alichofanya na kukisema, na pia, unaonekana hauna sauti kwenye hiyo familia. sio kwa ugomvi wala nini lakini jitahidi kuwa mwanaume baba mwenye nyumba. kama kweli hiyo nyumba umejenga wewe mwenyewe.
 
Hii tamaa ya kugawa mali baada kuachana kwa wanandoa ni kwa upande wa wakristo tu kwa waislamu hukuti huu upumbavu na mtoa mada inaonekanan ilo jambo la kugawana mali limekushtua san na uyo shemeg yako hajaongea ivo kwa bahat mbay huo ndo mkakati walionao yey na dada yake la kufanya fukuza uyo shemeg mtu ata kesh asubuh mpem san na mpige stop baba mkwe abaki uko uko kwake na kaa chini na mke umueleweshe kuwa wew ndie mkuu wa kaya
 
Wanaume wengi wanaolalamika hapa JF ukisoma mikasa yao….Yaan unaelewa kabisa moja kwa moja why wanadharaulika!
Man up mdau!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…