Mdogo wangu wa kike amenitusi muda huu, ninatetemeka kwa hasira

Fanya kama alivyokushauri, acha kumfatilia kwasababu swali la nini afanye, nini asifanye lipo MIKONONI MWAKE. Hivyo anaona kama unazingua tu.

Kuna wale wadada wanalindwa sana shule za bweni za wasichana.. wakimaliza kuja vyuoni huku mhula wa kwanza tu keshapita na 'boyfrendi' wawili, wengine mhula wa kwanza tu ameshaishi na jamaa yake geto. Binafsi sionagi dhima ya kumlinda mtoto wa kike aliyefika utu uzima. Kama ulishindwa kumfunda akaelewa akiwa kitoto imeisha hiyoo.
.. Sema ukiwa brother kuna wakat lazima u act kibabe kwa hawa madogo wa kike kwa sababu sawa maamuz yapo mikononi mwake ya nn afanye na nn asifanye shida tu inakuja akishajazwa mimba na hao bodaboda akakimbia mji mtoto inakua jukumu lako brother, ww ndio utasimama kama baba kwa huyo uncle...kwa sababu obvious mama atakuwa yupo yupo tu na shule hajamaliza.. Dingi kakimbia automatic unakua mzigo wako sasa ukianza kuona dalili hzo kwa nn usiwe mkali au kumuasa at least awe muangalifu..

Sent from my MAR-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Huyu mdogo wangu yupo kidato cha nne, ninampenda sana na nimekuwa kama mshauri wake hususani kwenye issues za kujikinga na mahusiano kwa ujumla. Humfundisha mbinu za kuepuka vishawishi vya wanaume, kumpa madhara ya mimba na kumsisitiza asome kwa bidii. Kifupi tunapendana.

Sasa leo nimekuja hapa home nimekuta wanamsema huyu mdogo wangu, kuhusu tabia za kihuni. Mimi kama kaka mwenye uchungu na kuharibikiwa kwake nikalazimika kuvunga ili baadaye nimuulize. Sasa hatimaye nikapata nafasi nikamuuliza shida nini, akasema wanamsingizia ameanza uhuni. Nikamshauri sana na kumuambia asome kwa bidii, ukizingatia nimemzidi miaka 6.

Akanijibu na kuniambia niache mambo ya kike, niwe kama mwanaume na nisimfuatilie fuatilie. Sikuamini kwa kauli hii, nusu nizimie kwa kweli. Mpaka muda huu bado siamini, kosa langu lipi?

Je, au ndio haitakiwi kumpenda na kuzoeana na mdogo wako wa kike? Kumsisitiza kusoma ni kosa? Nimeukumbuka uzi humu wa jamaa akisema hakuna kucheka cheka na mwanamke awe ndugu yako au mtu baki, nimeamini sasa. Mbaya zaidi haya matusi amesikia mpaka house girl, ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana. Hivi nitamuangaliaje usoni? Kifupi sipo sawa, bora angekuwa mtoto ndiye amenitukana, ila huyu binti wa form four mwenye akili timamu mwenye miaka 20 hapana.

Bado sijaamini! Sijui cha kuomba ni nini, ushauri au... Nashindwa ku type sipo sawa.
Hajawahi kusikia fununu au hata kukuona una mpenzi ndio maaa kakuambia uwe kama mwanaume, na kwa sababu kakuambia ukweli ndio maana pia inakuuma.
 
Sijui amanita wapi kukujibu huo ujinga, huyo dogo itakuwa ni kweli kaanza uhuni na wala hawamsingizi, hapo anamuheshimu huyo boy wake wengine wote anawaona takataka.

Kwa kweli ingekula ni mdogo wangu mimi ndio kanijibu hivyo angekula viboko vya kutosha na ninahakika angemtaja huyo muhuni wake nisingejali umri wake naamini asingenisahau kwa mboko ambazo angekula. Pole sana mkuu wewe ni mnyonge sana.
Duuuuh
 
Huyu mdogo wangu yupo kidato cha nne, ninampenda sana na nimekuwa kama mshauri wake hususani kwenye issues za kujikinga na mahusiano kwa ujumla. Humfundisha mbinu za kuepuka vishawishi vya wanaume, kumpa madhara ya mimba na kumsisitiza asome kwa bidii. Kifupi tunapendana.

Sasa leo nimekuja hapa home nimekuta wanamsema huyu mdogo wangu, kuhusu tabia za kihuni. Mimi kama kaka mwenye uchungu na kuharibikiwa kwake nikalazimika kuvunga ili baadaye nimuulize. Sasa hatimaye nikapata nafasi nikamuuliza shida nini, akasema wanamsingizia ameanza uhuni. Nikamshauri sana na kumuambia asome kwa bidii, ukizingatia nimemzidi miaka 6.

Akanijibu na kuniambia niache mambo ya kike, niwe kama mwanaume na nisimfuatilie fuatilie. Sikuamini kwa kauli hii, nusu nizimie kwa kweli. Mpaka muda huu bado siamini, kosa langu lipi?

Je, au ndio haitakiwi kumpenda na kuzoeana na mdogo wako wa kike? Kumsisitiza kusoma ni kosa? Nimeukumbuka uzi humu wa jamaa akisema hakuna kucheka cheka na mwanamke awe ndugu yako au mtu baki, nimeamini sasa. Mbaya zaidi haya matusi amesikia mpaka house girl, ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana. Hivi nitamuangaliaje usoni? Kifupi sipo sawa, bora angekuwa mtoto ndiye amenitukana, ila huyu binti wa form four mwenye akili timamu mwenye miaka 20 hapana.

Bado sijaamini! Sijui cha kuomba ni nini, ushauri au... Nashindwa ku type sipo sawa.
UACHE KWELI,mdogo ako ana akili kukuzid wewe, acha shobo
 
Bro kwa hayo majibu huyo dogo alikua tayari kwa lolote hata kugombana na katika kugombana Kuna Mambo mengi akikulia tu timing na mtwangio akakushia nao kwenye medula ukakolapsi je utafanya nn ....? Si ndio aibu itakuwa maradufu.

Hapo dawa ni kumfungia tinted tu, unakata kamba nyanja zote block kila mahali , huduma zote ambazo ulitakiwa kumpa yeye kwa jeuri unaelekeza mashambulizi kwa beki tatu , yaani unamfanya beki tatu ndio Dada yako sasa ....kwa kufanya hivyo najua ataanza kumletea wivu beki tatu lakini wewe hakikisha unakua upande wa beki tatu maana ndio Dada yako kwa Sasa na kwakua anatumika huko nje na hawana malengo nae akisha pigwa pumbu tu na wahuni wakakimbia hapa akili itaanza kumkaa sawa lazima atajileta kwako na kukuomba msamaha na wewe hakikisha amekuomba msamaha si chini ya Mara tatu mazingira tofauti hapo ndio umsamehe na kwa conditions zako ...hapo utamnyoosha na atakuheshimu kweli na kukuogopa Sana ila akijileta tu na kimsamaha Cha kwanza tu ukaanza kuchekacheka hapa imekula kwako hayo mambo lazima yajirudie in advance mode [emoji38][emoji38][emoji38] utakuja kuleta uzi Tena humu wenye kichwa kinacho sema mdogo wangu amenitukana Tena amesema Mimi ni shoga
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mtafanya mtoa post ajiue
 
Mazoea yakizidi sana kwa watu ambao mindset zao ziko negative huwa yanaleta dharau
💯FACT! Pale nyumbani kuna housegirl aliletwa daah kuna uncle wangu mmoja akawa anamzoea zoea kiboya aisee mwisho wa siku yule housegirl akawa anawadharau nyumba nzima!
 
hao sio wa kuongea nao ni wa bakora na viboko mwanzo mwisho…wewe kakutukana vile ila kuna kidume ambaye unamzidi miaka anapewa romantic za kutosha tena dada yako akileta ushenzi anapigwa akiwa kavaa kisha anapigwa tena akiwa kavua…
 
Huyu mdogo wangu yupo kidato cha nne, ninampenda sana na nimekuwa kama mshauri wake hususani kwenye issues za kujikinga na mahusiano kwa ujumla. Humfundisha mbinu za kuepuka vishawishi vya wanaume, kumpa madhara ya mimba na kumsisitiza asome kwa bidii. Kifupi tunapendana.

Sasa leo nimekuja hapa home nimekuta wanamsema huyu mdogo wangu, kuhusu tabia za kihuni. Mimi kama kaka mwenye uchungu na kuharibikiwa kwake nikalazimika kuvunga ili baadaye nimuulize. Sasa hatimaye nikapata nafasi nikamuuliza shida nini, akasema wanamsingizia ameanza uhuni. Nikamshauri sana na kumuambia asome kwa bidii, ukizingatia nimemzidi miaka 6.

Akanijibu na kuniambia niache mambo ya kike, niwe kama mwanaume na nisimfuatilie fuatilie. Sikuamini kwa kauli hii, nusu nizimie kwa kweli. Mpaka muda huu bado siamini, kosa langu lipi?

Je, au ndio haitakiwi kumpenda na kuzoeana na mdogo wako wa kike? Kumsisitiza kusoma ni kosa? Nimeukumbuka uzi humu wa jamaa akisema hakuna kucheka cheka na mwanamke awe ndugu yako au mtu baki, nimeamini sasa. Mbaya zaidi haya matusi amesikia mpaka house girl, ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana. Hivi nitamuangaliaje usoni? Kifupi sipo sawa, bora angekuwa mtoto ndiye amenitukana, ila huyu binti wa form four mwenye akili timamu mwenye miaka 20 hapana.

Bado sijaamini! Sijui cha kuomba ni nini, ushauri au... Nashindwa ku type sipo sawa.
Kama unaishi kwenu hama.

Pia umekuja na story ya upande wako. Unajua sisi wengine tunasoma between lines. Mpaka anafikia kukuambia uache mambo ya kike, ni wazi wewe haumshauri bali unamfanyia unoko kinoma na unapiga sana gubu ambalo hapa unasema ni ushauri.

Acha hasira na ubadilishe approach. Msikilize pia kwani naye anazo akili zake ambazo hautakaa usmzijue hadi uoneshe kumuamini.

Boya sana wewe
 
[emoji817]FACT! Pale nyumbani kuna housegirl aliletwa daah kuna uncle wangu mmoja akawa anamzoea zoea kiboya aisee mwisho wa siku yule housegirl akawa anawadharau nyumba nzima!
Iko hivyo always
 
Miaka 20 yuko form four 🙆‍♀️🙆‍♀

Eti Watu8 hii sio chai kweli?
Angeachana nae tu huyo mbibi, alierudua madarasa anajua kila kitu,
Mimi nikimkanya mtu mara mbili huwa sirudii tena,
na yakimkuta ya kumkuta huwa sina huruma kabisa
 
Mkuu acha mambo ya kike yaani mpaka mdogo wako anakujua
 
Yaani unaheshimiana hadi na hausigelo, eti atakuonaje.!

Ukimaliza kutetemeka endelea kuandika, kuna vitu umeficha au umesahau.
 
Back
Top Bottom