Mdude adaiwa kuanika unyama aliofanyiwa na "Watekaji" wake

Wengi jana katika ile Maria Space walilia wake kwa waume baada ya kuyasikia maelezo ya kina ya Mdude kwa mateso. ya kutisha aliyoyapata kutoka kwa magaidi wanaojiita polisi, Mwenyezi Mungu ni mkubwa ndiyo sababu Mdude yuko hai hadi hii leo.

Hii MariaSpaces ni moto wa kuotea mbali, nilikua na usingiizi ila alipoanza kuongea Mdude ambaye ni muhanga wa "utekaji" usingizi ulikata. Nitajaribu kuweka Audio kama itakubali...
 
Yaani Mimi usingizi ulikata kabisa. Mungu atusaidie
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
K
we hujui tu kauli zake zilivo mbaya, eti utamnyoa??? president na tena mwanamke? yaani nadhan hao watekaji warudi kwake tena
Kwa kuwa umeng'angania mara mbili kudhihaki mateso aliyoyapata mdude, na kwa kuwa umeonyesha kwamba hauna utu kabisa, basi nakutabiria ukutane na mateso aliyoyapata mdude, kabla ya mwaka huu kupita ili akili zikurudie. Ameen
 
Ni wazo zuri sana Mkuu. Jana pia alisema anaandika kitabu. Nahofia kama ataandika maovu ya jeshi la magaidi katika kitabu chake basi sitashangaa hii Serikali haramu kukipiga marufuku.

..pia kuna kesi ya madai dhidi ya Igp na maofisa wa polisi ambao Mdude aliwatambua.

..nimesikia ktk mahojiano kwamba Mdude na upande wake wameamshamaliza kutoa ushahidi, isipokuwa hakimu / jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amehamishwa kituo.

..hiyo ni kesi muhimu sana na namuombea Mdude ashinde. Ushindi huo hautakuwa wa Mdude peke yake, bali kwa wote waliodhulumiwa na jeshi la polisi.
 
Kweli Mdude Chadema aliteswa sana na Magufuli na watu wake kwa kile anachoita ukosoaji.

Nilichokiona kwa Mdude hana lugha ya staha katika kukosoa huko. Maana hata aliposhinda kesi akatoa kauli ya kumnyoa Mama kwa wembe uleule aliomnyolea mtangulizi wake.

Ushauri:
Kama CDM ina viongozi wenye busara, basi mpumzisheni MDUDE apate tiba ya kisaikolojia kwanza
Vp wakianza na kukupumzisha wew upate afya ya akili kwanza? Japo waweza kuwa na point
 
Uko sawa Mkuu nilisikia hilo pia lakini sina imani na hizi mahakama zetu hivyo sioni uwezekano wa Mdude kupata haki yake mahakamani. Hata hiyo ya hakimu kuhamishwa ni mikakati michafu ya kuichelewesha kesi hiyo.

..pia kuna kesi ya madai dhidi ya Igp na maofisa wa polisi ambao Mdude aliwatambua.

..nimesikia ktk mahojiano kwamba Mdude na upande wake wameamshamaliza kutoa ushahidi, isipokuwa hakimu / jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amehamishwa kituo.

..hiyo ni kesi muhimu sana na namuombea Mdude ashinde. Ushindi huo hautakuwa wa Mdude peke yake, bali kwa wote waliodhulumiwa na jeshi la polisi.
 
Uko sawa Mkuu nilisikia hilo pia lakini sina imani na hizi mahakama zetu hivyo sioni uwezekano wa Mdude kupata haki yake mahakamani. Hata hiyo ya hakimu kuhamishwa ni mikakati michafu ya kuichelewesha kesi hiyo.
Mungu yuko nasi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
K

Kwa kuwa umeng'angania mara mbili kudhihaki mateso aliyoyapata mdude, na kwa kuwa umeonyesha kwamba hauna utu kabisa, basi nakutabiria ukutane na mateso aliyoyapata mdude, kabla ya mwaka huu kupita ili akili zikurudie. Ameen

huo mda ungetumia kumuombea mdude akili zikae sawa nadhan angekua anaongea vitu vinavoeleweka saaahv! matumizi mabaya ya maombi
 
Hii MariaSpaces ni moto wa kuotea mbali, nilikua na usingiizi ila alipoanza kuongea Mdude ambaye ni muhanga wa "utekaji" usingizi ulikata. Nitajaribu kuweka Audio kama itakubali...

Kwa kifupi ni kwamba
1. Walimpigisha shoti ya umeme kwenye chuchu na sehemu ya haja kubwa Mara kadhaa

2. Kwamba alipigwa uume wake kwa chupa ya maji. Yaani inajazwa maji halafu unapigishwa kwenye uume

3. Kwamba alimuriwa kusali sala yake ya mwisho kabla ya $kupotezwa"
4. Kwamba mashahidi wake walitishwa na hivyo kuamua kutokutoa ushahidi
5. Kwamba aliumizwa sana kwenye nyayo zake kwa vipigo
6. Mengine utasikiliza

Naiombea Tanzania, sijui watesi wa Mdude ni akina nani na sitaki kuchukua upande wowote ila Mungu atusaidie.
Hatimaye Mungu ameshinda.
 
K

Kwa kuwa umeng'angania mara mbili kudhihaki mateso aliyoyapata mdude, na kwa kuwa umeonyesha kwamba hauna utu kabisa, basi nakutabiria ukutane na mateso aliyoyapata mdude, kabla ya mwaka huu kupita ili akili zikurudie. Ameen

na hata ivo kijana wenu anatuchanganya sana, mara kateswa mara kamnyoa mtu sasa tushike lipi
 
Back
Top Bottom