PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Masai wa Town

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
7,009
Reaction score
25,406
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.


​
Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

1746166179607.png


*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

Mdude-CHADEMA1.jpg
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
m2.jpg

​
Pia soma
  1. Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
  2. Sakata la kutekwa kwa Mdude, mzee afichua jinsi Polisi walivyomfuata kutaka awasaidie kumfanyia Ujasusi ili wampate
 
Mdude hakutakiwa kuishi namna hii, bila ulinzi, bila tahadhari yeyote na bila back-up. Mdude amekuwa target kwa siku nyingi na cold-blood murderers.
CHADEMA wanatakiwa waanzishe na kuimarisha mkakati wa kulinda watu wao, waandae mkakati wa tahadhari. Ukishakuwa mkosoaji kwa utawala kama wetu unakuwa haupo salama.
 
Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu. Walikuwa na silaha, wamevunja mlango. Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwakwe Mbeya.
Hivi polisi kumkamata mtu ni lazima kumpiga? Hii ni sheria ya wapi?
Kwa nini utaratibu mbovu huu ndio sasa uzoelekee na kukubaliwa kama ni kawaida ya polisi kufanya kazi?
 
Mdude hakutakiwa kuishi namna hii, bila ulinzi, bila tahadhari yeyote na bila back-up. Mdude amekuwa target kwa siku nyingi na cold-blood murderers.
CHADEMA wanatakiwa waanzishe na kuimarisha mkakati wa kulinda watu wao, waandae mkakati wa tahadhari. Ukishakuwa mkosoaji kwa utawala kama wetu unakuwa haupo salama.
Unataka red brigade waanze kupambana na polisi wenye silaha?
Mdude alitakiwa kutafuta namna ya kuishi usieleweke. Mtu unajua wakati wowote utafanywa chochote halafu unaishi kama kuku banda Hilo hilo saa 12 umeshaingia.
 
Mdude sio mkosoaji ni mjinga flan tu asiejielewam mwenyekiti wake maana huwa anaongea as if mdomo na ubongo vimetengana so lazima wamsynchronize. Unaona watu wana silaha na gwanda za polisi wamekuja kukukamata then unaanza kupambana nao. Wao wanaruhusiwaukugonga ukizubaa unavunjwa viungo. Anachokipata ni haki yake
 
Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu. Walikuwa na silaha, wamevunja mlango. Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwakwe Mbeya.
Hawa watu wanaumiza watanzania wasio na hatia, ina maana usiseme ukiona mtu anaonewa? Huu woga utaendelea mpaka lini? Tuamke watanzania, hao polisi si wengi wa kutunyanyasa hivyo. Tuchukue hatua, tujilinde
 
Hivi hao polisi kwani wanaishi wapi?

Kama wanaishi humu humu uraiani basi wananchi sasa nao inabidi waanze kuwawinda na kuwafanyia mbaya.

Hata ikibidi kuwawekea sumu kwenye vinywaji au vyakula, poa tu.

Ikibidi kuwawinda na kuwanyatia na kuwapiga mishale, mapanga, marungu, nayo poa tu.

Watu watakuwa wanyonge mpaka lini?
 
Hivi hao polisi kwani wanaishi wapi?

Kama wanaishi humu humu uraiani basi wananchi sasa nao inabidi waanze kuwawinda na kuwafanyia mbaya.

Hata ikibidi kuwawekea sumu kwenye vinywaji au vyakula, poa tu.

Ikibidi kuwawinda na kuwanyatia na kuwapiga mishale, mapanga, marungu, nayo poa tu.

Watu watakuwa wanyonge mpaka lini?
Yaani hao police wakijisikia tu kupiga na kuteka, wanavamia tu na kuvunja milango ya watu wasio na hatia. Mdude amekosa nini? Uonevu tu nchi hii, huyo mama ameshanogewa na kutesa na kuua.
 
Usiku huu, ndugu yetu Mdude_Nyagali amenyakuliwa na watu waliojitambulisha ni maafisa wa polisi akiwa katika makazi yake Mbeya usiku huu. Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Tazama clip hapa chini by MMM:

Hii ni damu ya Mdude baada ya makazi yake huko Iwambi, Mbeya kuvamiwa na watu waliojitambulisha ni polisi. Walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

 
Back
Top Bottom