Mdude Nyagali atendewe haki. Amewatambua watu waliomteka na kumtesa. Pia ametaja mpaka maeneo alipopelekwa kuteswa

Mdude Nyagali atendewe haki. Amewatambua watu waliomteka na kumtesa. Pia ametaja mpaka maeneo alipopelekwa kuteswa

April 22, 2022
Dodoma, Tanzania

TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA ( THBUB) YAPONGEZWA KWA KUWEKA MKAKATI KUTENGENEZA MPANGO KAZI WA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA NCHINI.


e06d4819c74678099ae438d8c3358729

Waziri wa Katiba na Sheria. Dkt. Damas Ndumbaro(MB) ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuona umuhimu wa kutengeneza mpango kazi wa Haki za Binadamu na nchini.

Mhe. Ndumbaro alitoa pongezi hizo Aprili 22,2022 wakati wa kikao kazi cha kuitambulisha Tume na majukumu yake katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo Mji mkuu wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

“Niwapongeze kwa andiko hilo,naimani andiko hilo litatibu matatizo ya haki na biashara nchini kwa kizazi cha sasa na baadae ’’Alisema Mhe. Ndumbaro
Aidha Mhe.Ndumbaro alitoa wito kwa Tume kuendelea na mchakato huo wa andiko kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuhakikisha kuwa tunasheria ya haki na usawa itakayosimamia haki za biashara nchini.

Awali akiwasilisha rasmi tamko kwa serikali Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Mathew P.M Mwaimu (Jaji Mstaafu) alisema kuwa mkakati wa kutengeneza mpango kazi wa haki za binadamu na biashara utasaidia kuepushaa migogoro hasa ya ardhi hasa kwa upande wa fidia inapotokea kuanzishwa kwa shughuli za biashara.

Mhe. Mwaimu alieleza kuwa ,Tume Katika kutekeleza masuala ya Haki za Binadamu na Biashara, inafanya uchunguzi, ufuatiliaji, tathimini, utafiti, kuendesha midahalo na kutoe elimu kwa wadua wa haki za binadamu na biashara pamoja na umma.

‘Tume kupitia kazi hizo imebaini kuwa shughuli za biashara kupitia sekta mbalimbali hupelekea uvunjifu wa haki za binadamu.’Alisema Mhe Mwaimu
Kwa hatua ingine Mhe.Ndumbaro alitoa rai kwa Tume kuweka utaratibu mzuri wa kushirikiana na Taasisi binafsi zinazoshughulikia maswala ya haki za binadamu na utawala bora nchini ili kuwa na taarifa za pamoja,Ikiwa pamoja na kuandaa andiko la haki jinai nchini

Source : THBUB | Habari
 
mbunge atoa mifano hai jinsi chombo hiki kilivyotelekezwa na serikali kikibaki ombaomba kusubiri fedha za wafadhili wa nje ili kiweze kufanya majukumu yake muhimu ya kuhakikisha haki za binaadamu na utawala bora nchini mwetu unafuatiliwa.

9 April 2022
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Jaji Mwaimu na Naibu Mkurugenzi DIHR wakutana kuzungumzia mashirikiano​



Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (wa pili kushoto) akiongea na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Danish Institute for Human Rights, Bi. Eva Grambye (mwenye vazi jekundu) na timu yake, hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam, Aprili 8, 2022.

Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (wa pili kulia) akiendelea kuongea, huku Bi. Eva Grambye na timu yake wakimsikiliza kwa makini.

Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Spandet (wa pili kushoto, mwenye vazi jeupe) akieleza jambo wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Danish Institute for Human Rights yaliyofanyika hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam, Aprili 8, 2022.

Washiriki wa mazungumzo baina ya Tume na Danish Institute for Human Rights wakipata mlo wa pamoja.

Na Fadhili Muganyizi

MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mstaafu) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya nchini Denmark (Danish Institute for Human Rights – DIHR), Bi. Eva Grambye hivi karibuni wamekutana kuzungumzia mashirikiano baina ya taasisi zao.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ijumaa Aprili 8, 2022 hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam viongozi hao pamoja na mambo mengine walizungumzia mashirikiano kwenye masuala ya haki za binadamu na biashara na mradi wa upatikanaji wa haki (Access to Justice Project).

Pia, walizungumzia mustakabali wa mradi uliofanyiwa marejeo (Revised National Human Rights Action Plan), hususan majukumu ya Tume kwenye mradi huo na namna ambavyo DIHR inaweza kuisaidia Tume.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Bi. Mette Spandet.

Kwa upande wa Tume, Mhe. Mwenyekiti aliambatana na Afisa Uchunguzi Mkuu, Bwana Philemon Thomas (kutoka Ofisi ya Tume Tawi la Dar es Salaam) na Afisa Uchunguzi Mwandamizi, Bwana Fadhili Muganyizi (kutoka Ofisi ya Tume Makao Makuu, Dodoma)
 

Tuesday, April 19, 2022​

Jaji Mwaimu awapongeza wanawake watetezi wa haki za binadamu​



Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (wa kwanza kulia) akifuatilia moja ya mawasilisho yaliyotolewa katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, iliyofanyika hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2022.



Washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wakifuatilia wasilisho lililokuwa likitolewa wakati wa ghafla hiyo iliyofanyika hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2022.


MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mstaafu) ameupongeza Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (CWHRDs) kwa kazi nzuri za kiutetezi wanazofanya hapa nchini.

Mhe. Mwaimu ametoa pongezi hizo leo (Aprili 19, 2022) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kwanza wa miaka mitano (2022 – 2026) wa taasisi hiyo, iliyofanyika hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mwenyekiti wa Tume amesema kuwa anaamini mpango mkakati uliozinduliwa utaongeza kasi ya utendaji kazi wa taasisi hiyo ya ulinzi na utetezi wa haki za binadamu, hususan haki za wanawake na watoto nchini.

Mhe. Jaji Mstaafu Mwaimu ameahidi kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kama taasisi iliyo kitovu cha ukuzaji na utetezi wa haki za binadamu nchini itatoa ushirikiano unaohitajika katika utekelezaji wa malengo ya mtandao huo.

CWHRDs yenye makao yake makuu Mwenge, jijini Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kuwaleta pamoja wanawake watetezi wa haki za binadamu, kulinda maslahi yao na kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa kazi zao.
 
kwamba ukitukana haubaki salama. Hatuna sheria wala mahakama hadi tuamue kutobakisha watu salama?

Ni wapumbavu tu hutafuta kutowabakisha watu salama.

Mbowe aliitwa gaidi sisi wanaCCM tukaishia kufurahia, mwisho wa siku ametoka bila kuhukumiwa kuwa ni gaidi.

Leo hii mnawajua mawakala wa CIA nchini ila mmeufyata mkia hamchukui hatua. Acheni chuki zenu zinazowafanya kujiropokea tu bila kufikiri.
Mdude ni mpumbavu, na kitabu chake kimejaa uchochezi, akamatwe tena. Huwezi kutukana watu hovyo hovyo mitandaoni ubaki salama, kauli yako ya kwamba wembe uliomnyolea JPM ndio mtamnyolea SSH imemlaza mwenyekiti wenu rumande. Ngoja maria akudanganye,mama wa Maria ni wakala wa CIA
 
Sheria inawalinda usalama wa taifa wakiwa wantekeleza majukumu yao, so akae kwa kutulia next time akizingua tena watamtengeneza vizuri zaidi.
 
Mdude ni mpumbavu, na kitabu chake kimejaa uchochezi, akamatwe tena. Huwezi kutukana watu hovyo hovyo mitandaoni ubaki salama, kauli yako ya kwamba wembe uliomnyolea JPM ndio mtamnyolea SSH imemlaza mwenyekiti wenu rumande. Ngoja maria akudanganye,mama wa Maria ni wakala wa CIA
Ambatanisha na facts otherwise wewe ndiye mpumbavu unaye-post uchochezi.
IMG_20220430_165809.jpg
 
..Haiwezekani mhanga atoe ushahidi kama huu wa Mdude halafu hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya waliohusika kumtesa.

..Ninashangaa kwanini Tume ya Haki za Binadamu, Chama cha wanasheria wa Tanganyika, na asasi nyingine za haki za binadamu, ziko kimya kuhusu suala hili.

..Msikilizeni Mdude akitoa ushuhuda wake kuhusu yaliyomtokea.


Ule utawala dhalimu kabisa kuwahi kutokea
 
Kuna tatizo kubwa, taasisi husika zimeingia ganzi miguuni

29 April 2022
Bunge la Bajeti
Dodoma, Tanzania

MBUNGE AIBUA HOJA KUWA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA TANZANIA NI TUME-MFU, IMEGOMA KUFUATILIA MATUKIO YA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU?



mbunge atoa mifano hai jinsi chombo hiki kilivyotelekezwa na serikali kikibaki ombaomba kusubiri fedha za wafadhili wa nje ili kiweze kufanya majukumu yake muhimu ya kuhakikisha haki za binaadamu na utawala bora nchini mwetu unafuatiliwa.

Raia wanatekwa na kuachiliwa mfano Mo Dewji, Roma Mkatoliki kwa kuwataja kwa uchache, Tundu Lissu kushambuliwa pia mauaji kule Mtwara na Tanga lakini hatujasikia Tume ikikemee wahusika wasiojulikana au kuzitaka na kuzisaidia taasisi na idara husika au maofisa kutoa taarifa nini wamefanya kuwafahamu watu wasiojulikana na pia kusaidia mfumo wa Jinai Haki (Criminal Justice System) kuweza kuwezeshwa kifedha, rasilimaliwatu na utashi haki itendeke.

Mbunge anasema kwa hali ilivyo ni kuwa Tume hiyo inafufuka tu wakati wa kusomwa bajeti ya wizara mama ya Katiba na Sheria lakini baada ya hapo inarudi kusinzia bila kufanya majukumu yake muhimu ya kuhakikisha haki za binadamu na utawala bora nchi unaimarishwa kwa vitendo, kwa kukemea, kuelimisha na kufuatilia kisha kutoa majibu kwa uwazi kwa umma wa waTanzania ili imani irudi kuwa haki za binadamu na utawala bora upo nchini.

Hii tume sijui huwa inafanya nini
 
Mdude ni mpumbavu, na kitabu chake kimejaa uchochezi, akamatwe tena. Huwezi kutukana watu hovyo hovyo mitandaoni ubaki salama, kauli yako ya kwamba wembe uliomnyolea JPM ndio mtamnyolea SSH imemlaza mwenyekiti wenu rumande. Ngoja maria akudanganye,mama wa Maria ni wakala wa CIA

..unataka kusema mke wa Prof.Sarungi ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wa Tz ni wakala wa CIA?

..hivi hizi propaganda zenu huwa mnazitafakari kabla ya kutuletea?
 
..unataka kusema mke wa Prof.Sarungi ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wa Tz ni wakala wa CIA?

..hivi hizi propaganda zenu huwa mnazitafakari kabla ya kutuletea?
Ndio, mama yake Maria Sarungi ni wakala wa CIA na CIA ndio wanaomfadhili Maria, wanamlinda huko Nairobi na wamemlipia nyumba, wachangiaji maalum huko space hulipwa na CIA milioni mbili kwa siku.

Mdude alitibiwa Nairobi kwa usaidizi wa CIA, Mbowe alivyotoka stoo, pia CIA walimlipia matibabu Nairobi, hata Lema walimpitisha boda na kumtafutia hadhi ya ukimbizi
 
Sema huyu ndorobo ana matusi jamani...khee!! Sijui kana jiamini nini!??
 
Back
Top Bottom