Mdude Nyagali na saluti: Hii tabia Watanzania tulio raia tumejifunzia wapi?

Mdude Nyagali na saluti: Hii tabia Watanzania tulio raia tumejifunzia wapi?

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2020
Posts
12,077
Reaction score
12,786
Leo katika mkutano wao wa katiba ambao Ndg. Mbowe ameendelea kudhihirisha ukaidi alionao kwa mamlaka za nchi ya "kijamaa" ndugu yetu mdude nyagali ametushangaza.

Mdude nyagali amenishangaza vipi?

Tabia inayoota mizizi hapa nchini.

Mdude nyagali alitoa ishara ya saluti kwa meza kuu pale alipoitwa kwenda kumsalimia mwenyekiti wake Mh. Mbowe.

Ishara ile aliyoitoa ni salamu ya jeshi (saluti).

Je, raia anatakiwa kutoa salamu ya saluti ya kijeshi kwa viongozi wake?

Majibu ni haya:

1) Hata askari wa cheo kikubwa wacha kidogo, haruhusiwi kutoa ishara ya salamu ya saluti akiwa nje ya majukumu ya kikazi ambayo anakuwa hajavaa sare kamili za kijeshi. Ikumbukwe bila ya kuvaa kofia ya kijeshi kichwani basi sare hiyo haijatimia.

Hapa tunapata funzo kutoka kwa mh.Mkuu wa mkoa Ndg. Makongoro Nyerere siku ile alipoapishwa na mh.Rais samia suluhu hassan. Ndugu Makongoro Nyerere aliisogelea meza ya uapisho kwa ukakamavu mkubwa wa kijeshi bila ya kupiga saluti bali kusimama kwa kuchuchumia akitanguliza ukakamavu wa utii baada tu ya kuinama kwa kuunyoosha mgongo kwa adabu na nidhamu tele.

2) Raia haruhusiwi kuipiga salamu hiyo ya kijeshi (saluti) kwa raia mwenzake ama hata kwa askari kwani ni kinyume kabisa na utaratibu wa kijeshi.

Ikumbukwe kipindi cha msiba wa mpendwa wetu hayati JPM (RIP) walionekana baadhi ya viongozi wakitoa salamu hiyo ya jeshi huku wakiwa ndani ya nguo zao za kiraia.

Kwa kuwa chadema wanavaa mavazi mekundu na wakati mwingine bereti nyekundu vichwani, je wameanza kujifanya ni chama cha "EFF" cha Afrika Kusini kinachoongozwa na el comandante tate julius malema?

Chadema wameanza lini kuwa wakomunisti? 🤣🤣🤣

Kweli chadema ni chama cha maigizo, yaani wao si wakomonisti ila wanavaa makombati na bereti nyekundu vichwani 🤣🤣🤣

Ushauri wangu:

Tabia hii ya raia kupiga saluti za kijeshi haina afya na vyema tukaiacha na kujirekebisha kwani kama wanasiasa wanapenda mambo ya jeshi basi wajue kujiunga nalo hakukatazwi, wanaweza kuacha siasa na kwenda JKT na majeshi mengineyo ili wakafurahie salamu hizo za kijeshi!

Ndimi MuuzaAl KasusuTandale

#NchiKwanza
#TaifaKwanza
#KaziIendelee
#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM

remembrance-sunday-harry1.jpg

Army-D-Day-commemoration-3200.jpg
 
Wapi pameandikwa ni za polisi ?!!

Mkuu hivi sare za jeshi la police zinakosa maandishi ya POLISI kifuani ?!!!

Hivi sare za Polisi huwa zinavaliwa na MKUFU shingoni ?!!!

Iangalie vyema hiyo picha ya Komredi SABAYA.....
 
Nyie mlihalalisha mbona inawauma sasa
Sisi akina nani ?!!!

Mimi nimemtaja MDUDE....pia nikawataja baadhi ya "viongozi" waliofanya hayo kipindi Cha msiba wa kipenzi chetu hayati JPM( May his soul rest easy amen)!
 
Back
Top Bottom