Mdude Nyagali na saluti: Hii tabia Watanzania tulio raia tumejifunzia wapi?

Mdude Nyagali na saluti: Hii tabia Watanzania tulio raia tumejifunzia wapi?

Leo katika mkutano wao wa katiba ambao Ndg. Mbowe ameendelea kudhihirisha ukaidi alionao kwa mamlaka za nchi ya "kijamaa" ndugu yetu mdude nyagali ametushangaza.

Mdude nyagali amenishangaza vipi?

Tabia inayoota mizizi hapa nchini.

Mdude nyagali alitoa ishara ya saluti kwa meza kuu pale alipoitwa kwenda kumsalimia mwenyekiti wake Mh. Mbowe.

Ishara ile aliyoitoa ni salamu ya jeshi (saluti).

Je, raia anatakiwa kutoa salamu ya saluti ya kijeshi kwa viongozi wake?

Majibu ni haya:

1) Hata askari wa cheo kikubwa wacha kidogo, haruhusiwi kutoa ishara ya salamu ya saluti akiwa nje ya majukumu ya kikazi ambayo anakuwa hajavaa sare kamili za kijeshi. Ikumbukwe bila ya kuvaa kofia ya kijeshi kichwani basi sare hiyo haijatimia.

Hapa tunapata funzo kutoka kwa mh.Mkuu wa mkoa Ndg. Makongoro Nyerere siku ile alipoapishwa na mh.Rais samia suluhu hassan. Ndugu Makongoro Nyerere aliisogelea meza ya uapisho kwa ukakamavu mkubwa wa kijeshi bila ya kupiga saluti bali kusimama kwa kuchuchumia akitanguliza ukakamavu wa utii baada tu ya kuinama kwa kuunyoosha mgongo kwa adabu na nidhamu tele.

2) Raia haruhusiwi kuipiga salamu hiyo ya kijeshi (saluti) kwa raia mwenzake ama hata kwa askari kwani ni kinyume kabisa na utaratibu wa kijeshi.

Ikumbukwe kipindi cha msiba wa mpendwa wetu hayati JPM (RIP) walionekana baadhi ya viongozi wakitoa salamu hiyo ya jeshi huku wakiwa ndani ya nguo zao za kiraia.

Kwa kuwa chadema wanavaa mavazi mekundu na wakati mwingine bereti nyekundu vichwani, je wameanza kujifanya ni chama cha "EFF" cha Afrika Kusini kinachoongozwa na el comandante tate julius malema?

Chadema wameanza lini kuwa wakomunisti? 🤣🤣🤣

Kweli chadema ni chama cha maigizo, yaani wao si wakomonisti ila wanavaa makombati na bereti nyekundu vichwani 🤣🤣🤣

Ushauri wangu:

Tabia hii ya raia kupiga saluti za kijeshi haina afya na vyema tukaiacha na kujirekebisha kwani kama wanasiasa wanapenda mambo ya jeshi basi wajue kujiunga nalo hakukatazwi, wanaweza kuacha siasa na kwenda JKT na majeshi mengineyo ili wakafurahie salamu hizo za kijeshi!

Ndimi MuuzaAl KasusuTandale

#NchiKwanza
#TaifaKwanza
#KaziIendelee
#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM

View attachment 1837245
View attachment 1837247
Kaka funguka ubongo, kuna vitu vidogo sana vya maisha vitakuua kwa kihoro. Live your life.
 
Kaka funguka ubongo, kuna vitu vidogo sana vya maisha vitakuua kwa kihoro. Live your life.
🤣🤣
Sina kihoro mkuu.....

Nafunguka kubainisha "uzushi na ubabaifu wenu" CHADEMA ....
 
Ali Kiba kaimba wimbo wa SALUTE na kapiga full ngwamba, navielekeza vyombo vya dola atiwe mbaroni mara moja.
 
Wapi pameandikwa ni za polisi ?!!

Mkuu hivi sare za jeshi la police zinakosa maandishi ya POLISI kifuani ?!!!

Hivi sare za Polisi huwa zinavaliwa na MKUFU shingoni ?!!!

Iangalie vyema hiyo picha ya Komredi SABAYA.....
Acha ubish hiyo ni unform ya police haijalish kavalia nn sabaya alilewa madaraka
 
Kwa hiyo hadi uwe recruited jeshini ndo unaruhusiwa kupiga saluti, unaelewa mtu anapokwambia 'I salute you' au tatizo ni kuweka ile ishara ya saluti, ila kuongea ni sawa.....
 
Yaani nimecheka mpaka mate yanaanguka hovyo. Tena Makonda akiwa raia plain kabisa akaisaluti maiti. Shida Moja kabla ya kuandika Jambo muhimu watu hatufanyi kautafuti kidogo.
Wanaonaga chadema tuu
 
Hii salute imeandikwa kama ilitoka kwenye maandiko na vitabu vya dini

Maajabu Africa hayaishi kwa kweli
Mbona John Cena anapiga salute
Hata shule tulikuwa tunapiga salute kwa sana tu
 
Sisi akina nani ?!!!

Mimi nimemtaja MDUDE....pia nikawataja baadhi ya "viongozi" waliofanya hayo kipindi Cha msiba wa kipenzi chetu hayati JPM( May his soul rest easy amen)!
Kwanini hukuandika alipofanya makonda unangoja mdude apige ndio uropoke
 
kwaiyo apo kaiba chombo cha dola au nyaraka ya serikali kosa ni nini apo?
 
Back
Top Bottom