Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Tatizo watanzania wengi hawaijui siasa,wanadhani siasa ni mapambio sijui mnataka Chama cha upinzani nacho kimsifie Mama kama CCM.
Tafuteni documentaries za Nchi zingine muelewe maana ya siasa.
Ndio Kamanda, makamanda tunataka siasa kama za Afghanistan, Chechnya, nk dadeki..
Mdude ni Mandela aliyetufufukia Tanzania..you know why...
Mzuka unapanda makamanda
 
Utakuwa wa uswahilini wewe kwa uchonganishi. Utakuwa bonge la mbea. Magufuli mwanamke = Tofauti yake na Joseph Magufuli ni kwenye me/ke tu. Matendo yake ni sawa na ya Magufuli tu.
Rais Samia Leo Tundulisu anakubatiza Jina ambalo sio lako anaamua kukuita Magufuli Mwanamke How Rais wa nch na Rais alie kua Madarakan wanakashifiwa kiasi ichi
 
Lisu hakomi huyu. Kumshambulia Rais kutamshushia credibility
 
Kwa maoni yako basi yupo hapo kwa bahati mbaya. Alafu usipende kumchukulia mwanamke kuwa hawezi na niwa kuonewa huruma tu. Huyo yupo hapo na anajitosheleza acha mfumo dume.
 
Mshauri mheshimiwa SSH,Kama unaweza kushauri. Mnajadili mada kwa pupa tu.
 
"...mwambieni huyo mama yenu, wembe niliotumia kumnyoa mtangulizi wake, nitamnyolea yeye akiendelea kuleta jeuri"

MDUDE NYAGALI,
Kada wa Chadema.
1 July 2021.
 
Lini credibility yake ilishuka?
Wkt wa Jiwe mlisema hivihivi.
Nyie mdaganyeni kwanini hamsomi alama za nyakati na situation yetu kwa Sasa nyie kujiropokea tu na hyo inatumiwa muonekane wahuni.
 
Kwa maoni yako basi yupo hapo kwa bahati mbaya. Alafu usipende kumchukulia mwanamke kuwa hawezi na niwa kuonewa huruma tu. Huyo yupo hapo na anajitosheleza acha mfumo dume.
Anajitosheleza kutukanwa? Mfumo dume umesema? Hapa unapotosha au umepotoshwa, mfumo dume ni nini haswa?

Mbona miaka 5 iliyopita hatukusikia hizi critics?
 
Mama Samia ameweka kando uhalisia na sasa anajaribu kudeal na hisia.

Hajawajua Chadema kwamba ni zaidi ya Chama cha Siasa.

wana stress za kufa mtu hivyo wanafanya lolote bila kujali madhara
 
Hakana adabu haka kajitu
 
Acheni ujinga...
Japo siungi mkono lakinil alichofanya Mdude ni nusu ya walichowahi kufanya viongozi kadhaa wa ccm kina Sabaya, Heri, Mwigulu, Hepi, Makonda, Magu, na wengine wengi tu. Hata humu jukwaani tua watu kina Jingalao, johnthebaptist n.k ambao wao mkitofautiana mawazo wanahalalosha matusi na bifu!
Tuache unafiki. Kama upinzani ukitumia lugha ngumu ni dhambi kubwa basi iwe hivyo kwa maccm.
Lakini ili haya yadhibitiwe tunahitaji Katiba Mpya iweje kabisa utaratibu wa kuzuia "Hate-Speech". Tusipofanya hivyo tunakoroga sumu moja mbaya sana!
 
Wana Siasa za Maji Taka sana hawa!
 
Habar wadau wa jamiforums

Nilikua nimesema nisijiusishe Tena na siasa ila kwenye ili nimeona ninayo haki ya kusema jambo...
Mdude aliishinda serikali ya ccm mahakamani , hakutolewa kwa huruma ya mtu , sasa tunapojenga hoja tujikite kwenye mambo yahusuyo
 
Nimelia vibaya mno

Mama kwa busara zake mdude alitoka

Mama kwa busara zake kairudisha nchi kwenye demokrasia

Mama kwa busara zake watumishi wa umma wameanza kuwa na matumaini

Mama kwa busara zake pesa imeanza kuonekana mtaani wananchi tunafurahia

Leo hii anaibukia mpuuzi mmoja, mkosa adabu mmoja,asiyefunzwa na mama yake wala ulimwengu aitwaye mdude nyangali anamtukana rais na lugha chafu ya kejeli kumbully rais kwa lugha ya matusi yaani nimeliaahhh.

Nimepandwa na jazba usiku huu nimejuta kwanini nimeiona hiyo video nimelia sana kwasababu huyu mama hastahili kutukanwa nimesikia hadi uchungu kwamba ndo mama yangu anatukanwa hivyo yaani ningekufa maana hata ningekosa cha kufanya maana mtoa matusi angestahili zaidi ya adhabu yoyote kali.

Huyu mdude kanifanya niichukie chadema sana,hiyo ndo shukrani yako mdude hii clip imeharibu siku yangu, nimelia sana kwa uanaharakati gani kama ndo hivi?Kwanini utukane na lugha kama hii?

Nimelia sana na sitosahau hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…