Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Mdude ni muathirika wa utawala wa CCM - bila mawakili imara pamoja na safari ya Mwendazake huko alikokwenda huyu jamaa angefungwa si chini ya miaka 30 jela, ina maana angetoka akiwa Mzee, huu ni ukatili wa ajabu kabisa kumfanyika mwanadamu mwenzako no matter what. .. yaani kisa tu kakukosoa kwamba wewe ni dikteta uchwara ndiyo umpe adhabu hii ya kuharibu kabisa future yake kabisa... no no no

Sasa kwa mliyomfanyia ana haki ya kusema hayo... CCM kama mnaona anakosea basi mtafutieni mwana saikolojia amsaidie - nyie ndiyo mmemsababishia hayo yote.
 

Mwenyewe nashangaa wanasapoti ujinga badala kumkana....Mwanaume mzima unamtolea kauli chafu mwanamke!!!, hata kwa mtu yeyote pia kauli hii sio nzuri aise.....kwanza huyo ni sawa na mama yake aliemzaa na isitoshe ni Raisi wake.....kama ni mimi namtia adabu

"Mwambieni huyo mama yenu nitamnyoa" duhh!
 
Ndugu yangu eliakeem hiyo ni dhana lakini si tusi kama linavyochukuliwa na chawa wa uvccm . Yeye mama anakatalia haki ya wananchi. AambiweJe ajue anawakwaza sehemu ya wananchi anaowaongoza ?!

Uchumi wa nchi hii umeanza kujengwa 1961 . Yeye mama akiwa na miaka miwili . Na haujawahi kusimama kujengwa hata mwaka moja . Sasa kuwakatalia wananchi hitaji lao ndiyo hekima kwa kigezo cha uchumi ?! Huyu anafaidika na ubovu wa katiba mbovu. Nothing much

Haki hupiganiwa , hailetwagi na watawala kama hisani
 

Je wewe unaona hiyo ni namna nzuri ya kumuambia kiongozi mkuu wa nchi, ambaye pia ni mama?
 

Tatizo mnapenda kuiga mila na desturi ambazo haziendani na jamii yetu. Huwezi kumuambia mtu mzima vile, halafu utegemee kuungwa mkono. Hata ukiwa na hoja nzuri namna gani, lkn ukaileta kipumbavu vile, halafu uchekelewe.
 
Je wewe unaona hiyo ni namna nzuri ya kumuambia kiongozi mkuu wa nchi, ambaye pia ni mama?
Mdude ana stress zake na wala si msemaji wa chama chao. Kikubwa ni nini kinacholeta mkinzano huu ?! Ni uamuzi mbaya wa mama kuwakatalia wananchi hitaji lao. Tena akiwa anazuia vyama vingine kujieneza . Moja kati ubovu wa katiba iliopo. Anataka wabunge na madiwani ndiyo wafanye siasa kwa sasa . Huku akijua walivyopora chaguzi zote zilizopita . Wamehakikisha wapinzani wao hawaongozi mtaa, kata, wala Jimbo . Sasa vitafanyaje siasa za kujieneza ?!

Mama ashauriwe vizuri. Unakuwa kiongozi wa wote wanaokukubali na kukupenda, na wale wanaokuchukia na kukupinga .
 
Kama hamtaki kukosolewa ekeni mfumo wa chama kimoja, kazi kushabikia upumbavu tu, unaona ni sawa mashekhe kuekwa ndani bila hatia basi subiri siku mzee wako aje kuekwa ndani na serikali ya ccm ndio akili zitakukaa sawa
 
Kama hamtaki kukosolewa ekeni mfumo wa chama kimoja, kazi kushabikia upumbavu tu, unaona ni sawa mashekhe kuekwa ndani bila hatia basi subiri siku mzee wako aje kuekwa ndani na serikali ya ccm ndio akili zitakukaa sawa

Nyie endeleeni kumtumia kama chambo. Kwa hiyo huo upumbavu anaoongea ndiyo namna bora ya kufanya suala la katiba lipewe kipaumbele!!?
 
Ni dhahiri Chadema wamechagua upande wa wafanya siasa UCHWARA.

Huwezi kujenga chama chako kwa kuwatumia vijana wasio na akili na maarifa.

Kwa style hiyo ya kuwatumia vijana kichwa mchunga Chadema inakwenda kupotea kwenye uso wa siasa za Tanzania.

Ali Mkwavingwa
 
Tangu lini mchanga aondoke CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…