Mechi gani ya Watani wa jadi (Simba na Yanga) unaikumbuka zaidi?

Mechi gani ya Watani wa jadi (Simba na Yanga) unaikumbuka zaidi?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Habari zenu wakuu,

Leo katika pita pita zangu katika mtandao wa YouTube nikakutana na vipande vinavyoonesha mechi mbalimbali za Simba na Yanga. Nikiwa kama mdau ma mfuatiliaji wa soka la nyumbani mara nyingi huwa naona mechi zinazoikutanisha Miamba hii ya soka nchini huwa zinakosa mvuto kutokana na kukamiana sana.

Kwa kusema haya, haimaanishi mechi zote wanazokatana Timu hizi huwa zinakosa mvuto. Binafsi licha ya kupenda sana soka huwa napenda sana kitu tunaita 'COMEBACK' au kwa kiswahili cha kisoka tunaita 'kuchomoa'. Kwahiyo, miongoni mwa mechi pekee zilizonivutia ni ile ya "Kichuya Kona" na ile ya Yanga 3 na Simba tatu kwa sababu zilionesha maana halisi ya Mpira dakika tisini.

Vipi kwa upande wenu wanasoka wenzangu gemu ipi ya Watani wa Jadi unaikumbuka na ilikuvutia zaidi? inakukumbusha nini gemu hiyo?

Nini unakiona katika mechi ijayo kati ya miamba hii?

Karibuni tujadili wazee wenzangu.
 
Mechi ya 1962, hii mpaka leo inabaki kuwa mechi ya kihistoria haijawahi tena kutokea katika soka
 
Hahaha Mkuu wewe inaonekana Simba damu. sema kuna raha sana timu yako ikipata ushindi mnono katika hio gemu. mi napendaga piga nikupige yani

Ile game I think it was 1994, naikumbuka sana kwa sababu 1993 yote Yanga walitutesa kupitia Kizota na Lunyamila.

Sasa siku ile George Masatu ndo alianza kufunga, Kimanda akarudisha. Tukaja kumaliza na goli 4, nakumbuka tulizunguka mji mzima tunashangilia.

Nilirudi home saa 6 usiku, mama akagoma kunifungulia, dingi anauliza nilikuwa wapi nikamwambia. Akasema ingia ndani, bila zengwe.
 
Ile game I think it was 1994, naikumbuka sana kwa sababu 1993 yote Yanga walitutesa kupitia Kizota na Lunyamila.

Sasa siku ile George Masatu ndo alianza kufunga, Kimanda akarudisha. Tukaja kumaliza na goli 4, nakumbuka tulizunguka mji mzima tunashangilia.

Nilirudi home saa 6 usiku, mama akagoma kunifungulia, dingi anauliza nilikuwa wapi nikamwambia. Akasema ingia ndani, bila zengwe.

Ile mechi ya 4-1 iliuzwa...Wale wafanyabiashara wa kiasia waliokuwa wamejazana Yanga kwa madai ya kuifadhili walikula njama kwa lengo la Yanga ifungwe ili George mpondela ''Castro' aliyekuwa madarakani kama Katibu Mkuu ang'oke madarakani...'Castro' alikuwa hataki Yanga ijiegemeze kwa wafayabiashara hao wa kiasia.

Hii ni sawa na mechi ya 5-0 ambapo mfanyabiashara mmoja wakiwemo baadhi ya vizee vya Yanga walikula njama Yanga ifungwe nyingi ili mwenyekiti Nchunga ang'oke madarakani na alifanya hivyo baada ya kichapo hicho ...Mechi ya kihistoria ya Yanga na Simba ni ile ya mwaka 1974 pale Nyamagana Mwanza ambapo Simba alilala 2-1. Wafungaji Yanga ni Gibson Sembuli na Sunday Manara na Simba ni Adam Sabu.

Mechi hii ilichezwa dakika 120 ...Sunday alifunga goli la 2 kwenye dakika za nyongeza ...Yaani kwenye dakika 15 za mwanzo za nyongeza. Sembuli alisawazisha dakika ya 87. Adam Sabu alifunga goli la Simba kipindi ha kwanza kati ya dakika 16 na 20....Hiyo ndiyo ilikuwa game ya ukweli.

Simba walilalamika kwa goli la Sembuli wakidai kuwa alifunga wakati dakika 90 zimemalizika ...waliwasilisha malalamiko hadi CAF lakini haikusaidia kitu...ukweli goli lile lilifungwa ndani ya dakika 90....Mechi hii ilikuwa na hisia kali sana miongoni mwa mashabiki wa timu zote mbili.

Yanga ilikuwa ikiigaraza Simmba kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1972. Na mwaka 1973 Simba ilijikomboa kwa kuifunga yanga goli 1-0 goli lililofungwa na Willy Mwaijibe kama sijakosea..kumbukumbu zinanitupa kidogo inawezekana ni Haidari Abeid.

Mwaka 1974 timu zote mbili zikajiandaa vilivyo..Kabla ya michuano ya ubingwa kuanza Simba ikaenda Poland kwa mazoezi Yanga nayo ikaenda Romania ...Ikawa ni vita...Yanga anataka kuifunga Simba akidai kuwa simmba ilibahatisha tu mwaka 1973...Simba nayo ikaona kuwa ni lazima iendeleze kichapo kwa Yanga.

Siku ya mechi pale Nyamagana nchi ikasimama...masikio ya mamilioni ya mashabiki wa pande zote mbili yakaelekezwa Mwanza. Kulikuwa hakuna TV watu wanasikiliza kupitia RTD na viredio vvya dudu proof...betri za redio kabla ya mechi zikawa zinaanikwa ili kuongeza nguvu.

Baada ya game wapenzi kadhaa wa Simba waliripotiwa kujinyonga na kufa kukwepa muendelezo wa masimango mitaani..kwa mfano kule Tabora mnazi mmoja wa Simba aliamua kujitumbukiza kwenye pipa la pombe aina ya kangara iliyokuwa jikoni.

Baadhi yetu tulikuwa wanafunzi sekondari na wakati wa mechi hiyo tulikuwa likizo...sasa shule zilipofunguliwa baadhi ya wanafunzi manazi wa Simba walichelewa kuja shuleni kukwepa kejeli za manazi wa Yanga. Mchezo ule ulitungiwa kitabu na goli la kusawazisha la Sembuli likawa kwenye mchoro kitabuni kuelezea namna lilivyofungwa...Kama sijakosea mwandishi wa kitabu kile aliitwa Hadji Konde.

Nakummbuka Sembuli alifunga goli lile kwa pasi ya Kichwa ya Kitwana Manara ....Aisee ilikuwa raha sana...Kwangu mimi haitatokea mechi kama ile iliyojaa hisia kali..Katika mechi ile ya Nyamagana mchezaji nyota wa Simba, Saad Alli.

alizirai uwanjani dakika za mwanzo kabisa na kukimbizwa hospitali ya mkoa wakati ule nadhani ni Sekou Toure pale Mwanza....ilikuwa ni katika dakika za mwanzo kabisa za mchezo...Mengi yalisemwa kuhusu kuzirai kwa Saad Alli wengi wakihusisha na imani za ushirikina... .
 
Historia inaonyesha mechi kali ni ile ya 1987 marehemu Sahau Kambi akiwabeba mikia wasishuke daraja na Fred Felix Minziro akimshushia kipigo cha mbwa mwizi Kambi
 
Ile game I think it was 1994, naikumbuka sana kwa sababu 1993 yote Yanga walitutesa kupitia Kizota na Lunyamila.

Tukaja kumaliza na goli 4, nakumbuka tulizunguka mji mzima tunashangilia.

Nilirudi home saa 6 usiku, mama akagoma kunifungulia, dingi anauliza nilikuwa wapi nikamwambia. Akasema ingia ndani, bila zengwe.
Umekula chumvi!

Shikhamoo Mkuu, habari za jumapili?
 
Mpambano naona kila mmoja ana mnadi mwenzake!
Ila tunachojua ni kua kuchukua point 3 au hata hiyo 1 anfield si rahisi.

Mwaka jana Almanusura waondoke na 3 points kama siyo Mahrez kupaisha penati.

Nahisi Pep ataendeleza utaratibu wake wa kucheza kwa counters akikutana na Liverpool.

Ngoja tuone itakuwaje.
 
Ile mechi ya 4-1 iliuzwa...Wale wafanyabiashara wa kiasia waliokuwa wamejazana Yanga kwa madai ya kuifadhili walikula njama kwa lengo la Yanga ifungwe ili George mpondela ''Castro' aliyekuwa madarakani kama Katibu Mkuu ang'oke madarakani...'Castro'...
Duuh mzee heshima yako! Wenzetu mlifaidi kuona vipaji halisi kipindi hichoi! Siku hizi msisimko wa pambano la watani wa jadi umepungua sana! Mzee tukumbushe na ile simba aliyotia mpira kwapani!
 
Back
Top Bottom