Duuh mzee heshima yako! Wenzetu mlifaidi kuona vipaji halisi kipindi hichoi! Siku hizi msisimko wa pambano la watani wa jadi umepungua sana! Mzee tukumbushe na ile simba aliyotia mpira kwapani!
hahahahahaha ile game nilikuwepo uwanjani uwanja wa taifa sasa uwanja wa Uhuru...Yanga ilikuwa na kikosi kikali sana...Akina Sanifu Lazaro na wengineo..Simba nayo ilikuwa na vijana wazuri lakini kiukweli Simba walikuwa underdog kwa Yanga...Simba katika game ile kipindi cha kwanza walicheza rafu za ajabu na za kushangaza lakini hakuna kadi nyekundu iliyotolewa kwa mshangao wa wengi...Refa alikuwa ni Hafidh kutoka Zanzibar sasa ni marehemu ...wakati anafariki alikuwa ni Mbunge....Kipindi hicho cha kwanza mpira ulikuwa unachezwa kwenye lango la Simba lakini matokeo bado yalibaki 0-0 na hakuna kadi iliyotolewa kwa Simba pamoja na rafu za ajabu...Kepteni wa Simba alikuwa nadhani ni Method Mogella akicheza namba nane...msimu uliofuatia Method alihamia Yanga ambako alikuwa anacheza namba 4 au 5...sasa katika game ile Simba wakagoma kuingia uwanjani kipindi cha pili...Ilifahamika baadaye kuwa Simba walikuwa wanafanya rafu makusudi ili wapewe kadi nyekundu na iwe ndiyo sababu ya wao kususia mechi kwa kisingizio cha kuonewa...Ilifahamika baadaye kuwa refa aligundua janja hiyo ya Simba na ndiyo maana akawa hawapi kadi....Na habari ambazo hazijathibitishwa zinasemma kuwa ndani ya uwanja Hafidhi aliwaambia wachezaji wa Simba kuwa hatawapa kadi nyekundu ila watafungwa tu kihalali...Kiukweli Simba walizidiwa mno game ile na wangerudi tu uwanjani wangepigwa nyingi...hawakuingia uwanjani kipindi ha pili kukwepa aibu ya kufungwa.....